Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Sasa nakuwa nimedhulumu vipi ilihali sijawahi mshurutisha wala kumuomba anifanyie hivyo? Nyumba na gari ni vitu wala sina shida navyo kwa sasa naweza nunua zangu hivyo kumrudishia wala sioni tatizo. Hofu yangu ni atalichukulia poa bila kunidhuru?
inategemeana na gharama alizotumia kwako, pengine alitaka akuzalishe uwe mke wa pili na vyake ndo ushakula bila hata kumzalia, na bado unataka umteme live bila chenga. Heri kama ungekuwa na watoto nae angeweza akakuachia bure hizo mali akijua ni za watoto.

wee nenda moja kwa moja na funguo za gari lake pamoja na hati ya nyumba yake alokupa mkabizi, afu mwambie umepata mume unataka kuolewa na unahitaji kuwa na familia, hawezi kukukataza wala kukuzuru.

Shida ni anapopata taarifa kuwa umeolewa ghafla tuu, na vyake ndo ushakula ikiwemo mpaka nyumba yake na gari, hapo lazma atakuchukulia ulikuwa unamchuna (tapeli) ili ukaolewe, na ndo uadui utakapoanzia, ama ufe, tena kifo cha kikatili au upotezwe kusikojulikana na usionekane kabisa, ikabaki historia tuu.
 
Ujengewe nyumba
Gari ununuliwe..
Kazi nzuri utafutiwe ..


Halafu unasema anaku suffocate?

Tukusaidie umuache vipi?

Huyo Kijana umemwambia kuhusu kodi?


Why usirudishe nyumba na gari kwanza uone huyo Kijana mpya atakupenda vipi?

Ukiuliwa wala usimlaumu mtu
Huna akili
Yaani hawa viumbe ni pasua kichwa aisee daah
 
Ukisikia mchepuko kumuua mume wa mtu ndio hii.

Tafadhali wewe na boyfriend wako mpya msije mkapanga mauaji ya mzee kwa tamaa ya kubaki na mali na kuwa huru.

Mtahukumiwa jela kunyongwa na mtakosa vyote.
hapa nae umesema neno, anaweza wakapanga njama za kumuua mzee wa watu au kumdhuru wakijua ndo watasalimika. Tena asijaribu kabisa, ni heri akubali kufa yeye mara 7 zaidi kuliko kupanga njama za kumuua au kumdhuru huyo mzee, maana akijaribu kumuua tuu au kumdhuru kwa lolote lile, kuolewa kwake itabaki historia ataskia kwa wengine, na huyo anaetegemea kuolewa nae anaweza asimuoe au hata akafa kabisa.

Pia na ikawa ndo chanzo cha kuharibikiwa mambo yake na maisha yake yote. Maana laana ya kumwaga damu ya mtu tena asie na hatia haijawai muacha mtu salama.
 
Wanawake hivi kwenye maisha huwa mnataka vitu gani hasa???
 
Wanaohisi huyo dada asipokua makini atauawa wekeni likes hapa.
 
Married men have accomplished greater things in this country than all the NGOs combined.
Married men tunawainua wanawake kiuchumi kuliko Any Government or NGO program ya kuwainua iliwahi kuendeshwa humu nchini!!
Lakini hatuwi recognized!!
 
Kuna wakati huwa nafikiria kumrudishia gari na hati ya nyumba na viwanja alivyoninunulia kisha nimwambie tuachane. Ila nahofu atavipokea bila kinyongo?

BTW Sina hata huo uzuri na hilo tako unalofikiria ninalo. Ni wa kawaida sana.
Kumbe Hadi viwanja umenunuliwa.
We mzalie tu huyo mwamba maisha yasonge mbele.
Kwani kuwa mke wa pili Kuna shida gani?
Hicho kiboyfriend ukiwa huna kitu kinakupiga chini.
Maana yeye ndio itabidi aanze kuhudumia sasa
 
Wanawake bana mnapenda slop sana, mtu akununulie gari, na akujengee nyumba alafu unakuja kutuomba ushauri,, sasa nakwambia tu siku zako zinahesabika na litakua fundisho kwa wajinga wengine kama ww..

Ikitokea mtu amaua tuwe tunauluza sababu tusimlaum muuwaji aisee,,sasa mtu kama huyu binti siunafuta kifo tu ww.

Hakuna mwanaume wa kuvumlia kufanya unachotaka ww rudisha vitu vya watu utakufa kabla ya siku yako
 
This is amaizing hela tamu, unaitwa mama mwenye mjengo, gari na kazi...ila sasa vyote hivyo vimewekwa na kiegemeo cha mtu, akitoa mguu unaogopa kuanguka.

Fanya yafuatayo:

1. Wekeza hela kuanzia sasa hadi miez 6 ikibid kopa hapo kazini ziwe nyingi zaidi.

2. Uza hiyo gari ikiisha hiyo miezi 6

3. Kwa vile nyumba yako ina hati na jina lako uza kimia kimia

4. Uza viwanja kimia kimia.


Ule mwezi wa mwisho uza vitu vyako vya ndani vyoote.

Hakikisha unabadili kila kitu kuwa hela, na hizo hela weka account, usiweke account moja anaweza kufanyia ujinga, ikibidi kama una ndugu yako ana account hatumii muazime utunzie hela.


Kisha ukiona kila kitu kiko kwenye mahala pake yani huna kitu cha kukushikilia amka safarini nenda tafuta Mkoa kaa utulie udifanye chochote, zima simu badili laini chonga mpya.

Atapata hasira ndani ya mwezi mmoja wa pili zilisha isha anarudi kutulizana kwa mkewe, na litakuwa libido linatia mkewe hadi mkewe atakuwa ananjiuliza kulikon natiwa hivi siku hizi.

Ukikosa mkoa njoo nikuelekeze nilipo ukae wakat unajiandaa upepo upite utumie hizo hela ulizokusanya kufanyia baishara zako na kuishi maisha ya uhuru.

Nipe like basiiiiii[emoji3]
 
Kumbuka
Hapana amechoka kuwa mtumwa na anahitaji kuwa huru na mtu atakayelala na kuamka naye. So Ms Saaly sell the house Tena hakikisha kuanzia dalali mpaka mnunuzi wawe ni wageni maeneo hayo wasije vujisha kwa Mzee baba ukalambwa Shaba. The day umepata malipo ndipo acha kazi Ile ya masaa 24.
On the same day or the day after, get away leaving everything else behind including your dear friends, I mean everything; car, contacts, some personal belongings. Tanzania ni kubwa hii na Africa ni Moja. If you will pocket 20m it's enough to start afresh somewhere else in Tz or EAC.
Wapenzi kuuana ni real, take care.
Ukishauza niambie nikufiche!!
Kumbuka milima haikutani, binadamu hukutana mkuu.
 
Habari wanajamii forum, ni matumaini yangu kuwa mko salama. Ama la, basi Mungu awafanyie wepesi.

Ndugu zangu nahitaji msaada wa mawazo yenu sana. Ninapitia sijui niseme ni wakati mgumu au ni ujinga wa kujitakia. Niko kwenye mahusiano na mume wa mtu sasa yapata miaka mitatu. Imefikia hatua nimechoka na nahitaji kujing’atua ila nakosa njia nzuri ya kuachana nae. Am not even proud with what i did so if you judge me i’ll understand.

Huyu mtu tangu nafahamiana nae ameyabadilisha sana maisha yangu maana ana mchango mkubwa sana. Alinisaidia kupata kazi nzuri na kuachana na kakazi kangu nilikokuwa nafanya, alinihamisha na kunipangishia sehemu nzuri zaidi. Baadae alininunulia gari nami nikawa natembea nimekaa, pia amenijengea nyumba iliyo kwa jina langu ila kwakuwa ipo nje ya mji nimeipangisha nakula kodi ila bado analipia kodi hapa ninapoishi.

Mahusiano yalipoanza sikufikiria hata yangechukua miezi 6, ila sasa ni miaka mitatu+. Ni mwanaume anayejali sana ila ana wivu balaa. Ni mara kadhaa amekuwa akinitishia kuwa akigundua ninamsaliti atanikata shingo. Sasa huwa najiuliza huyu ni mume wa mtu, anatarajia kweli niwe na yeye tu ili iweje?

Sasa nimechoka jamani, natamani niwe na mpenzi wangu na sio mume wa mtu. Kuna huyu kijana nimeanza nae mahusiano sasa ni miezi 5, kusema kweli nampenda na ninaona kabisa nae ananipenda. Haya ndio aina ya mahusiano niyatakayo. Nimekuwa nikitafuta visingizio kuwa asije kwangu maana sio maadili ila ukweli ni kuwa naogopa mlipa kodi akijua atanitoa roho.

Huyu mume wa mtu nishamtafutia visingizio ili tuachane ila inashindikana. Natamani yeye ndio aanze ili asije kuwa na kinyongo. Ila kuna wakati najipa moyo kuwa nimwambie tu tuachane lakini nikikumbuka aliwahi kunikunja nusura anipige alipokuta msg asizozielewa kwenye simu nahisi kutetemeka. Aliwahi kunionyesha silaha anayomiliki, nilipomuuliza ni ya nini akasema hata mimi nikimletea ujinga ananifyatua. Japo ulikuwa utani ila niliogopa kusema kweli.

Balaa zaidi recently ameanza kung’ang’ania nimzalie. Nimekuwa nikijifanya mimba hazishiki ila kusema kweli natumia dawa zisishike maana siko tayari kuzaa nae. Kwanza nahisi kama suffocation maana ananibana sana. Kwangu anakuja tu muda wowote akijisikia, na ole wangu asinikute nyumbani ni tatizo kubwa. Kila ninachofanya anahitaji apate taarifa kwanza, yaani kama mkewe vile jamani.

Nimejaribu kuelezea haya ili angalau muelewe ni kwanini nahitaji msaada wa mawazo yenu ili nijikwamue kwenye hili shimo nililojichimbia. Nipeni ushauri naachanaje na huyu mwanaume bila kuleta madhara kwangu.
Anza kwa kurudisha kila kitu chake then nenda kwa serengeti boy. Ila ukileta za kuleta atakutanguliza kweli
 
This is amaizing hela tamu, unaitwa mama mwenye mjengo, gari na kazi...ila sasa vyote hivyo vimewekwa na kiegemeo cha mtu, akitoa mguu unaogopa kuanguka.

Fanya yafuatayo:

1. Wekeza hela kuanzia sasa hadi miez 6 ikibid kopa hapo kazini ziwe nyingi zaidi.

2. Uza hiyo gari ikiisha hiyo miezi 6

3. Kwa vile nyumba yako ina hati na jina lako uza kimia kimia

4. Uza viwanja kimia kimia.


Ule mwezi wa mwisho uza vitu vyako vya ndani vyoote.

Hakikisha unabadili kila kitu kuwa hela, na hizo hela weka account, usiweke account moja anaweza kufanyia ujinga, ikibidi kama una ndugu yako ana account hatumii muazime utunzie hela.


Kisha ukiona kila kitu kiko kwenye mahala pake yani huna kitu cha kukushikilia amka safarini nenda tafuta Mkoa kaa utulie udifanye chochote, zima simu badili laini chonga mpya.

Atapata hasira ndani ya mwezi mmoja wa pili zilisha isha anarudi kutulizana kwa mkewe, na litakuwa libido linatia mkewe hadi mkewe atakuwa ananjiuliza kulikon natiwa hivi siku hizi.

Ukikosa mkoa njoo nikuelekeze nilipo ukae wakat unajiandaa upepo upite utumie hizo hela ulizokusanya kufanyia baishara zako na kuishi maisha ya uhuru.

Nipe like basiiiiii[emoji3]
Mimi nadhani Solution hapo ni kurudisha vitu vyote alivyopewa khs kazi sijui itakuaje lkn amrudishie jamaa vitu vyake vinginevyo cha moto kitamkuta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu uzi kama ni majibu wa ule uzi wa jamaa anayetaka kumdhuru mwizi kwa mchepuko wake. Dada kama ni wewe amua moja. Maana jamaa kasema hana mpangi wa kuachana na wewe.
 
Back
Top Bottom