Niko na binamu yangu umri hatujapishana. Tumekua wote, likizo hii kwao likizo ijayo kwetu, shati, viatu suruali tunavaliana mpaka tukakua kila mtu akaoa Ila ukaribu uko pale pale. Nikiwa na pesa anahesabu Ni zake.
E bwanae kumbe jamaa Ni nyoka mlà mavi. Kuna siku tulipishana kidogo tu, jamaa akatoa yake ya moyoni sikuamini.
Kwanza kaniambia sisi sio kabila moja kwa hivyo Mimi na yeye wapi na wapi. (Mama zetu ndio wanazaliwa) ilibidi nikodoe macho tu. Baadaye akanipigia Nika m blok na kufutilia mbali namba yake. Sasa anapita huku na kule kuwashawishi ndugu tupatanishwe ule ulikua Ni ulimi tu umeteleza.
Nikikumbuka hapo zamani nilinunua viwanja viwili nikampa kimoja bure na ndio alipojenga, Leo ananiambia Mimi na yeye wapi na wapi.
Mwaka wa sita huu hatuongei japo Yuko very eager turudishe uhusiano ili apate vya bure kutoka kwangu. NIMESEMA NIMEMSAMEHE LKN UHUSIANO NA NYOKA SITAKI TENA.