Nimekuwa mtu wa kusaidia sana ila sifanikiwi na kila siku niko palepale maishani

Miss Natafutwa

Senior Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
190
Reaction score
593
Nimekuwa mtu wa kusaidia sana angalau kwa kiasi kidogo ninachopata kuwatimizia wahitaji.

Anaweza akapita mtu anahitaji msaada wenzangu wote watakaa kimya ila mimi lazima nitoe hata kama nimebakisha hikohiko mfukoni.

Natoa sana msaada huko barabarani.

Najitoa sana kwa mtu hata kama kaja kwangu atahitaji kula au nauli ila ndio hivyo sifanikiwi na kila siku niko palepale maishani.

Je, naweza nikawa ninakosea kusaidia? Au kuna sehemu pana walakini?
 
Saidia tu,Kuna watu wapo chini yetu wanahitaji msaada wetu kama ambavyo tunasaidiwa na waliojuu yetu...kama ipo ni ipo tu..mi huwa natoa atajua yeye kama ni mwanga au ni mtakatifu...
Moyo uumie kwa ajili ya kitu ambacho naweza fanya moyo utulie...ili iweje?
 
Kwahiyo unasaidia ili ufanikiwe?
 
Kizazichako
Hivyo ndivyo ulivyoumbwa kiufupi hiyo ndio tabia yako wala usijilaumu,utakapojizuia kumsaidia mtu wakati uwezo wa kumsaidia unao utajikuta unakosa amani.
We saidia pale unapoweza pasipo kujiumiza matunda yako yatakujaliwa na kizazichako cha baadae pasipowao kujua neema zinatokea wapi kumbe wewe ndio ulipanda mbegu.
 
Ombaomba wa barabarani sio wahitaji wengi wao ni wachangishafedha,unapotoa msaada usijali uchawi kwani mchawi anaweza kukudhuru hata bila kumpa msaada isitoshe unaposaidia jua umeguswa na shida za mtu hivyo ni roho ya ki Mungu iliyo ndani yako ndio inakusukuma kusaidia,mathalani mimi ni mtu wa kujitoa sana pale ninapoguswa na shida ya mtu ambayo ipo ndani ya uwezowangu nitamsaidia mwenyewe ikiwa nje ya uwezowangu nitamsaidia kwa njia nyingine ambayo itapelekea kutatua tatizo.
Lakini kuna watu wengine huwa roho yangu inagoma kabisa kuwasaidia huwa sielewi kwa nini na roho ikigoma huwa silazimishi.
Saidia tu ila sio Kila msaada ni mzuri Tena hasa huu wa barabaran naskia Kuna uchawi mwingi so maybe upunguze misaada ya kupita njian dear si Kuna charity kama shida ni msaada
 
Mlipa ya roho za uhurma ina riba kubwa achana nalo ni mda kuwa mr kuku sasa na LBL kudai kama ccm
 
Mama angu ,kufanikiwa ni suala la financial literacy, hayo mambo ya kusaidia ili ufanikiwe hakuna mahala economics imeeleza hizo habar hata ukasome Havard hutakutana na hiyo concept.
Mafanikio is all about

  • what you earn
  • what you save/keep out of earning
  • what you spend (should be less than earning)
  • what you invest out of your income.

Mengine hayo ni mahubiri ya wachungaji tu ambapo wakimaliza kuhubiri, unatakiwa kuwapa/kutoa sadaka (you pay for the service)
 
Oohhhh..... Hapo kwenye ambaye hazalishi pesa.... Fafanua zaidi Mkuu🙏🏽
Usimpe pesa Malaya, usimpe pesa omba omba. Usiitumie pesa Yako kuumiza watu n.k. mpe pesa mzazj wako, ndugu Yako wa damu, mke wako, watoto wako, wafanyakaz wako, partner wako/ mpambanaji mwenzio. Hao wengine wape mahitaji si pesa. Akikuomba hela ya msosi mnunulie msosi ale
 
Saidia kwa moyo wa huruma wala usisaidie ili upate. Kuna watu ukiwaona unaona wazi, anahitaji msaada hata kama anafanya biashara ndogondogo. Nina jicho la kuona hivyo, inaanzia rohoni na kwa hilo jicho nitatoa kwa huruma. Na kuna ambao sitoi kwa kumuangalia tu najua sitakiwi kutoa. Mimi hulipwa hata mara 10 yake nayotoa. Usitoe ili upate, saidia tu mengine Mungu anajia roho yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…