Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Duh,una ubinafsi sana mwanaume aliyekufanyia kila kitu mpaka na familia yako kuingia na kutoka kwako ni jambo la kuhoji?
Aisee

Kuja haina tatizo ila basi atoe taarifa. Kuna wakati unastukia tu saa sita ya usiku katoka safari badala aende kwa mkewe anakuja kwangu!
 
Habari wanajamii forum, ni matumaini yangu kuwa mko salama. Ama la, basi Mungu awafanyie wepesi.

Ndugu zangu nahitaji msaada wa mawazo yenu sana. Ninapitia sijui niseme ni wakati mgumu au ni ujinga wa kujitakia. Niko kwenye mahusiano na mume wa mtu sasa yapata miaka mitatu. Imefikia hatua nimechoka na nahitaji kujing’atua ila nakosa njia nzuri ya kuachana nae. Am not even proud with what i did so if you judge me i’ll understand.

Huyu mtu tangu nafahamiana nae ameyabadilisha sana maisha yangu maana ana mchango mkubwa sana. Alinisaidia kupata kazi nzuri na kuachana na kakazi kangu nilikokuwa nafanya, alinihamisha na kunipangishia sehemu nzuri zaidi. Baadae alininunulia gari nami nikawa natembea nimekaa, pia amenijengea nyumba iliyo kwa jina langu ila kwakuwa ipo nje ya mji nimeipangisha nakula kodi ila bado analipia kodi hapa ninapoishi.

Mahusiano yalipoanza sikufikiria hata yangechukua miezi 6, ila sasa ni miaka mitatu+. Ni mwanaume anayejali sana ila ana wivu balaa. Ni mara kadhaa amekuwa akinitishia kuwa akigundua ninamsaliti atanikata shingo. Sasa huwa najiuliza huyu ni mume wa mtu, anatarajia kweli niwe na yeye tu ili iweje?

Sasa nimechoka jamani, natamani niwe na mpenzi wangu na sio mume wa mtu. Kuna huyu kijana nimeanza nae mahusiano sasa ni miezi 5, kusema kweli nampenda na ninaona kabisa nae ananipenda. Haya ndio aina ya mahusiano niyatakayo. Nimekuwa nikitafuta visingizio kuwa asije kwangu maana sio maadili ila ukweli ni kuwa naogopa mlipa kodi akijua atanitoa roho.

Huyu mume wa mtu nishamtafutia visingizio ili tuachane ila inashindikana. Natamani yeye ndio aanze ili asije kuwa na kinyongo. Ila kuna wakati najipa moyo kuwa nimwambie tu tuachane lakini nikikumbuka aliwahi kunikunja nusura anipige alipokuta msg asizozielewa kwenye simu nahisi kutetemeka. Aliwahi kunionyesha silaha anayomiliki, nilipomuuliza ni ya nini akasema hata mimi nikimletea ujinga ananifyatua. Japo ulikuwa utani ila niliogopa kusema kweli.

Balaa zaidi recently ameanza kung’ang’ania nimzalie. Nimekuwa nikijifanya mimba hazishiki ila kusema kweli natumia dawa zisishike maana siko tayari kuzaa nae. Kwanza nahisi kama suffocation maana ananibana sana. Kwangu anakuja tu muda wowote akijisikia, na ole wangu asinikute nyumbani ni tatizo kubwa. Kila ninachofanya anahitaji apate taarifa kwanza, yaani kama mkewe vile jamani.

Nimejaribu kuelezea haya ili angalau muelewe ni kwanini nahitaji msaada wa mawazo yenu ili nijikwamue kwenye hili shimo nililojichimbia. Nipeni ushauri naachanaje na huyu mwanaume bila kuleta madhara kwangu.
Huyo ni mumeo,Huko unakotaka kwenda kunaonesha una wenge.Au unafikiri MUME maana yake ni nini?Hivi nyie wanawake mnatuonaje wanaume.KAZI,KODI,NYUMBA,GARI,PENZI na bado unawashwa.Naweka BET huyo Jamaa ukiachana naye unaweza ukadanda maisha yako yote.MARK this POST
 
Fanya hivi:
1. Iba namba ya mkewe kwenye simu yake.
2. Tumia namba ngeni ujifanya msamaria umpe mkewe ubuyu kuwa mumeo anatembea na fulani na anampa mihela kibao ikiwezekana mtumie na namba yako ya simu ambayo sio main. Atakupigia na vagi litaanzia hapo.
3. NB uwe tayari kurudisha nyumba au gari maana atakunyanyasa navyo ila usimpe vyote maana naye kakulegeza misuli hawezi kukulipa.
4. Ushike msimamo kuwa hutaki tena mkewe keshajua nuachane. Huyo nwanamke gakikisha unamwambia ni kweli ila aliniambia mmetengana ila samahani sana mana nisamehe sirudii.

Alishawahi sema mkewe akijua ndio vizuri ili tuwe huru.
 
Habari wanajamii forum, ni matumaini yangu kuwa mko salama. Ama la, basi Mungu awafanyie wepesi.

Ndugu zangu nahitaji msaada wa mawazo yenu sana. Ninapitia sijui niseme ni wakati mgumu au ni ujinga wa kujitakia. Niko kwenye mahusiano na mume wa mtu sasa yapata miaka mitatu. Imefikia hatua nimechoka na nahitaji kujing’atua ila nakosa njia nzuri ya kuachana nae. Am not even proud with what i did so if you judge me i’ll understand.

Huyu mtu tangu nafahamiana nae ameyabadilisha sana maisha yangu maana ana mchango mkubwa sana. Alinisaidia kupata kazi nzuri na kuachana na kakazi kangu nilikokuwa nafanya, alinihamisha na kunipangishia sehemu nzuri zaidi. Baadae alininunulia gari nami nikawa natembea nimekaa, pia amenijengea nyumba iliyo kwa jina langu ila kwakuwa ipo nje ya mji nimeipangisha nakula kodi ila bado analipia kodi hapa ninapoishi.

Mahusiano yalipoanza sikufikiria hata yangechukua miezi 6, ila sasa ni miaka mitatu+. Ni mwanaume anayejali sana ila ana wivu balaa. Ni mara kadhaa amekuwa akinitishia kuwa akigundua ninamsaliti atanikata shingo. Sasa huwa najiuliza huyu ni mume wa mtu, anatarajia kweli niwe na yeye tu ili iweje?

Sasa nimechoka jamani, natamani niwe na mpenzi wangu na sio mume wa mtu. Kuna huyu kijana nimeanza nae mahusiano sasa ni miezi 5, kusema kweli nampenda na ninaona kabisa nae ananipenda. Haya ndio aina ya mahusiano niyatakayo. Nimekuwa nikitafuta visingizio kuwa asije kwangu maana sio maadili ila ukweli ni kuwa naogopa mlipa kodi akijua atanitoa roho.

Huyu mume wa mtu nishamtafutia visingizio ili tuachane ila inashindikana. Natamani yeye ndio aanze ili asije kuwa na kinyongo. Ila kuna wakati najipa moyo kuwa nimwambie tu tuachane lakini nikikumbuka aliwahi kunikunja nusura anipige alipokuta msg asizozielewa kwenye simu nahisi kutetemeka. Aliwahi kunionyesha silaha anayomiliki, nilipomuuliza ni ya nini akasema hata mimi nikimletea ujinga ananifyatua. Japo ulikuwa utani ila niliogopa kusema kweli.

Balaa zaidi recently ameanza kung’ang’ania nimzalie. Nimekuwa nikijifanya mimba hazishiki ila kusema kweli natumia dawa zisishike maana siko tayari kuzaa nae. Kwanza nahisi kama suffocation maana ananibana sana. Kwangu anakuja tu muda wowote akijisikia, na ole wangu asinikute nyumbani ni tatizo kubwa. Kila ninachofanya anahitaji apate taarifa kwanza, yaani kama mkewe vile jamani.

Nimejaribu kuelezea haya ili angalau muelewe ni kwanini nahitaji msaada wa mawazo yenu ili nijikwamue kwenye hili shimo nililojichimbia. Nipeni ushauri naachanaje na huyu mwanaume bila kuleta madhara kwangu.
Hayo ndio hua matatizo yenu mtu kakufanyia yote hayo mazuri na sababu zinakuja baada ya kupata hako ka kijana haya uko tayari kurudisha vitu vyote ulivyo nunuliwa au kuvunjwa miguu
 
Naona unahangaika bure tu, kwa uandishi wako unaonekana bado ni mtoto. Hauwezi kuwa muhusika hata kidogo na wala hatumii Jamii forums. Mimi gari ninayo mwaka wa tatu sasa na mwaka jana ndio alinibadilishia kaIST na kuninunulia vanguard ninayotumia sasa. Gari la kwanza alininunulia baada ya miezi 6 ya mahusiano, Na yote yako kwa majina yangu kabisa.
Naona unatafuta kifo surely u will die hat ukirudisha unaenda kulosse hii Vita na utaibika
 
Nakuonea huruma sa wewe na wazazi wako,huna maisha marefu yaani,chakufa ya rudisha kila kilicho chake alafu umwambie ukweli
 
mama atajengewa nyumba ndio utashangaa mama naye anasema mwanangu wewe mzalie tuu muhimu huduma

Hahahaaa nimecheka kama mazuri, hajajengewa ila alifanyiwa ukarabati mkubwa nyumba ikawa ya kisasa zaidi.
 
Wabona...mie nilijua tuu. Wamama wetu bwana wapuuzi sana ikija suala la watoto wao wa kike wakihudumiwa na mume wa mtu...hawakaripii kabisaaaa. Nilionaga hili kwa bibi yangu tuwards mama yangu mdogo....yeye alikuwa anapokea tuu hajali kuwa mwanae anajenga matatuzo tuu
 
Nitajikita kwenye upande unao utaka wewe japo unaweza usiwe sahihi,

Kwanza amini hakuna kisichowezekana chini ya jua, ukiwa na nia thabiti na tayar kukabili yatokanayo na maamuzi yako itawezekana.

Pili, jikite kwenye kumjua huyo mwanaume wako mpya, umejenga uhusiano kwenye uongo,
1. anaweza akaujua ukweli na penzi pale pale likapungua.
2.Na huwez ficha ukweli daima
3. Wanaume almost wote tunafanana unalokimbia huku utakutana nalo kule(mchepuko, vitisho, wivu, etc) tathmini uone kama ndo unachohitaji

Ukishaona anafaa na ndo uende naye rudi Sasa kwenye uhalisia na hyu jamaa.

1. Amekupa maisha kiasi cha wewe kuweza kujisimamia na kutamka unaweza jitunza bila yeyote na bado ukajifanyia vyote alivyokufanyia... Sasa ondoa haya kwenye point za kutumia wakati unafanya maamuzi.

A/ Kamwe hutoweza kujificha popte asikupate... Nenda nchi yoyote ila kama aliweza kukupeleka kote huko, ni suala la muda tu. Akiwa na nature kama yangu, hata miaka 10 kulipia kisasi atavumilia.

B/ Hutoweza kumwacha nae akakubali kama utatumia Aina yoyote ya ubabe au kumchallenge. Ni hivi akiona njia uliyotumia ni Maji marefu( yaan kwa pesa na influence hakuwezi) atakaa chini na kujisuka aje strategically kukumaliza( na kwa summary ulotoa huna background powerful kiasi cha kumtisha hvo)

C/ Usiwazie suala la kumlipa, huna cha kumlipa, ni kama ingekuwa vice versa nae Hana cha kukulipa, kuliamsha Hilo ni kuonesha dharau kwa mambo meng yaliyoendelea mioyoni mwenu, nyakati na nia zenu, wala Usiwazie kwenda kwa mkewe kwa namna yoyote.

D/ Mungu unayemsema na kutaka kumrudia tambua hakushangai kwa haya maana anajua fika ungefanya hvo, atakacho kushangaa ni kutaka kumlaghai kwa kutubu kwako wakati tabia yako ilokusukuma kufanya hvo bado iko ndani yako na unaweza rudia tena na tena kosa Hilo hlo(rejea petro kumkana Yesu japo alijiapia hawezi kamwe)

Cha kufanya

Namna pekee kwangu nnayoiona ni kwa kupata huruma ya huyo mwanaume basi. Hyo huruma utaipataje, wewe ndo unamjua ilivyo.

Bila huyo mwanaume kupuuzia uamuzi wako au kufikia hatua ya kukuchukulia kama mpuuzi kiasi cha kuona bora aache kupoteza hela na muda kwako huna namna ya kibabe ya kumchomoa labda umuue, au ukeshe kwenye maombi.

Mwisho wa siku jitafakari na ww pia, je yaliyokukera ni kweli yana kero kwako? Au ni kwasababu mhusika ni hyu mhudumiaji?

Asante.
 
Ushauri wangu upo tofauti na wa wanaume wengi, si umesema nyumba na gari vipo kwenye jina lako? basi hakuna kurudisha, ndio ukumbusho wa penzi lenu, unapolipiwa kodi hama, kapange pengine. Mwanaume mwenye uwezo wa kukujengea nyumba, kukununulia gari na kukupeleka vacations bila kuwaza hawezi kupoteza muda wake kukusumbua urudishe vyake penzi linapoisha, off course atakuwa disappointed na wewe lakini iyo wewe haikuhusu coz you are looking after your own best interests.

Kuhusu kumuacha mshua kwenda kwa mshkaji, hakikisha unapoenda ni upgrade ya ulipotoka, some fellas look good on paper( kazi nzuri, gari nzuri, kapanga pazuri) lakini ukishaingia ndani ya mahusiano unagundua it's all a facade, mchizi anateseka na madeni yasiyolipika to mantain his lifestyle, hapo ujamuongezea majukumu ya mke na watoto. Play your cards right.

Ni bora kuwa mchepuko wa mwanaume mwenye uhakika wa maisha kuliko kuwa mke wa ndoa wa mwanaume anayebahatisha maisha.

Asante.
 
Nilitaka kuongea neno ila naona umemaliza. Hasa nyumba!!!!!! Kagari na mengine anaweza kusahau ila nyumba, thubutu. Hata sie tulikuwa na michepuko ambayo ni under 25, tulienda sawa ila ikifika 25 inaanza kulazimisha ipate usafiri na kujengewa nyumba. Msichana ambaye anajitambua kama sex partner, ataomba hela ya Bolt na si kutaka anunuliwe gari. Ataomba hela ya kupanga chumba na sebule si kujengewa nyumba maana kujenga ni kuinvest bandugu.

Mimi hivyo vyote sikuwahi kuomba, alifanya kwa mapenzi yake binafsi.
 
Habari wanajamii forum, ni matumaini yangu kuwa mko salama. Ama la, basi Mungu awafanyie wepesi.

Ndugu zangu nahitaji msaada wa mawazo yenu sana. Ninapitia sijui niseme ni wakati mgumu au ni ujinga wa kujitakia. Niko kwenye mahusiano na mume wa mtu sasa yapata miaka mitatu. Imefikia hatua nimechoka na nahitaji kujing’atua ila nakosa njia nzuri ya kuachana nae. Am not even proud with what i did so if you judge me i’ll understand.

Huyu mtu tangu nafahamiana nae ameyabadilisha sana maisha yangu maana ana mchango mkubwa sana. Alinisaidia kupata kazi nzuri na kuachana na kakazi kangu nilikokuwa nafanya, alinihamisha na kunipangishia sehemu nzuri zaidi. Baadae alininunulia gari nami nikawa natembea nimekaa, pia amenijengea nyumba iliyo kwa jina langu ila kwakuwa ipo nje ya mji nimeipangisha nakula kodi ila bado analipia kodi hapa ninapoishi.

Mahusiano yalipoanza sikufikiria hata yangechukua miezi 6, ila sasa ni miaka mitatu+. Ni mwanaume anayejali sana ila ana wivu balaa. Ni mara kadhaa amekuwa akinitishia kuwa akigundua ninamsaliti atanikata shingo. Sasa huwa najiuliza huyu ni mume wa mtu, anatarajia kweli niwe na yeye tu ili iweje?

Sasa nimechoka jamani, natamani niwe na mpenzi wangu na sio mume wa mtu. Kuna huyu kijana nimeanza nae mahusiano sasa ni miezi 5, kusema kweli nampenda na ninaona kabisa nae ananipenda. Haya ndio aina ya mahusiano niyatakayo. Nimekuwa nikitafuta visingizio kuwa asije kwangu maana sio maadili ila ukweli ni kuwa naogopa mlipa kodi akijua atanitoa roho.

Huyu mume wa mtu nishamtafutia visingizio ili tuachane ila inashindikana. Natamani yeye ndio aanze ili asije kuwa na kinyongo. Ila kuna wakati najipa moyo kuwa nimwambie tu tuachane lakini nikikumbuka aliwahi kunikunja nusura anipige alipokuta msg asizozielewa kwenye simu nahisi kutetemeka. Aliwahi kunionyesha silaha anayomiliki, nilipomuuliza ni ya nini akasema hata mimi nikimletea ujinga ananifyatua. Japo ulikuwa utani ila niliogopa kusema kweli.

Balaa zaidi recently ameanza kung’ang’ania nimzalie. Nimekuwa nikijifanya mimba hazishiki ila kusema kweli natumia dawa zisishike maana siko tayari kuzaa nae. Kwanza nahisi kama suffocation maana ananibana sana. Kwangu anakuja tu muda wowote akijisikia, na ole wangu asinikute nyumbani ni tatizo kubwa. Kila ninachofanya anahitaji apate taarifa kwanza, yaani kama mkewe vile jamani.

Nimejaribu kuelezea haya ili angalau muelewe ni kwanini nahitaji msaada wa mawazo yenu ili nijikwamue kwenye hili shimo nililojichimbia. Nipeni ushauri naachanaje na huyu mwanaume bila kuleta madhara kwangu.
Ni rahisi tu, njoo uwe mchepuko wangu, wakati yupo na mkewe, wewe unakuwa na Mimi, akishutuka na kukuacha tunafunga ndoa!
 
Wabona...mie nilijua tuu. Wamama wetu bwana wapuuzi sana ikija suala la watoto wao wa kike wakihudumiwa na mume wa mtu...hawakaripii kabisaaaa. Nilionaga hili kwa bibi yangu tuwards mama yangu mdogo....yeye alikuwa anapokea tuu hajali kuwa mwanae anajenga matatuzo tuu

Mama yangu hajui kama ni mume wa mtu, anajua ni mchumba wangu hivyo anauliziaga tu ndoa na wajuiuu lini? Sijui nikimueleza ukweli itakuwaje?
 
Mama yangu hajui kama ni kume wa mtu, anajua ni mchumba wangu hivyo anauliziaga tu ndoa na wajuiuu lini? Sijui nikimueleza ukweli itakuwaje?
Hatari hiyo...dah wee kweli umelikoroga. Sasa unataka kumkatili mama vyuku maburger ya mume wa mtu kwa kwenda kutafuta true love🤔🤔🤔🤔🤔
 
Kama unataka kuachana naye, mwombe ndoa. Na unajua hatokubali kwa vile ana mke tayari (unless awe muislamu). Akikataa, unamwambia umekuwa mtu mzima sasa, akuruhusu upate mwenza uolewe na uanzishe familia yako. Ktk mazingira hayo ni rahisi kuondoka. Hauwezi kuwa kimada mpaka uzeeni. Simple...
Inatokea tu.
 
Back
Top Bottom