Nimekutana na “my soulmate” nikiwa nimeshaoa

Wewe sio mzima ni wakuonewa huruma.Uwezo wa kunidhalilisha mimi huna sababu naongea reality na sidanganyi kama ww.Kama ulicho fanya ww.
 
Mwanamke kama unamtegemea mumeo akuhudumie kila kitu kama baba mwenye nyumba na uko chini kiuchumi kuliko mumeo. Basi tegemea wewe kuheshimu mumeo kuliko baba yako mzazi. Nipo Ujerumani , huku haki sawa ipo kuanzia uchumba mkienda out kila mtu analipa bill yake. Mkioana bill mnagawana nusu kwa nusu. Kama mke wangu Kala 45EUR na mimi nimekulia 55 EUR basi kila mtu analipa 50 EUR. Hayo maisha unayaweza ? Vile vile huku kuna ndoa za wanaume mabilionea na wake zao wa kushinda nyumbani. Hawa watu wanambato ma models na wanachukua likizo binafsi bali na familia na mke anakaa kimya. Ni wewe tu kuchagua maisha u nayotaka. Wanawake wengi wa Kiafrika walio-olewa Ulaya wanakumbuka nyumbani maana maisha ya 50-50 wanaona magumu. Wanaona bora wawe mama wa nyumbani na mume asimamie shoo muhimu. Huu ni mfano wa kate Middleton akiheshimu wakwe zake.Usishindane na mtu mwenye pesa. Kama unataka heshima na kusujudiwa tafuta hela mumeo atakuletea mauwa kila siku. Kama utaendelea kuwa feminist nakushauri achana na hela ya mwanaume yaani tafuta za kwako.
 

Attachments

  • rapidsave.com_the_curtsies_of_princess_kate-4yyujwrdk9nc1.mp4
    9 MB
How old are u?? We ni mwanaume au mvulana?? Hauko kwenye right state utakua na shida kidogo au Kuna stage kwenye mahusiano ulivuka
 
Huko hakufai kwakweli, hiyo sio ndoa hiyo ni business partnership, sasa hapo kama mwanume sauti unaitolea wapi?
 
Wanaume wengi wanawaoa wanawake wasiopendwa nao
 
Natamani nikusomee kifungu Cha Biblia kwenye kitabu Cha Yakobo.

Ila kwanza nianze kusema Usaliti mwisho wake ni maangamizi na kifo/kifo Cha ndoa Yako. Kile kiapo ulikula na ahadi ulizomuwekea mkeo Leo unamwona Hana thamani IPO siku soulmate pia utamwona Hivyo.
 
Unadham laana zinafika kirahisi hivyo? Wengi wangeshakufa. Take it easy.
 
We hifadhi tu maadam unapenda ligi dhidi ya gentlemen Tutakutana huko mahali
Sawa
Wewe sio mzima ni wakuonewa huruma.Uwezo wa kunidhalilisha mimi huna sababu naongea reality na sidanganyi kama ww.Kama ulicho fanya ww.
Mimi kudanganya kuhusu maisha yangu kunahusiana nini na hii mada inayohusu jamii kwa ujumla hebu jibu hayo maswali acha kukwepa hoja, endelea kushusha hayo magazeti yako ili nikudhalilishe ijulikane nani mweupe kichwani, mbona umekimbia mada umejificha kwenye kichaka cha hiyo comment yangu kama kweli unajiamini una hoja si urudi kwenye mada au vipi
Oohh kwahiyo hiyo kwa mujibu wa hiyo kanuni yako ni kwamba siku baba akitetereka kiuchumi, na mama akalazimika kusukuma gurudumu mpaka baba atakapokaa sawa, maana yake kwa kipindi hicho baba atatakiwa kumtii mama si ndio

By the way unasahau kwamba huko kwa wenzetu mke hawajibiki kumtii mume na hakuna mgawanyo wa majukumu yeyote ana wajibu wa kufanya jukumu lolote, kwahiyo huko 50/50 haipo kwenye kulipa bills tu bali ipo hadi kwenye kazi za nyumbani na malezi ya watoto, na kama mnaweka housemaid yeye ndio atafanya majukumu yote ya nyumbani ili mume na mke wasaidiane majukumu ya kiuchumi tu

Na hutasikia mwanaume akilalamika kuwa eti mke wake kajisahau kazi zote kamuachia dada na wala hawafikii hatua ya kutembea na hao wadada kwa sababu hiyo, lakini huku afrika ambako hadi leo wanaume wanapenda kunyenyekewa, kupikiwa na kufuliwa na wake zao na wanaona kwamba kazi za nyumbani haziwahusu kabisa

Msitegemee wanawake wataikubali hiyo 50/50 ya kwenye kulipa bills kwa sababu hata ninyi hamuwasaidii majukumu yao, kwahiyo msiwalaumu kwamba hawawezi kuwasaidia yenu siku mtakapokubali kuacha kupenda kunyenyekewa, na mtakapokubali kuyachukulia majukumu ya nyumbani na malezi ya watoto kama wajibu wenu

Basi nawahakikishia hata wanawake nao wataanza kulichukulia serious hilo suala la kulipa bills 50/50, yani kwa kifupi hiyo 50/50 isiwe applicable kwenye majukumu ya mwanaume tu bali hata ya mwanamke pia kama huko kwa wazungu, ila tatizo linakuja wanaume ndio hamko tayari kufanya majukumu ya wanawake yani unataka wewe ufanye majukumu yako tu ila mwanamke afanye majukumu yako pamoja na yake hapo ndipo wanawake wanapogoma
 
Una ndoa ya miaka 25....... ?😀😀😀

Utanifanya ni kurupue thread za nyuma,nilizokuwa na kuelekeza ww........ unajikanyaga kanyaga na kuongopa mpaka hujui ulisema nini.
 
Niliwai kua kwenye Hali Kama yako Kama ni muislamu ongeza mke wa pili Ila Kama ni mkristo acha matamanio yako ya kimwili maana ndoa ni moja ya mke mmoja..

Alinambia hakuwai dhani angeweza kua na mahusiano na mume wa mtu Ila kwangu aliweza nacho shukuru mungu aliweza kuniambia anaiheshimu ndoa yangu na aka move on mpaka Leo ni washikaji Sana marafiki pia alikua na UWEZO wa kuivunja ndoa yangu now ni marafiki wa KAWAIDA

Zingine ni FANTASY 😇 heshimu ndoa taka TIFU
 
Una ndoa ya miaka 25....... ?😀😀😀

Utanifanya ni kurupue thread za nyuma,nilizokuwa na kuelekeza ww........ unajikanyaga kanyaga na kuongopa mpaka hujui ulisema nini.
Hebu kurupua hizo threads sasa hivi nione hayo uliyokuwa unanielekeza hadi nikawa najikanyaga, ila naomba tu usije ukakwepa hoja ukakimbia mada au kuniita mbishi na wala usije ukaanza kuleta personal attacks, naomba unapoleta hizo threads tujadili mada husika tu na siyo maisha yangu binafsi au chochote kisichohusiana na mada

Na kama ni ile thread kuhusu 50 50 basi afadhali umejileta mwenyewe maana nakumbuka vizuri mwisho wa siku ni wewe ndio ulikimbia ile mada ukaanza kuniita mimi mbishi, na naomba kabla hujaileta hakikisha umeisoma yote na siyo kichwa cha habari tu ili kuepuka kunipotezea muda kwa kunifanya nirudierudie kuandika ambayo nilishayaandika kwenye thread, narudia usije tu ukatafuta kichaka cha kujifichia

Zilete hizo threads uzuri mie sijawahi kukwepa hoja wala kukimbia mada
 
Kalale ukue kwa details hizo ndio soule mate🥺🥺
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…