Nimekoma mimi, katu, katu, katu usitangaze matarajio yako mazuri

Nimekoma mimi, katu, katu, katu usitangaze matarajio yako mazuri

Pengine umeepushwa na vitu vingi kwa hilo dili unahisi lingekutoa, wait bro Mungu anatujua kabla yakutuweka hapa. Pengine kuna fursa kubwa inakuja hii ilikuwa nikukujengea misuri ya kuiishi hiyo future opportunitie
 
Kweli ni muhimu kukaa kimya hadi jambo lako litimie kwa sababu kunazuia watu wasiokutakia mema kuliharibu. Pia hukupa nafasi ya kulifanya kwa utulivu bila presha ya maoni ya nje. Mimi nilifanya interview ya kazi basi nikasema hata simuambii mtu nikafanikiwa kupita interview zote sasa nilivyopata email ya kwamba nimepata kazi nisubiri offer letter ndani ya siku tatu itakuwa imetumwa, aisee nilishindwa kuvumilia nikapigia simu baadhi ya watu wangu wa karibu kuwapa habari njema 😁, offer letter inakuja kutumwa majukumu ya kazi na mshahara ni mbingu na ardhi basi ikabidi tubargain lakini waliongeza kidogo tuu, kazi ni ngumu nikasema siwezi fanya kwa huo mshahara ni exploitation. Deal likawa limekufa hivyo 😭
 
Ndugu zangu naandika huku natememeka, kulia nataka kucheka nataka yaani kiufupi sijielewi,

Nilikua nikisikia sana watu wakisema usiseme mipango yako, usiamini watu hata akiwa mzazi wako, watu wanatia nuksi, vijicho, husda kiukweli hiyo misamiati kwangu ilikua haipo kabisaaaaaaaa ila sasa nimeamini,

Ishu ilikua hivi, nilirusha ndoano mahali, nikawa nasubiri samaki anase sasa kile kipindi nasubiri samaki anase si ndio nikawaambia wazazi bhana, niombeeni dua nzito mwanenu nikifanikiwa hili baaasi nawapeleka Paris kwanza mkale bata la kifaransa dah mama yangu asimwambie mwanae kipenzi na mwanae kipenzi asimwambie nduguye kipenzi, habari zikasambaa kama moto wa petrol nikavutiwa waya na ndugu zangu vipenzi nikaulizwa ulizwa wee wote walikua na furaha juu yangu, ila kiwango cha pesa sikuwaambia pia mazingira halisi ya jinsi itakavyopatikana nayo sikuwaambia, so wakaniombea duaa nzito, maisha yakaendelea, ila sasa simu kila mara naulizwa kama tayari, pesaaaa🙌🏻

Kwenye ndoano yangu akanasa samaki mkubwa kuliko hata matarajio yangu, tukaanza mchakato stahiki, saini documents kama zote, wakuu tarehe 28/05/2025 maisha yangu yalikua yabadilike, new milionea in town 😎 mara paaaaaap! kibao kikageuka tena kimegeuka mazimaaaa deal off hata sababu haieleweki, yaani nilichanganyikiwa almanusura nizimie,

Nimeapa, mimi Mariposa bin Posa bin Mari nikiwa na jambo langu tena hata sikio la pili halitajua, hata mkono wa pili hautajua, SIRI, SIRI, SIRI,
Sijasema familia yangu imeniwekea kauzibe, ila ninachoona jambo lilijulikana na watu kwa haraka ikaweka husda na kijicho,

Wakuu siko sawa kabisa kila nikikumbuka moyo unalipuka sana😭😭😭😭
I learnt this thing in hard way kilichobaki mipango ni yangu peke yangu siamini mtu. Matokeo ndio yatasema yenyewe. Fanya kimyakimya waone matokeo. Sisemi mipango yangu, sipost chochote kinachohusu maisha yangu never. Sisemi ideas zangu, watu wanachukua wanafanyia kazi wananiona fala. Nikipata idea nzuri au fursa ya kuifanyia kazi naandika kwenye notebook yangu muhimu. Naendelea kusubiri implementation.

Niliwahi tengeneza in cash flow moja ya hatari. Kosa nilipokea mgonjwa nyumbani ambaye ndugu na marafiki walikuwa wanamtembelea kumuona it was a mistake of my life. I wish ningemhudumia huko aliko.
Kwa sasa ndugu nasaidia huko waliko ila nyumbani kwangu hapana. Mambo ni mengi

Nakuelewa unachopitia. Tuliza kichwa kubali lililotokea na jipange kwa mipigo mingine mikubwa.
 
Ukitaka mambo yako yasiwe na kiwingu kuwa msiri tu, japo mengne hayahitaji usiri, waje waone matokeo tu.

Mim pia iliniponza, nilijikusanya mwaka jana nikapanga huu mwaka ukianza niwe na biashara x nitulie nianze kulia kimvulin.
Ukienda kwa ndugu wanakupeleleza kinoma maisha yako, ila mim nikawa mkwel nawambia mipango yangu.
Aise saiv cjui ata mtaji umeishia wapi, matatzo yanakusonga unapukutika daa.
Ila ukiisha tu matatizo nayo yanakomea hapohapo.

Afu kibaya zaidi mda huo dem ata ukimjaribu tu hakatai, japo mim sio mtu wa madem msululu. mkibadilishana namba yey ndo atahangaika kukutafta.

Salini sana Mungu yupo, kama kuoga dawa ogeni sana.
MAFANIKIO SI LELEMAMA
 
Ukitaka mambo yako yasiwe na kiwingu kuwa msiri tu, japo mengne hayahitaji usiri, waje waone matokeo tu.

Mim pia iliniponza, nilijikusanya mwaka jana nikapanga huu mwaka ukianza niwe na biashara x nitulie nianze kulia kimvulin.
Ukienda kwa ndugu wanakupeleleza kinoma maisha yako, ila mim nikawa mkwel nawambia mipango yangu.
Aise saiv cjui ata mtaji umeishia wapi, matatzo yanakusonga unapukutika daa.
Ila ukiisha tu matatizo nayo yanakomea hapohapo.

Afu kibaya zaidi mda huo dem ata ukimjaribu tu hakatai, japo mim sio mtu wa madem msululu. mkibadilishana namba yey ndo atahangaika kukutafta.

Salini sana Mungu yupo, kama kuoga dawa ogeni sana.
MAFANIKIO SI LELEMAMA
HATARI SANA
 
Umeacha mbachao Kwa msara upitao


Apa wabetting tunasema over 0.5 imechana
Pole mkuu
Kazi ya kifua kutunza Siri na ndo mana wakat unazaliwa ulikuja peke yako jifunze ilo
 
Back
Top Bottom