Nimekutana na Mchina aliyekuja kama kibarua Tanzania ila sasa yeye ni Big Boss

Kama ulipomuuliza ndo kakujibu hivyo basi kakuona wewe ndo ndo mjinga.... Kwa sababu gan? Kwa sababu hayo aliyoyafanya yeye ni kutokana na exposure aliyokuwa nayo kutokea nchini kwao alipotoka, Wenzetu wameshafundishwa sana masuala ya production by action wakati wewe unahangaika ku-copy notes za Mabala ze Fama pale shuleni kwenu Kitobokikubwa Secondary School... Hivyo sio akili tuu bali hata mazingira ya upatikanaji wa vitendea kazi huwafanya jamaa kujua afanye nini ili apate nini ndo sababu hata wenyewe kwa wenywe wanaaminiana na kuwezeshana.

Huwezi kuwalinganisha watu ambao wanajua maana ya Family co-operation in Business na sisi ambao tumetoka kwenye familia ambazo mzazi hajui kupanda ila anataka kuchuma, (Kila mzazi anawaza mtoto akue akajitegemee ili amtegemee) Mtoto kabla hujakua ushakuzwa na hali duni ya familia yenu.

Nilitegemea angekosoa mifumo yetu ya maisha na Hali duni tulizonazo kama sababu ya kutokufika mahali fulani lakini kama anasema sisi ni wajinga basi nafikiri alikuzungumzia wewe kimafumbo

Unaweza ukazungukwa na malighafi kibao ila usiweze kujua ni namna gani utayatumia kutengeneza bidhaa kutokana either na kutokuwa na ujuzi au kukosa vitendea kazi so, What Will you expect?
 
Daah Mungu aniepushe na hii dhahama
 
Nunua solar acha kulaza vitukuu vyako gizani..karne hii unailalamikia serikali kwani wewe umefanyia nini hili taifa mpaka sasa
 
Anyway....
Haya maneno ni yako.
 
Mbona siku za karibuni umekuwa mwanaharakati wa kutetea haki za wajinga?
 
Sasa anza kumuandaa mtoto wako si usha jua? si umejua tatizo ni mfumo wa elimu? anza sasa
 
tusha jua sasa badilika anza na watoto wako, acha kuwapeleka English medium daily wanapewa Homowrk, haziwasaidii
 
Sawa, tumezaliwa katika jamii isiyoona fursa na kusoma katika mfumo wa elimu wa kijinga lakini sasa tunatoka huko ujingani, tumeanza kujitafuta na kujitambua, hatutaki tena watoto wetu wawe na mentality mbovu za elimu kama tulivyosoma sisi. Nchi hii ina fursa na utajiri mwingi tuuone na tuumiliki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…