Nimekuta Condom na kilainishi kwenye Pochi ya Mke wangu

Pole sana kaka, mtu hafundishwi kulia.
 
Nimeupitia uzi wako unaotamani mke wa mtu, ukashindwa kumueleza.

Sasa kuna vijana walimtamani mkeo. Wakamueleza, naye kawatunuku. Wanambabua.

Dunia ni hii hii.

Kilainishi gani hicho?
Hivi kumbe ndo huyu huyu kijana alkua ana mtamani mke wangu?! Akae kwa kutulia dawa imuingie alidhani kummezea fundo la mate mke wangu ndo kamaliza.
 
Ww ni zuzu kama mazuzu mengine kabonyeze rinda la mkeo utajua kama katumika ama laa alaf fanya maamuzi
 
Binafsi nakushauri mtoa mada kama ifuatavyo;
1. Kama huna uwezo wa kumuacha usimuulize.
2. Muulize tu pale unapojiona kuwa umemchoka na unatafuta sababu ya kuacha.
3. Kama huwezi kumuuliza, tafuta namna ya kuishi nalo. Ila kuna siku atafanya kosa dogo utauwa mtu
 
Unapokuwa na mawazo ya kujiua ni wazi tatizo kubwa lipo ktk ssikolojia.

Kaa na mkeo muulize ingawa umepoteza ushahidi kwa kutomhoji instant ulipokuta hizo zana
 
Huenda kuna semina alihudhuria ndipo wakagawiwa km ni Mtumishi wa umma ama taasisi fulani pia huenda alizipata siku ya UKIMWI DUNIANI Desemba 1 km ana mizunguko wa kumkutanisha na shughuli za hivyo.
Kuhusu kilainishi sijui ni cha aina gani labda kina matumizi mbalimbali.
 
Aisee hili nalo la kuja kuomba ushauri hapa. Acha mambo ya kizungu.
 
Nimesoma heading nikaona nikoment kabisa kabla ya kwenda kusoma uzi!
Kwa hivyo vitu ulivyovikuta kwa mkeo ni dhahiri kabisa kwamba mkeo ni "double line" (yaani anapigiwa mitandao yote)
Ngoja nisome sasa uzi wako ntarudi
 
Sio kweli.. ingekua ni kweli usingeweza kuandika hata hili bandiko hapa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…