Nimekutana na rafiki yangu mwarabu tuliesoma shule ya Msingi, Nasikitika kuona wageni wanavyotajirika huku wenyeji tumeridhika na vimafanikio vidogo

Uka mdiss mama ako🤔🤣😆
 
Alafu yakitokea ya kutokea anakuambia ujiajiri wakati hakuna msingi aliokuwekea tofauti na elimu ya darasani 😃
 
Angalau wachaga wana talanta hyo
 
Nashukru KWA mchango wako .....naungana na ww
 
Tungekuwa mbali Kama tungeiga Wahindi. Tangu mtoto weekend anabaki kwenye biashara
 
Wazazi Watanzania ambao wamefanikiwa ni waoga sana kuwatumia watoto wao kuendeleza miradi yao ya kibiashara iliyofanya wafanikiwe tofauti na wenzetu wenye asili ya Asia (Waarabu na Wahindi)

Nikupe mfano utakuta baba alikuwa mkulima mzuri sana, mkubwa na mwenye mafanikio hata watoto wake kawasomesha kupitia hiko kilimo

Cha ajabu akiwasomesha watoto wake haukuti anawasomesha waje waendeleze biashara hiyo ya familia waje na idea mpya. Watoto watasoma waje kuajiriwa, baba umri ukienda (uzee) au kifo na biashara ya kilimo inakufa

Watanzania tunakosa kujiamini sana kuendeleza biashara za kifamilia. Tunapenda sana kuajiriwa. Wenzetu wanatengeneza brands
 
Ombwe la historia, udini udini. Tabia za kitumwa(slavery trauma) bado zinatuandama.
Ujinga ujinga na ujuaji usio wa kimaarifa
Watanzania wengi wanajifanya wanajua mambo kumbe empty, ndio maana tunafeli mambo mengi kwa kukosa weledi.
Waafrika weusi tulichbakiza ni kulalamika tu.
Hao wahindi na warabu hawatuzuii sisi kuwa matajiri ila wakitajirika tunawachukia.
 
Umenyooshaaa mkuu...

Ubinafsi,ubinafsiii umetujaa ..

Mtu Kwenye familia anapesa lkn kusupport hata wadogo zake mtaji n shidaa..

Anatakaa aonekanee kwenyee ukoo yy pekee ndio tajirii[emoji23][emoji23][emoji23]
Unaongeleaje hili la kumpa mdogo wako mtaji,anakula unaisha anarudi kwenye foleni ya kukupiga mizinga
 
Wakati wao wanaumiza vichwa kutafuta njia ya kupata,wewe uko bize unawaza kula tunda kimasihara na kusaka papuchi. Si ndo hivo?

Af,wao wana ushilikiano mkubwa. Huku ngozi nyeusi,kila mmoja anaona ndugu akifanikiwa ni hasara kwake sasa.
 
Kama mwarabu alikuja Africa huyo mtu mweusi alikuja kutokea wapi ?


Kihistoria binadamu wa kwanza duniani kaishi Africa tena ni mweusi unasemaje mwarabu ana muda mrefu Africa kuliko mtu mweusi

Sent from my Pixel 5 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…