Nimekosana na rafiki yangu baada ya kumdai pesa niliyomkopesha

Nimekosana na rafiki yangu baada ya kumdai pesa niliyomkopesha

Kutokumkopesha rafiki yako hela hua hawafundishi shule, wao wanasema yu kua na nidhamu ya hela basi.

Sass haya mengine tunafundishwa na mtaa. Alafu huyo sio rafiki ni mshikaji tu na ushkaji unakufa baada ya kuhamia kwenye issue zingine ila urafiki haufi isipokua tu kwenye masuala ya hela.
 
Mkuu, mtu akiamua kuacha tu jambo lipite haimaanishi hana cha kufanya. Miaka ya nyuma kabisa nilikuwa sitaki upuuzi kabisa. Niliwahi kumpasua jicho mtu sababu alinisumbua kunilipa. Nilishatia watu hasara sababu nawadai. Niliishia kufungwa tu. Niliamua kubadilika na kuwa mtu wa tofauti ila kumbe dunia haitaki watu wa aina ambayo nimekuwa mimi. Napotezea, sihitaji kurudi kule mkuu. Nimeamua kutosaidia mtu tu kivyovyote vile.
Mpk ukampasua hilo jicho hukutumia KY?
 
Huyo sio rafiki ako, alafu ondoa mentality ya kwamba ukiwa unamdai mtu ni kama unammiliki yeye mzima,kwamba inabid ajieleze asipopatkana,apokee simu yako,awe mpole et tu kwasababu ya wewe unamdai, wewe ukiona hakupi ushirikiano jua anamambo yake na yeye binafsi yamekwamisha sio lazma aanze kujielezea.

Endelea na mipango mingine, siku akipata ataleta hata ikipita mwaka, la pendekeza kumtumia sms kwamba kama mambo hayajakaa sawa asijal itanipa ukipata, alafu unaleta story zingine za maisha.

Hîi tabia ya kujifanya kupunguza marafiki ,kwa kuona wanashindwa kulipa kwa wakati , na kuwaona waswahili ni tabia ya umaskini sana, wenye akili za kitajiri hawana kabisa hii.
Tajiri wewe unadai pesa ngapi mpk sasa kwa marafikj?
 
...Wewe ni Mkopaji ??...Ndio Unavyofanyaga Ukiisha Kopa ?? ACHA...!

Sent from my TECNO BD4j using JamiiForums mobile app
 
Mshikaji wangu Mponda ukitaka akukopeshe laki anakupa elfu 50 anasema hiyo nimekupa tafuta kwingine elfu 50 maana nikikukopesha nitakuwa nimekupoteza hii principle nilijua utani kumbe ilikuwa inatuepusha na ugomvi kama wa mleta mada namimi nimeanza kuitumia kama sitakuwa nacho sikupi nikiwanacho sikukopeshi nakupa nusu au pungufu zaidi
 
Mkuu, mtu akiamua kuacha tu jambo lipite haimaanishi hana cha kufanya. Miaka ya nyuma kabisa nilikuwa sitaki upuuzi kabisa. Niliwahi kumpasua jicho mtu sababu alinisumbua kunilipa. Nilishatia watu hasara sababu nawadai. Niliishia kufungwa tu. Niliamua kubadilika na kuwa mtu wa tofauti ila kumbe dunia haitaki watu wa aina ambayo nimekuwa mimi. Napotezea, sihitaji kurudi kule mkuu. Nimeamua kutosaidia mtu tu kivyovyote vile.
Achana nae huyo kakosa shukrani
 
Mm ndio dawa ya hao watu ,sikia kwanza mtumie ujumbe wa kumuomba msamaha kwa kilichotokea na kumwambia urafiki wenu ni bora kuliko hiyo pesa, baada ya hapo mwambie utanilipa siku ukipata kuwa na amani muendelee na ratiba kama kawaida, akisahau siku ukionana nae mwambie akuazima cm yake kuna mtu unataka kumpigia na unahisi amekupiga pin kwenye namba yako, akikupa mwambie ngoja nikaongeze vocha kisha tembea mazimaaaaa, wakati unafanya hayo hakikisha zile sms za kudaiyana haujazifuta, ukichukua cm yake endelea na ratiba zako akikufuata mwambie alete pesa yako umpe simu yake, hata lain usimpe . Hii njia nimeitumia na nimelipwa na watu wengi ambao walidhamilia kutonilipa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulichofanyiwa the same na Mimi nilimkopesha jamaa yangu hela TZS.laki 3 toka sept,2023 simu zangu hakupokea hadi leo,SMS hajibu nikipiga kwa simu tofauti akijua ni Mimi anakata nimeamua kufuta namba zake zote za simu najua nimeppoteza hela ila atabaki na aibu mbaya zaidi kaenda kwenye kampuni za mikopo kaniweka Mimi mdhamini wake nikawapa ramani ya kumpata kazini kwake na namba ya bosi wake ili awajibishwe
 
Huyo sio rafiki ako, alafu ondoa mentality ya kwamba ukiwa unamdai mtu ni kama unammiliki yeye mzima,kwamba inabid ajieleze asipopatkana,apokee simu yako,awe mpole et tu kwasababu ya wewe unamdai, wewe ukiona hakupi ushirikiano jua anamambo yake na yeye binafsi yamekwamisha sio lazma aanze kujielezea.

Endelea na mipango mingine, siku akipata ataleta hata ikipita mwaka, la pendekeza kumtumia sms kwamba kama mambo hayajakaa sawa asijal itanipa ukipata, alafu unaleta story zingine za maisha.

Hîi tabia ya kujifanya kupunguza marafiki ,kwa kuona wanashindwa kulipa kwa wakati , na kuwaona waswahili ni tabia ya umaskini sana, wenye akili za kitajiri hawana kabisa hii.
Wewe utakua wale wadhulumaji wasio penda kulipa madeni ya watu sio kwa kauli zako hizo,.......jambo muhimu ni kuachana na marafiki omba omba kila wakati.
 
Kuna mchaga mmoja ilikuwa December kama hivi anataka kwenda kwao,kwanza nilimpa kama 50k kama free maana jamaa yupo intership ofisini ila analipwa.

Sasa siku hiyo hiyo mtu umempa pesa usiku ananipigia simu kapata tatizo anajitaji kama laki na hamsini...pale ofisini wapo ndugu zake kabisa wa huko kwao.

Nikawa najiuliza huyu jamaa ni vip nikamchenga achek kwa washkaji , siku ya pili usiku akasema sijui kwao hali mbaya yeye ndio kila kitu hamna wa kumpa kalalama kinoma mpaka roho ikaniuma.

Akaniambia mshahara ukitoka tu ananipa basi nikamtumia 150k ,huu jamaa alikuwa tapeli kinoma na mlevi...Ile pesa tangu mwaka huu sikupata hata mia naona mwaka wa tatu huu😂😂.

Ujinga wake ni mmoja ukimchek anakuambia nakutumia mda huu ngoja niende kwa wakal ,ila ndio basi hakupi hata upige simu na kazini anaingia .

Sijapata hata thumni mpaka kesho hii ndio mara ya mwisho kupigwa , nyingine nampa tu mapema kama ninayo kama laki nampa halafu namwambia haina haja ya kurudisha.
 
Back
Top Bottom