Nimekosa ujasiri kwenye hili

Shukran sanaaa boss, umenipa ushauri wa kina. Kwel kuna mda najisikia low hasa tukijadili mipango ya mda mfupi ambayo mwishoni inataka pesa. Ila kuna mda anakuwa mzito nikimpatia ushauri zaidi kuhusu ujenzi.
 
Asante kwa ushaur boss. Na io nyumba vipi? Yan ni play kivipi hapo? Tuchangie nguvu tu au na pesa?
Acha akili za kimaskini wewe ni MWANAUME Malizia nyumba hiyo, nunua kiwanja/viwanja jenga zingine, kama hutakua na amani kukaa hapo hakikisha unajenga kwingine hiyo mtapangisha mwanaume ndio mwenye maamuzi.

Usiwe na mawazo ooh kwamba mwanamk ana hela au laa fanya maendeleo usije ukaacha mtu anayejiweza kwenda kukimbilia tegemezi changa karata zako vizuri mtu anayejiweza kuna mgawanyo wa majukumu na hapa utajiri ndo upo.

Mwanamke kama huyo huwazi vitu vidgo vidgo unawaza mambo makubwa makubwa tu sasa wewe muache utajuta atapata mtu mwingine mwenye kujitambua wataenda sawa.

Kama unamucha naomba namba zake🙏.
 
Ogopa pesa ya mwanamke weww
 
Kuchangia sio lazima materially, hata mawazo yako na kujitoa inaweza kuwa mchango mkubwa. Kikubwa shikamana...... tupilia mbali dramas, maisha ni haya haya and we only live once.
 
Sikia ndugu uyo binti nipe namba yake nimuulize kitu cha muhimu sana, anayway ni hivii fanya umpe ujauzito uyo alafu tafuta ela kwa nguvu zote bila ivyo utakuja kudhalilika pia jutahid usicheat akajua
😅😅 Ukikutana na mrembo ambae hujawai kumuona ndio yeye basi muombe namba. Kwenye kutafuta pesa io naongeza juhudi boss ila kwenye mimba anajielewa sanaa akiwa kwenye danger hata meeting na Mimi hataki anadai mtoto hadi ndoa
 
Mkuu una malengo naye? kama ndiyo, basi akimaliza mkakaa hapo usiishi hiyo nyumba kwa muda mrefu mkuu, jipange mkioana mkaishi ulipojenga wewe hata kama ni nyumba ya mabati, usikae sana hapo kwake pakiisha, nimekukanya
Malengo nae yapo nampenda and she loves me io sifichi ndio mana hata pesa ya kazi anaweza nipa nifuate vitu na kusimamia nikiwa free. Sawàaa mkuu kwa busara, sasa nichangie pesa kidogo ninayo pata tukamilishe au nguvu tu na mawazo nimuache ajenge yeye pekee?
 
Ukishampenda mtu maana yake ni mrembo kwako. Kwa wengine inaweza isiwe hivyo. Kwa hivyo haina maana ya kueleza kuwa ni mrembo.
Miezi michache iliyopita nilifanikiwa kuwa na mahusiano na binti mrembo na muonekano wake ni kama ana miaka 20 hivi.
 
Usiingize pesa kwenye mradi wa mwanamke, ungekuwa na ndoa naye sawa lkn sasa ukitoa iwe umempa tu kama sapoti ya kirafiki lkn usiweke pesa yako kama kitu chenu wote.

Waogope sana wanawake kwenye vitu vyao...ipo siku utanielewa
 
Ushaolewa ww...
 
Umeombwa uchangie unasita ama unataka kujiongeza tu akuone muwajibikaji??

Ushauri wangu jikune unapoweza kufikia, ila usilazimishe eti akuone unajali mwisho ulete uzi mwingine hapa kua umemjengea bado ukaachwa.

Kama haiathiri kipato chako si mbaya kumsaidia hapa na pale, na si lazima pesa hata muda wako na mawazo yako ni muhimu sana mkuu. Jiamini kama unatoa toa kama hutoi usitoe, ukiwa na msimamo mmoja kati ya hiyo utakua safe sana.
 
Kuchangia sio lazima materially, hata mawazo yako na kujitoa inaweza kuwa mchango mkubwa. Kikubwa shikamana...... tupilia mbali dramas, maisha ni haya haya and we only live once.
sawa mkuu asante kweli nishikame Ila nisisahau kujiweka sawa pia🙏
 
Umeombwa uchangie unasita ama unataka kujiongeza tu akuone muwajibikaji??
Alisema tupambane tukamilishe nyumba alafu tuanzishe familia ila Kuna mda vitu vidogo vinapelea na nipo karibu mafundi wakinicheki inakuwa mtihani kwamba nifix au nimwambie Ila kipato chake ni kikubwa Sanaa kufananisha na changu, ushauri wako ni mzuri asante boss.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…