Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Habari wanajamii forum, ni matumaini yangu kuwa mko salama. Ama la, basi Mungu awafanyie wepesi.

Ndugu zangu nahitaji msaada wa mawazo yenu sana. Ninapitia sijui niseme ni wakati mgumu au ni ujinga wa kujitakia. Niko kwenye mahusiano na mume wa mtu sasa yapata miaka mitatu. Imefikia hatua nimechoka na nahitaji kujing’atua ila nakosa njia nzuri ya kuachana nae. Am not even proud with what i did so if you judge me i’ll understand.

Huyu mtu tangu nafahamiana nae ameyabadilisha sana maisha yangu maana ana mchango mkubwa sana. Alinisaidia kupata kazi nzuri na kuachana na kakazi kangu nilikokuwa nafanya, alinihamisha na kunipangishia sehemu nzuri zaidi. Baadae alininunulia gari nami nikawa natembea nimekaa, pia amenijengea nyumba iliyo kwa jina langu ila kwakuwa ipo nje ya mji nimeipangisha nakula kodi ila bado analipia kodi hapa ninapoishi.

Mahusiano yalipoanza sikufikiria hata yangechukua miezi 6, ila sasa ni miaka mitatu+. Ni mwanaume anayejali sana ila ana wivu balaa. Ni mara kadhaa amekuwa akinitishia kuwa akigundua ninamsaliti atanikata shingo. Sasa huwa najiuliza huyu ni mume wa mtu, anatarajia kweli niwe na yeye tu ili iweje?

Sasa nimechoka jamani, natamani niwe na mpenzi wangu na sio mume wa mtu. Kuna huyu kijana nimeanza nae mahusiano sasa ni miezi 5, kusema kweli nampenda na ninaona kabisa nae ananipenda. Haya ndio aina ya mahusiano niyatakayo. Nimekuwa nikitafuta visingizio kuwa asije kwangu maana sio maadili ila ukweli ni kuwa naogopa mlipa kodi akijua atanitoa roho.

Huyu mume wa mtu nishamtafutia visingizio ili tuachane ila inashindikana. Natamani yeye ndio aanze ili asije kuwa na kinyongo. Ila kuna wakati najipa moyo kuwa nimwambie tu tuachane lakini nikikumbuka aliwahi kunikunja nusura anipige alipokuta msg asizozielewa kwenye simu nahisi kutetemeka. Aliwahi kunionyesha silaha anayomiliki, nilipomuuliza ni ya nini akasema hata mimi nikimletea ujinga ananifyatua. Japo ulikuwa utani ila niliogopa kusema kweli.

Balaa zaidi recently ameanza kung’ang’ania nimzalie. Nimekuwa nikijifanya mimba hazishiki ila kusema kweli natumia dawa zisishike maana siko tayari kuzaa nae. Kwanza nahisi kama suffocation maana ananibana sana. Kwangu anakuja tu muda wowote akijisikia, na ole wangu asinikute nyumbani ni tatizo kubwa. Kila ninachofanya anahitaji apate taarifa kwanza, yaani kama mkewe vile jamani.

Nimejaribu kuelezea haya ili angalau muelewe ni kwanini nahitaji msaada wa mawazo yenu ili nijikwamue kwenye hili shimo nililojichimbia. Nipeni ushauri naachanaje na huyu mwanaume bila kuleta madhara kwangu.
Rudisha nyumba, gari, na uache kulipiwa Kodi. Dakika mbili tu unamuacha na anaridhika Kabsa. Chaguo ni lako
 
Mwana kulitafuta, Mwana kulipata. Hiyo silaha itakuacha salama kweli?. Mwambie kijana wa watu usije mletea dhahama bure kwa ulafi wako.
 
Nitajikita kwenye upande unao utaka wewe japo unaweza usiwe sahihi,

Kwanza amini hakuna kisichowezekana chini ya jua, ukiwa na nia thabiti na tayar kukabili yatokanayo na maamuzi yako itawezekana.

Pili, jikite kwenye kumjua huyo mwanaume wako mpya, umejenga uhusiano kwenye uongo,
1. anaweza akaujua ukweli na penzi pale pale likapungua.
2.Na huwez ficha ukweli daima
3. Wanaume almost wote tunafanana unalokimbia huku utakutana nalo kule(mchepuko, vitisho, wivu, etc) tathmini uone kama ndo unachohitaji

Ukishaona anafaa na ndo uende naye rudi Sasa kwenye uhalisia na hyu jamaa.

1. Amekupa maisha kiasi cha wewe kuweza kujisimamia na kutamka unaweza jitunza bila yeyote na bado ukajifanyia vyote alivyokufanyia... Sasa ondoa haya kwenye point za kutumia wakati unafanya maamuzi.

A/ Kamwe hutoweza kujificha popte asikupate... Nenda nchi yoyote ila kama aliweza kukupeleka kote huko, ni suala la muda tu. Akiwa na nature kama yangu, hata miaka 10 kulipia kisasi atavumilia.

B/ Hutoweza kumwacha nae akakubali kama utatumia Aina yoyote ya ubabe au kumchallenge. Ni hivi akiona njia uliyotumia ni Maji marefu( yaan kwa pesa na influence hakuwezi) atakaa chini na kujisuka aje strategically kukumaliza( na kwa summary ulotoa huna background powerful kiasi cha kumtisha hvo)

C/ Usiwazie suala la kumlipa, huna cha kumlipa, ni kama ingekuwa vice versa nae Hana cha kukulipa, kuliamsha Hilo ni kuonesha dharau kwa mambo meng yaliyoendelea mioyoni mwenu, nyakati na nia zenu, wala Usiwazie kwenda kwa mkewe kwa namna yoyote.

D/ Mungu unayemsema na kutaka kumrudia tambua hakushangai kwa haya maana anajua fika ungefanya hvo, atakacho kushangaa ni kutaka kumlaghai kwa kutubu kwako wakati tabia yako ilokusukuma kufanya hvo bado iko ndani yako na unaweza rudia tena na tena kosa Hilo hlo(rejea petro kumkana Yesu japo alijiapia hawezi kamwe)

Cha kufanya

Namna pekee kwangu nnayoiona ni kwa kupata huruma ya huyo mwanaume basi. Hyo huruma utaipataje, wewe ndo unamjua ilivyo.

Bila huyo mwanaume kupuuzia uamuzi wako au kufikia hatua ya kukuchukulia kama mpuuzi kiasi cha kuona bora aache kupoteza hela na muda kwako huna namna ya kibabe ya kumchomoa labda umuue, au ukeshe kwenye maombi.

Mwisho wa siku jitafakari na ww pia, je yaliyokukera ni kweli yana kero kwako? Au ni kwasababu mhusika ni hyu mhudumiaji?
 
Wapendwa badala mnipe ushauri mnaniongezea magazijuto kweli? Najua i messed up big time and an not proud. Nisaidieni najikwamuaje hapa.
OK simple and clear ...mrudishie gari, nyumba yake. Then mwambie ts over akileta shida mwambie utampa mkewe taarifa
 
Ushauri wangu upo tofauti na wa wanaume wengi, si umesema nyumba na gari vipo kwenye jina lako? basi hakuna kurudisha, ndio ukumbusho wa penzi lenu, unapolipiwa kodi hama, kapange pengine. Mwanaume mwenye uwezo wa kukujengea nyumba, kukununulia gari na kukupeleka vacations bila kuwaza hawezi kupoteza muda wake kukusumbua urudishe vyake penzi linapoisha, off course atakuwa disappointed na wewe lakini iyo wewe haikuhusu coz you are looking after your own best interests.

Kuhusu kumuacha mshua kwenda kwa mshkaji, hakikisha unapoenda ni upgrade ya ulipotoka, some fellas look good on paper( kazi nzuri, gari nzuri, kapanga pazuri) lakini ukishaingia ndani ya mahusiano unagundua it's all a facade, mchizi anateseka na madeni yasiyolipika to mantain his lifestyle, hapo ujamuongezea majukumu ya mke na watoto. Play your cards right.

Ni bora kuwa mchepuko wa mwanaume mwenye uhakika wa maisha kuliko kuwa mke wa ndoa wa mwanaume anayebahatisha maisha.
 
Hivyo vitu vyake sina shida navyo naweza virudisha hata leo.

Mpenzi wangu hana shida maana ni mhudumiaji mzuri tu pia. Sijawahi muomba pesa ila huwa ananipa bila kuomba. Ni mtu anajali sana na ndio maana nimesema ndio aina ya mahusiano nahitaji kwa sasa.
Sasa kama unayaweza usisuburi uambiwe rudisha kama uanvyotaka kurudisha mapenzi.
Kwasasa utaona huombi kwakuwa unacho na huyo mtu anakuhudumia kawaida tu, Subiri siku yatokee utarudia tabia ile ile ya kuomba na hapo ndio utamuona huyo mhudumiaji mpya sio mhudumiaji kabisa.
Huyo mume wa mtu ukimpata kwakuwa ulikuwa na shida Sasa shida huna ndio maana umeweza kutafuta unayemudu.
 
1. Hukumuomba asiheshimu ndoa yake, hakuiheshimu akakutongoza...na wewe hukuiheshimu ukamkubali.

2. Hukumuomba akujengee nyumba, ni kiherehere chake, badala ya kujengea mkewe na watoto akaamua kutapanya

3. Hukumuomba akununulie gari, inawezekana mkewe hajawahi mnunulia ila ametapanya

4. Muite, ukiwa na ukinzi [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] mwambie mahusiano yenu yamefika mwisho arudi kwa mkewe.

5. Hama anapokulipia kodi ujilipie mwenyewe

6. Kata RB

7. Tembea na ulinzi atakukata shingo kwelj huyo ohooooo

8. Muachage kutembea na waume za wenyewe.....matokeo yake mkishachuma ndio mnajiona mnahitaji wa kwenu peke yenu
Hivi yule wa dar alifanywa aje
 
Kua na Mali Ni suala jingine, na moyo wa kuhudumia Ni suala jingine.

Kuna Watu wanamali Sana ila Ni mabahili Hadi kwenye afya zao wenyewe.

Muda always Ni mwamuz mzur[emoji4]

Ubahili sidhani, ananihudumia vizuri tu tena bila kuomba.
 
Yaani nyie wajinga mnaojifanya maslayqueen wa kuchuna hela za watu mnawaacha. Yaani nyie chombo cha moto kinawahusu. Pumbavu kabisa.

Rudisha hizo mali ndio uolewe

Mie sio slay queen.
 
Yote haya umeanza kuyaona baadaya kuhongwa gari na nyumba !?

Okay okay I understand now why huwaga mnauwawa ,

Mahusiano yalipoanza nimesema nilikuwa najiegesha tu wala sikutarajia yangefika hata miezi 6 ila ndio hiyo miaka mitatu + sasa. Ila at some point si ni lazima yaishe? Unakuwa vipi na mahusiano ya kudumu na mume wa mtu?
 
Habari wanajamii forum, ni matumaini yangu kuwa mko salama. Ama la, basi Mungu awafanyie wepesi.

Ndugu zangu nahitaji msaada wa mawazo yenu sana. Ninapitia sijui niseme ni wakati mgumu au ni ujinga wa kujitakia. Niko kwenye mahusiano na mume wa mtu sasa yapata miaka mitatu. Imefikia hatua nimechoka na nahitaji kujing’atua ila nakosa njia nzuri ya kuachana nae. Am not even proud with what i did so if you judge me i’ll understand.

Huyu mtu tangu nafahamiana nae ameyabadilisha sana maisha yangu maana ana mchango mkubwa sana. Alinisaidia kupata kazi nzuri na kuachana na kakazi kangu nilikokuwa nafanya, alinihamisha na kunipangishia sehemu nzuri zaidi. Baadae alininunulia gari nami nikawa natembea nimekaa, pia amenijengea nyumba iliyo kwa jina langu ila kwakuwa ipo nje ya mji nimeipangisha nakula kodi ila bado analipia kodi hapa ninapoishi.

Mahusiano yalipoanza sikufikiria hata yangechukua miezi 6, ila sasa ni miaka mitatu+. Ni mwanaume anayejali sana ila ana wivu balaa. Ni mara kadhaa amekuwa akinitishia kuwa akigundua ninamsaliti atanikata shingo. Sasa huwa najiuliza huyu ni mume wa mtu, anatarajia kweli niwe na yeye tu ili iweje?

Sasa nimechoka jamani, natamani niwe na mpenzi wangu na sio mume wa mtu. Kuna huyu kijana nimeanza nae mahusiano sasa ni miezi 5, kusema kweli nampenda na ninaona kabisa nae ananipenda. Haya ndio aina ya mahusiano niyatakayo. Nimekuwa nikitafuta visingizio kuwa asije kwangu maana sio maadili ila ukweli ni kuwa naogopa mlipa kodi akijua atanitoa roho.

Huyu mume wa mtu nishamtafutia visingizio ili tuachane ila inashindikana. Natamani yeye ndio aanze ili asije kuwa na kinyongo. Ila kuna wakati najipa moyo kuwa nimwambie tu tuachane lakini nikikumbuka aliwahi kunikunja nusura anipige alipokuta msg asizozielewa kwenye simu nahisi kutetemeka. Aliwahi kunionyesha silaha anayomiliki, nilipomuuliza ni ya nini akasema hata mimi nikimletea ujinga ananifyatua. Japo ulikuwa utani ila niliogopa kusema kweli.

Balaa zaidi recently ameanza kung’ang’ania nimzalie. Nimekuwa nikijifanya mimba hazishiki ila kusema kweli natumia dawa zisishike maana siko tayari kuzaa nae. Kwanza nahisi kama suffocation maana ananibana sana. Kwangu anakuja tu muda wowote akijisikia, na ole wangu asinikute nyumbani ni tatizo kubwa. Kila ninachofanya anahitaji apate taarifa kwanza, yaani kama mkewe vile jamani.

Nimejaribu kuelezea haya ili angalau muelewe ni kwanini nahitaji msaada wa mawazo yenu ili nijikwamue kwenye hili shimo nililojichimbia. Nipeni ushauri naachanaje na huyu mwanaume bila kuleta madhara kwangu.
Ninyi wanawake huwa hamueleweki, hivi matukio ya watu kuuana kisa mapenzi unadhani ni ya kufikirika? ? Subiri wakumwage ubongo ndo utajua! Yaani umefanyiwa yote hayo eti unasema "...nipeni ushauri naachanaje na huyu mwanaume bila kuleta madhara kwangu" madhara yapo tena sana p#mbi wewe!
 
Back
Top Bottom