Wakuu,
Kuna vitu vinakasirisha kwa kweli iko hivi,
Mimi ni mteja mwaminifu wa huduma ya maji mtaani kwetu,na ni miongoni mwa watu wanaotumia maji bombani kwa kiasi kikubwa
Mtakubaliana na Mimi kuwa serikali kupitia wizara ya maji imeajiri watu wale wa kuunganisha maji kwa wateja na wakapewa pikipiki kwa ajiri ya kazi hiyo
Cha ajabu na Cha kushangaza Jana walikuwa na operation ya kubaini wadaiwa sugu ili kuwakatia maji
Walipofika ktk mita yangu wakasema nadaiwa kiasi Cha 1750 hivyo wanakata maji na ili kuunganishiwa ni mpaka nilipe faini ya TSH 15000
Nikawaambia Mimi sijashindwa kulipa Deni Hilo na nikichekelea kulipa so kwa maksudi Bali ni kujisahahau tu na nalipa punde isitoshe Mimi ni mteja mwaminifu kwa Nini mnikatie kids kiasi kidogo Cha pesa?
Watumishi wakakata maji na
Kuondoka,kwa vile Nina uhitaji wa maji hayo kwa sana ikanibidi niwaite tena waniunganishie,watumishi wakaja nikalipa elfu 15000 wakaniunganishia
Sijaelewa utaratibu wa wizara ya maji kwamba mtu anadaiwa 1750 unakatiwa na kurudishiwa na ili urudishiwe ni mpaka utoe faini
Wizara ya maji naombeni ufafanuzi juu ya hili