Nimekosa ujasiri kwenye hili

Nimekosa ujasiri kwenye hili

Una kitu tunaita inferiority complex, unajiona duni mbele yake kwa sababu amekuzid umri na uwezo kifedha. Wengi wetu, wanaume, hukosa ujasiri mbele ya mwanamke wa aina hiyo. Sababu kubwa ni tamanio la kimaumbile lililowekwa ndani yetu kumuongoza mwanamke na tunafikiri ili kuweza kufanya hivyo lazima uwe na pesa kumzidi na umri mkubwa kuliko yeye.

Pesa na umri ni catalyst lakini sio msingi wa hierarchy ya kiuongozi hasa kwenye mahusiano. Akili, ufahamu wa kutosha, maono na namna unavyojitazama ndo msingi. Kwa hiyo jitazame hapo, unaweza kuwa na umri mdogo kwa namba lakini ukawa na uwezo wa kufikiri na kutenda kwa uwezo mkubwa kulinganisha na vijana wa umri wako. Usijione duni, Jiamini, tafuta maarifa, kutana na watu sahihi and be a good man. Huyo mwanamke ana akili mnaweza kufanya maisha vizuri ukitulia.
Shukran sanaaa boss, umenipa ushauri wa kina. Kwel kuna mda najisikia low hasa tukijadili mipango ya mda mfupi ambayo mwishoni inataka pesa. Ila kuna mda anakuwa mzito nikimpatia ushauri zaidi kuhusu ujenzi.
 
Asante kwa ushaur boss. Na io nyumba vipi? Yan ni play kivipi hapo? Tuchangie nguvu tu au na pesa?
Acha akili za kimaskini wewe ni MWANAUME Malizia nyumba hiyo, nunua kiwanja/viwanja jenga zingine, kama hutakua na amani kukaa hapo hakikisha unajenga kwingine hiyo mtapangisha mwanaume ndio mwenye maamuzi.

Usiwe na mawazo ooh kwamba mwanamk ana hela au laa fanya maendeleo usije ukaacha mtu anayejiweza kwenda kukimbilia tegemezi changa karata zako vizuri mtu anayejiweza kuna mgawanyo wa majukumu na hapa utajiri ndo upo.

Mwanamke kama huyo huwazi vitu vidgo vidgo unawaza mambo makubwa makubwa tu sasa wewe muache utajuta atapata mtu mwingine mwenye kujitambua wataenda sawa.

Kama unamucha naomba namba zake🙏.
 
Ogopa pesa ya mwanamke weww
Natumaini ni wazima wa afya na poleni na majukumu.

Niingie kwenye mada.

Mimi ni mwanaume nina miaka 24, najishughulisha na kazi binafsi Ila bado kipato changu sio kikubwa. Miezi michache iliyopita nilifanikiwa kuwa na mahusiano na binti mrembo na muonekano wake ni kama ana miaka 20 hivi.

Nilimueleza ya moyoni akanielewa saivi tupo kwenye mahusiano. Sikujua kumbe binti ana kazi nzuri ameajiriwa kaka yake na kipato kikubwa tu anapata. Miaka yake ni 26 Ila kimuonekano ni mdogo, juzi kanambia tuende mahali kumbe ni kununua materials ya kupeleka site, kumbe ana eneo na nyumba msingi umeanza.

Tukienda mahali hata pesa za manunuzi ananikabidhi na akiwa busy ananiomba nikasimamie mafundi. Nashindwa kuwa na ujasiri wa kuchangia ujenzi naomba ushauri halafu pia wakuu hili ni zali au nikimbie tu nimuache na projects zake.
 
Kuchangia sio lazima materially, hata mawazo yako na kujitoa inaweza kuwa mchango mkubwa. Kikubwa shikamana...... tupilia mbali dramas, maisha ni haya haya and we only live once.
 
Sikia ndugu uyo binti nipe namba yake nimuulize kitu cha muhimu sana, anayway ni hivii fanya umpe ujauzito uyo alafu tafuta ela kwa nguvu zote bila ivyo utakuja kudhalilika pia jutahid usicheat akajua
😅😅 Ukikutana na mrembo ambae hujawai kumuona ndio yeye basi muombe namba. Kwenye kutafuta pesa io naongeza juhudi boss ila kwenye mimba anajielewa sanaa akiwa kwenye danger hata meeting na Mimi hataki anadai mtoto hadi ndoa
 
Mkuu una malengo naye? kama ndiyo, basi akimaliza mkakaa hapo usiishi hiyo nyumba kwa muda mrefu mkuu, jipange mkioana mkaishi ulipojenga wewe hata kama ni nyumba ya mabati, usikae sana hapo kwake pakiisha, nimekukanya
Malengo nae yapo nampenda and she loves me io sifichi ndio mana hata pesa ya kazi anaweza nipa nifuate vitu na kusimamia nikiwa free. Sawàaa mkuu kwa busara, sasa nichangie pesa kidogo ninayo pata tukamilishe au nguvu tu na mawazo nimuache ajenge yeye pekee?
 
Ukishampenda mtu maana yake ni mrembo kwako. Kwa wengine inaweza isiwe hivyo. Kwa hivyo haina maana ya kueleza kuwa ni mrembo.
Miezi michache iliyopita nilifanikiwa kuwa na mahusiano na binti mrembo na muonekano wake ni kama ana miaka 20 hivi.
 
Malengo nae yapo nampenda and she loves me io sifichi ndio mana hata pesa ya kazi anaweza nipa nifuate vitu na kusimamia nikiwa free. Sawàaa mkuu kwa busara, sasa nichangie pesa kidogo ninayo pata tukamilishe au nguvu tu na mawazo nimuache ajenge yeye pekee?
Usiingize pesa kwenye mradi wa mwanamke, ungekuwa na ndoa naye sawa lkn sasa ukitoa iwe umempa tu kama sapoti ya kirafiki lkn usiweke pesa yako kama kitu chenu wote.

Waogope sana wanawake kwenye vitu vyao...ipo siku utanielewa
 
Natumaini ni wazima wa afya na poleni na majukumu.

Niingie kwenye mada.

Mimi ni mwanaume nina miaka 24, najishughulisha na kazi binafsi Ila bado kipato changu sio kikubwa. Miezi michache iliyopita nilifanikiwa kuwa na mahusiano na binti mrembo na muonekano wake ni kama ana miaka 20 hivi.

Nilimueleza ya moyoni akanielewa saivi tupo kwenye mahusiano. Sikujua kumbe binti ana kazi nzuri ameajiriwa na kaka yake na kipato kikubwa tu anapata. Miaka yake ni 26 Ila kimuonekano ni mdogo, juzi kanambia tuende mahali kumbe ni kununua materials ya kupeleka site, kumbe ana eneo na nyumba msingi umeanza.

Tukienda mahali hata pesa za manunuzi ananikabidhi na akiwa busy ananiomba nikasimamie mafundi. Nashindwa kuwa na ujasiri wa kuchangia ujenzi naomba ushauri halafu pia wakuu hili ni zali au nikimbie tu nimuache na projects zake.
Ushaolewa ww...
 
Umeombwa uchangie unasita ama unataka kujiongeza tu akuone muwajibikaji??

Ushauri wangu jikune unapoweza kufikia, ila usilazimishe eti akuone unajali mwisho ulete uzi mwingine hapa kua umemjengea bado ukaachwa.

Kama haiathiri kipato chako si mbaya kumsaidia hapa na pale, na si lazima pesa hata muda wako na mawazo yako ni muhimu sana mkuu. Jiamini kama unatoa toa kama hutoi usitoe, ukiwa na msimamo mmoja kati ya hiyo utakua safe sana.
 
Kuchangia sio lazima materially, hata mawazo yako na kujitoa inaweza kuwa mchango mkubwa. Kikubwa shikamana...... tupilia mbali dramas, maisha ni haya haya and we only live once.
sawa mkuu asante kweli nishikame Ila nisisahau kujiweka sawa pia🙏
 
Umeombwa uchangie unasita ama unataka kujiongeza tu akuone muwajibikaji??
Alisema tupambane tukamilishe nyumba alafu tuanzishe familia ila Kuna mda vitu vidogo vinapelea na nipo karibu mafundi wakinicheki inakuwa mtihani kwamba nifix au nimwambie Ila kipato chake ni kikubwa Sanaa kufananisha na changu, ushauri wako ni mzuri asante boss.
 
Back
Top Bottom