Nimekula pilau kwa rafiki zangu wakristo

Nayaheshimu maoni yako japo siyakubali
Sawa mimi nishajiondoa dhima kwa Allaah nimefikisha ujumbe leo Jf , utamua ufuate au ukatae Mimi jukumu langu nimemeliza , Allaah atuongoze kwenye haki na utuzidishie elimu ya kumjua yeye na dini yake . Aamiyn

وَقُلِ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكُمۡۖ فَمَن شَآءَ فَلۡيُؤۡمِن وَمَن شَآءَ فَلۡيَكۡفُرۡۚ
Na sema: Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akatae.

{Suratul- kahf 18 : 29 }

#Nimemaliza
 
Umekula pilau la nguruwe.
 
sio wakristo wote wana amini yesu ni Mungu, halafu it's just a celebration why be bothered when orhers do it?
 
Usi mpangie namna ya kuishi maisha yake, we all got a free will ukiona dini kwako ni bora kwa mwingine ni njia ya kawaida tu.
 
Acha kijana ale na kufurahi , wamatumbi sera yetu ni umoja na upendo ,haya madini mmeletewa tu, mbona papuchi za Wala kiti moto mnazifakamia na denda juu?
Umoja upo Mimi mbona nashirikiana na Wakristo wengi tu na kuwasaidia mpaka wananikubali na kuniona kijana mwema ?

Sikuu ni ibada sawa na kuingia kanisani na kusali ndio maana wao hawaingii msikitini kuswali kuonyesha solidarity kwani wanajua ni ibada
 
Sehemu gani kwenye Quran inakataza waislamu kusherehekea Christmas?
Hakuna ay explicitly imesema usherheekee Christmas . Lakini kutokana Uislamu sikuu ni ibada na asili ya ibada kwenye Uislamu hauwezi kufanya bila kupata amri na ikija amri unafanya kutokana na melekezo sio kama unavyotaka .

Ndio maana hata Waislamu walizusha kusherehekea maulidi ambayo kwenu kama X_mass kufurahia kuzaliwa kwa Mtume Muhammad ( peace and blessings be upon Him) MaSheikh na wanavyuoni wenye elimu walioinganhilo swala na wanapinga mpka Leo sababu sikuu ni ibada na ibada hauwezi kujitungia.

1. Kuamini kuwa Yesu Mwana wa Maryam (Amani iwe juu yake na Mama yake) ni Mungu ni ukafiri. Ametakasika Allah kutokana na wanayomshirikisha nayo.

2. Kuamini kuwa Allah amejifanyia mtoto ni ukafiri. Allah Ametakasika kutokana na kuwa na mshirika na Ametakasika kutokana na kuwa na mwana. Hana mwana wala mke.

3. Yesu (Amani iwe juu yake) ni Mtume wa Allah, sio mwanae Allah, sio Mungu wala sio katika nafsi tatu za Allah. Ametakasika Allah kutokana na kuwa mtoto na wala Mola wetu hana nafsi 3 na Allah Ametakasika kutokana na kuwa na mshirika yoyote yule. Yesu (Amani iwe juu yake) ni Mtume wake na ni Mtumwa wake.

4. Wakristo wanasheherekea krismasi wakiamini ni siku aliyozaliwa wanayemuabudu kinyume na Allah ambaye wanadai ni mtoto wake, bali wanadai kuwa ndie Mungu mwenyewe. Haya ni matusi makubwa kwa Allah. AMETAKASIKA MOLA WETU KUTOKANA NA YALE WANAYOMSHIRIKISHA NAYO. Hivyo hatushirikiani nao katika huu ushirikina na matusi makubwa wanayomtukana Allah Aliyetukuka. Na wala hatuwapi pongezi katika hili.
 
Acha sisi tule Christmas na marafiki zetu waislamu kwa raha zetu. Nyinyi endeleeni kutuita makafiri, sawa?
 
Umekula haramu🐼
Waislam na itikad zenu ,yesu alishasema kuwa kiingiacho tumboni mwa mtu hakimtii unajis, coz kikisha ingia kinapita haja kubwa na kwenda chooni ,bali kimtokacho mtu moyoni mwake ndicho kinachomnajis kama vile wivu ,husuda,chuki,unafiki ,i guess waislam kuhate chair fire(kitimoto) there is reason behind nasikiaga story kuwa mohammed aling atwa kalio na nguruwe
 
Si utoe hoja zako mbona unaleta ngonjera ?

Anzisha mjadala wowote tupimane kwa hoja tuone nani ana akili au kama akili shule ndio kabisa level yangu ya Elimu hauigusi

 
Sehemu gani kwenye Quran inakataza waislamu kusherehekea Christmas?
Katika uislamu sherehe zote zinaingia katika ibada na siku za sikukuu kwa mwaka mzima ni mbili tu, eid ya kufungua baada ya ramadhan na eid ya kuchinja wakati wa dhulhijjah, zaidi ya hapo haturuhusiwi kushiriki kwenye sikukuu yeyote ya ibada including maulid ambayo ni cloned version ya christmas.

Sasa muislamu anaeshiriki kwenye hizo sherehe za kikafiri za Christmas na mwaka mpya kuna tatizo kwake na sio katika uislamu, wao wana dini yao na sisi tuna dini yetu.
 
Muumini wa hovyo!mna ubaguzi wa kijinga sana ninyi.

Kualikwa ni kushiriki ibada?imani ipo moyoni haipo kwenye taste ya vitu mdomoni yaani nikiitwa kula nisiende kisa siyo dini yangu?huo ni uzwazwa!
Imani katika uislamu inaswadikishwa na matendo, sio imani hewa kama kuamini ndege zinazoacha ukungu angani ni rocket na kiwanja kipo misri na afrika kusini, so kula chakula kilichoandaliwa kwaajili ya kuadhimisha sherehe za miungu ya washirikina inaingia katika imani.

By the way ni mmepika vyakula vimewashinda kumaliza au? mbona kutulazimisha kula nyie jamaa, kwani lazima?.
 
Bahati mbaya sana Watanzania hawajali hayo mambo.
Kwa hiyo sisi kuanzia Christmas hadi Eid tunasherehekea wote kwa pamoja bila kujali kitu.
Watu wanazini huko na linachukuliwa kama jambo la kawaida, lakini kusherehekea Christmas mnaona ni ukafiri
Sometimes ni bora tu tusingeletewa hizi dini huku Africa. Zinatutenganisha sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…