Nimekonda sana, naomba ushauri nifanyaje nirudishe kilo zangu haraka

Kula unachojisikia, achana na ratiba ya wali nyama etc.

Kunywa maziwa kila asubuhi nusu lita

Baada ya chakula tafuna cheese (tafuta cheddar cheese), itasaidia kujaza tumbo. Vumilia ladha.

Nilifanya haya kuongeza uzito
 

queenkami haya magonjwa hapa mbona yanawezekana kukuletea uzito kupungua, Je umeshayapatia matibabu-ukapona?
 
Kula unachojisikia, achana na ratiba ya wali nyama etc.

Kunywa maziwa kila asubuhi nusu lita

Baada ya chakula tafuna cheese (tafuta cheddar cheese), itasaidia kujaza tumbo. Vumilia ladha.

Nilifanya haya kuongeza uzito
Asante kwa ushauri mkuu.
Nitazingatia na cheddar cheese mimi naipenda.

Uliongezeka kg ngapi mkuu baada ya muda gani?
Barikiwa sana.
 
Muulize yule Prof anayetaka wote tukonde kama wanywa gongo.
 
Hayo magonjwa yote yamepona mkuu kasoro ACID REFLUX,huo ninao toka niko mtoto,hauna tiba so far. Haujawahi kunikondesha.
 
Kwa kimo hicho (164) ongeza, kilo 2 tu unakuwa kwenye normal bmi ya 19.

Zingatia tu lishe, fasta sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…