Nimekua disappointed sana na Mtu ambaye nilikua namuona wa thamani sana....ni week sasa Tangu nikutane na hio disappointment

Ishi ukijuwa kila mtu ni adui yako,ni muda tuu ndio haujafika.
 
Mkuu sio emotional dependant ni Ile umemuamini sana mtu ukamuona katika miongoni mwa watu na yeye yumo then unakuja kugundua kumbe jamaa yupo opposite kabisa
Pole Mkuu, sasa unatakiwa kuachana nae na kuendelea na mambo mengine. Kuanza kumfikiria na kuja kulalamika huku ina maana kuna namna ulikuwa tegemezi kwake bila hata wewe kujua.

Hapaswi kukuumiza akili wala moyo. Mchukulie hivyo alivyo endelea na maisha yako. Wala usimchunie, endelea kusalimiana naye, stori chache na ufocus kwenye ishu zako.

Again, pole sana Mkuu.
 
Halafu kwanini unachagua mtu wa kuwa nae close ?
Why usiache Tu itokee yenyewe Nani awe close na nani Asimwe close?
Unachagua ili iweje ...
Wa treat watu wote Kwa wema ...rafiki atajitambulisha na adui atajitokeza
Kwa kilichonitokea Mkuu sitaman Tena kua na Mtu close nimeamua kuweka boundaries watu nitaishi nao lakini to the certain extent
 
Mkuu sikuexpect chochote kutoka kwake ni kwamba nilizani ni mwenzangu kumbe sio I was wrong
 
Shukrani Mkuu
 
Niko na binamu yangu umri hatujapishana. Tumekua wote, likizo hii kwao likizo ijayo kwetu, shati, viatu suruali tunavaliana mpaka tukakua kila mtu akaoa Ila ukaribu uko pale pale. Nikiwa na pesa anahesabu Ni zake.
E bwanae kumbe jamaa Ni nyoka mlà mavi. Kuna siku tulipishana kidogo tu, jamaa akatoa yake ya moyoni sikuamini.
Kwanza kaniambia sisi sio kabila moja kwa hivyo Mimi na yeye wapi na wapi. (Mama zetu ndio wanazaliwa) ilibidi nikodoe macho tu. Baadaye akanipigia Nika m blok na kufutilia mbali namba yake. Sasa anapita huku na kule kuwashawishi ndugu tupatanishwe ule ulikua Ni ulimi tu umeteleza.
Nikikumbuka hapo zamani nilinunua viwanja viwili nikampa kimoja bure na ndio alipojenga, Leo ananiambia Mimi na yeye wapi na wapi.
Mwaka wa sita huu hatuongei japo Yuko very eager turudishe uhusiano ili apate vya bure kutoka kwangu. NIMESEMA NIMEMSAMEHE LKN UHUSIANO NA NYOKA SITAKI TENA.
 
Ahsante Mkuu nilikaa nalo hili jambo likawa linaninyima raha nikaona Nije nitoe sumuu
 
Tatzo lenu vijana hamuudhurii vikao[emoji4]
 
Pole Mkuu
 
Mkuu Pole sana.Hiyo ni Kawaida ktk Maisha,so cool down.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Pole sana mkuu ata mimi iliwahi kunitokea nilichanganikiwa nikapiga moyo konde nikaamua kujipenda mwenyewe mwisho wa siku aliyeniona mimi mavi leo anaona umuhimu wangu nmesikitika sana anaona aibu ila hana wa kumlilia
 
Mm sina rafiki permanent ktk maisha nipo kivyangu vyangu kila mtu ni rafiki lkn urafiki wetu unadumu kwa siku moja ama mbili.
 
Wewe jinsia gani?

Manake wadada ndo wanapenda kuchagua rafiki halafu wanataka huyo rafiki arithi na maadui zao...

Shida nini?
Rafiki wa kweli ni mungu na kazi yako fukuza hiyo umbwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…