Nitajikita kwenye upande unao utaka wewe japo unaweza usiwe sahihi,
Kwanza amini hakuna kisichowezekana chini ya jua, ukiwa na nia thabiti na tayar kukabili yatokanayo na maamuzi yako itawezekana.
Pili, jikite kwenye kumjua huyo mwanaume wako mpya, umejenga uhusiano kwenye uongo,
1. anaweza akaujua ukweli na penzi pale pale likapungua.
2.Na huwez ficha ukweli daima
3. Wanaume almost wote tunafanana unalokimbia huku utakutana nalo kule(mchepuko, vitisho, wivu, etc) tathmini uone kama ndo unachohitaji
Ukishaona anafaa na ndo uende naye rudi Sasa kwenye uhalisia na hyu jamaa.
1. Amekupa maisha kiasi cha wewe kuweza kujisimamia na kutamka unaweza jitunza bila yeyote na bado ukajifanyia vyote alivyokufanyia... Sasa ondoa haya kwenye point za kutumia wakati unafanya maamuzi.
A/ Kamwe hutoweza kujificha popte asikupate... Nenda nchi yoyote ila kama aliweza kukupeleka kote huko, ni suala la muda tu. Akiwa na nature kama yangu, hata miaka 10 kulipia kisasi atavumilia.
B/ Hutoweza kumwacha nae akakubali kama utatumia Aina yoyote ya ubabe au kumchallenge. Ni hivi akiona njia uliyotumia ni Maji marefu( yaan kwa pesa na influence hakuwezi) atakaa chini na kujisuka aje strategically kukumaliza( na kwa summary ulotoa huna background powerful kiasi cha kumtisha hvo)
C/ Usiwazie suala la kumlipa, huna cha kumlipa, ni kama ingekuwa vice versa nae Hana cha kukulipa, kuliamsha Hilo ni kuonesha dharau kwa mambo meng yaliyoendelea mioyoni mwenu, nyakati na nia zenu, wala Usiwazie kwenda kwa mkewe kwa namna yoyote.
D/ Mungu unayemsema na kutaka kumrudia tambua hakushangai kwa haya maana anajua fika ungefanya hvo, atakacho kushangaa ni kutaka kumlaghai kwa kutubu kwako wakati tabia yako ilokusukuma kufanya hvo bado iko ndani yako na unaweza rudia tena na tena kosa Hilo hlo(rejea petro kumkana Yesu japo alijiapia hawezi kamwe)
Cha kufanya
Namna pekee kwangu nnayoiona ni kwa kupata huruma ya huyo mwanaume basi. Hyo huruma utaipataje, wewe ndo unamjua ilivyo.
Bila huyo mwanaume kupuuzia uamuzi wako au kufikia hatua ya kukuchukulia kama mpuuzi kiasi cha kuona bora aache kupoteza hela na muda kwako huna namna ya kibabe ya kumchomoa labda umuue, au ukeshe kwenye maombi.
Mwisho wa siku jitafakari na ww pia, je yaliyokukera ni kweli yana kero kwako? Au ni kwasababu mhusika ni hyu mhudumiaji?