Nimekoma mimi, katu, katu, katu usitangaze matarajio yako mazuri

Nimekoma mimi, katu, katu, katu usitangaze matarajio yako mazuri

Pole sana madam,

Kutunza Siri zako hasa your next move, plan, au mipango yoyote ni vzr sana.

wengi wetu tuna wivu, vijicho husda, hapo mtu Hana hata uchawi...

wengi wanatuchekea usoni Ila moyoni wivu unawazonga.
 
ndio maana wasiojulikana wakina muriro,igp,waziri na raisi wanataka iwe siri ili msijue chupi zao kuwa zina matobo
 
Pole sana, unapaswa kukabidhi mipango yako kwa Mungu, ukiwa na Mungu vizuri, hakuna kinachoweza kuzuia. Tuna mifano mingi kwenye biblia, Yusuf alisema ndoto yake, alipata changamoto nyingi, ila hakuna kilichozuia ndoto yake.
 
Kama imepangwa iwe yako ni yako tu hata ukisema au usiposema itabaki kuwa yako.
Ukiona hujapata jua tu haikua bahati yako.
Japo siri nayo inahusika! Ila kama kitu alipanga Mungu kiwe chako inamaanisha ameshakuandaa kitakua..

"Kun faya Kun"
 
Pole sana, unapaswa kukabidhi mipango yako kwa Mungu, ukiwa na Mungu vizuri, hakuna kinachoweza kuzuia. Tuna mifano mingi kwenye biblia, Yusuf alisema ndoto yake, alipata changamoto nyingi, ila hakuna kilichozuia ndoto yake.
Tupe mifano Mengine ambao ijapokua walisema mipango yao ila ilitimia kwa kuwa ilikua ni kusudi la Mungu.
 
Ndugu zangu naandika huku natememeka, kulia nataka kucheka nataka yaani kiufupi sijielewi,

Nilikua nikisikia sana watu wakisema usiseme mipango yako, usiamini watu hata akiwa mzazi wako, watu wanatia nuksi, vijicho, husda kiukweli hiyo misamiati kwangu ilikua haipo kabisaaaaaaaa ila sasa nimeamini,

Ishu ilikua hivi, nilirusha ndoano mahali, nikawa nasubiri samaki anase sasa kile kipindi nasubiri samaki anase si ndio nikawaambia wazazi bhana, niombeeni dua nzito mwanenu nikifanikiwa hili baaasi nawapeleka Paris kwanza mkale bata la kifaransa dah mama yangu asimwambie mwanae kipenzi na mwanae kipenzi asimwambie nduguye kipenzi, habari zikasambaa kama moto wa petrol nikavutiwa waya na ndugu zangu vipenzi nikaulizwa ulizwa wee wote walikua na furaha juu yangu, ila kiwango cha pesa sikuwaambia pia mazingira halisi ya jinsi itakavyopatikana nayo sikuwaambia, so wakaniombea duaa nzito, maisha yakaendelea, ila sasa simu kila mara naulizwa kama tayari, pesaaaa🙌🏻

Kwenye ndoano yangu akanasa samaki mkubwa kuliko hata matarajio yangu, tukaanza mchakato stahiki, saini documents kama zote, wakuu tarehe 28/05/2025 maisha yangu yalikua yabadilike, new milionea in town 😎 mara paaaaaap! kibao kikageuka tena kimegeuka mazimaaaa deal off hata sababu haieleweki, yaani nilichanganyikiwa almanusura nizimie,

Nimeapa, mimi Mariposa bin Posa bin Mari nikiwa na jambo langu tena hata sikio la pili halitajua, hata mkono wa pili hautajua, SIRI, SIRI, SIRI,
Sijasema familia yangu imeniwekea kauzibe, ila ninachoona jambo lilijulikana na watu kwa haraka ikaweka husda na kijicho,

Wakuu siko sawa kabisa kila nikikumbuka moyo unalipuka sana😭😭😭😭
 
Joke aside, pole Dokta hopefully mawazo hayajaathiri mfumo wa maziwa anko angu akashindwa kunyonya 🥺🤠
 
Back
Top Bottom