Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Wapendwa badala mnipe ushauri mnaniongezea magazijuto kweli? Najua i messed up big time and an not proud. Nisaidieni najikwamuaje hapa.
Kwanza tubu, alafu mtafute mkewe, muombe muonane, mueleze jinsi ambavyo unajutia matendo yako, alafu mkabidhi nyumba, gari ulilopewa na mume wake. Najua ni ngumu kuachilia mali lakini shhukuru bado una kazi, jiwekeze kidogo kidogo utafanikiwa. Ila ukiendelea kupenda vya bure utaliwa, utazalishwa, ukianza kuzeeka mwenzio anakwambia nimeokoka tena anatoa ushuhuda kanisani kuhusu wewe , mtoto anampeleka boarding school na mapenzi unakosa unabaki kuwa sugarmama
 
Kwanza nikwambie Hapo huwezi kutoka kwenye kifungo icho ulichokuwepo labda aamue mwenyew kukupotezea au Mungu amchukue, Si rahisi yeye kukuelewa kwa chchte kwa sababu ashawekeza vitu vingi kwako Ila all in all ulisema alikuonesha bastola kimasihara hio ilikua masihara Ila alifanya vile very serious so Kua makini Kama unataka umuache anza na kurejesha vitu vyake
mkuu ukimwambia hivi utamfanya mdada aanze mbinu za kumuua jamaa ili atoke kwenye kifungo
 
Wapendwa badala mnipe ushauri mnaniongezea magazijuto kweli? Najua i messed up big time and an not proud. Nisaidieni najikwamuaje hapa.
Acha kuact kijinga , kwanza just imagine wewe ndo ungekuwa huyo jamaa, umejitoa mwili na roho kumfanya mpenz wako awe na furaha and comfortable then after lots of hustles anakuja na kauli Sijui za Ku-suffocate !!! My dear yakikuta ya kukukuta ujue mchawi ni wewe mwenyewe!

Oops walisema mchumba hasomeshwi kwa uzi wako huu nadhani naongezea Mchepuko usiufanyie maendeleo!
Hivi wadhani huyo jamaa Hana ndugu/wazazi wenye shida akawajengea na kuwafanyia ukarimu woote huu alokufanyia? Mkuu just kuwa na utu aisee na Mtoto wa mwanamke mwenzio.
 
wee bwana warembo wa mujini walishazoea life zuri unadhani kuviachia hivyo vitu inakuwa rahisi kihivyo bwana. cha msingi bidada yeye aendelee kumpa jamaa mbusus basi na kumwambia ukweli kuwa mie kwa sasa siwezi kuzaa na mume wa mtuile kutombaaa wee tombaaa tuu style zote utaakazo
Hahahahaha
 
Kama umemchoka tupasie namba zake kuna ndugu yangu ana shida nazo.(jokes)

Pole dada..
 
Habari wanajamii forum, ni matumaini yangu kuwa mko salama. Ama la, basi Mungu awafanyie wepesi.

Ndugu zangu nahitaji msaada wa mawazo yenu sana. Ninapitia sijui niseme ni wakati mgumu au ni ujinga wa kujitakia. Niko kwenye mahusiano na mume wa mtu sasa yapata miaka mitatu. Imefikia hatua nimechoka na nahitaji kujing’atua ila nakosa njia nzuri ya kuachana nae. Am not even proud with what i did so if you judge me i’ll understand.

Huyu mtu tangu nafahamiana nae ameyabadilisha sana maisha yangu maana ana mchango mkubwa sana. Alinisaidia kupata kazi nzuri na kuachana na kakazi kangu nilikokuwa nafanya, alinihamisha na kunipangishia sehemu nzuri zaidi. Baadae alininunulia gari nami nikawa natembea nimekaa, pia amenijengea nyumba iliyo kwa jina langu ila kwakuwa ipo nje ya mji nimeipangisha nakula kodi ila bado analipia kodi hapa ninapoishi.

Mahusiano yalipoanza sikufikiria hata yangechukua miezi 6, ila sasa ni miaka mitatu+. Ni mwanaume anayejali sana ila ana wivu balaa. Ni mara kadhaa amekuwa akinitishia kuwa akigundua ninamsaliti atanikata shingo. Sasa huwa najiuliza huyu ni mume wa mtu, anatarajia kweli niwe na yeye tu ili iweje?

Sasa nimechoka jamani, natamani niwe na mpenzi wangu na sio mume wa mtu. Kuna huyu kijana nimeanza nae mahusiano sasa ni miezi 5, kusema kweli nampenda na ninaona kabisa nae ananipenda. Haya ndio aina ya mahusiano niyatakayo. Nimekuwa nikitafuta visingizio kuwa asije kwangu maana sio maadili ila ukweli ni kuwa naogopa mlipa kodi akijua atanitoa roho.

Huyu mume wa mtu nishamtafutia visingizio ili tuachane ila inashindikana. Natamani yeye ndio aanze ili asije kuwa na kinyongo. Ila kuna wakati najipa moyo kuwa nimwambie tu tuachane lakini nikikumbuka aliwahi kunikunja nusura anipige alipokuta msg asizozielewa kwenye simu nahisi kutetemeka. Aliwahi kunionyesha silaha anayomiliki, nilipomuuliza ni ya nini akasema hata mimi nikimletea ujinga ananifyatua. Japo ulikuwa utani ila niliogopa kusema kweli.

Balaa zaidi recently ameanza kung’ang’ania nimzalie. Nimekuwa nikijifanya mimba hazishiki ila kusema kweli natumia dawa zisishike maana siko tayari kuzaa nae. Kwanza nahisi kama suffocation maana ananibana sana. Kwangu anakuja tu muda wowote akijisikia, na ole wangu asinikute nyumbani ni tatizo kubwa. Kila ninachofanya anahitaji apate taarifa kwanza, yaani kama mkewe vile jamani.

Nimejaribu kuelezea haya ili angalau muelewe ni kwanini nahitaji msaada wa mawazo yenu ili nijikwamue kwenye hili shimo nililojichimbia. Nipeni ushauri naachanaje na huyu mwanaume bila kuleta madhara kwangu.
Tafuta namba ya mkewe halafu tafuta simu ya bodaboda mtumie mkewe msg ujishitakie kuwa mumewe anatoka na wewe.
 
Miaka 3 kwenye mahusiano nyinyi ni mme na mke na mtaachana kwa taraka. Au fanya hivi Mrudishie gharama zake zote alizotumia kwako then muache bila kufanya hivyo my dear utakufa tu
 
Sijui nani atatuletea mrejesho juu ya kuchomwa na gunia mbili za mkaa ama kupigwa risasi ya ubongo maana wakati huo mleta mada atakuwa marehemu.

Anyways tukiona kimya kirefu kutoka kwako tujue tu ndo basi tena.

Yaani kila siku unasikia mauaji mapya kuhisiana na mapenzi halafu nawewe unaleta mzaha.

Kwanza akigundua tu una huo mchepuko anaweza akakutwanga risasi papo hapo jiandae.
Daah🤣🤣
 
Yaani wataalam wa afya huwa wanatuambia kula wanga na mafuta mengi kunasababisha pressure na kisukari Ila kwa watanzania wengi hasa wanaume michepuko ndo huwa inawasababishia pressure na stroke juu 😄😄😄 yaani huyo father house siku akijua unachowaza au akikufumania na huyo kijana atakuua na asipokuua msongo wa mawazo utazaa pressure na maradhi mengine halafu mke wake ndo ataanza kumuuguza Sasa na kumpikia chukuchuku na chumvi kwa mbaliii, michepuko nyie mbingu mtaisikia tu.
 
ifike mahala wanawake nasisi tujikwamue TU kutoka kwa waume zawatu mwisho wa siku mwanaume atatubu na kubaki na familia yake tu amekufuuuuuuuuujjjaaa huku wewe umri ushasonga aargghhh!
Na wanaume nao vichomi tu baada apambane na mkewe anakimbilia wa vibinti mwisho ndio haya sasa!
Hamuwezi kubadilika hata siku Moja hkn Niko nadate na mke wa mtu Ni mpumbafu wa Hali ya juu mpk naona aibu mm kwa jins anavyo mfanyia mumewake Ni aibu wanawake wanao jielewa Sasa HV Ni 10 %
 
Hawezi kufa...

Anamtishia hivyo sababu anajua hajaolewa ila akiolewa hana mamlaka nae tena...
anamtisha sio!!!! vp hayo magari na majumba aliyoinvest kwake? kibinadamu tuu na hata kwa hali ya kawaida unazani hata kama ni wewe ungemuacha tuu aende na mali zako kwa mwanaume mwingine?

hapo lazma arudishe vya watu, ndo akaolewe huko anapotaka kwenda, la sivyo ajiandae kubanikwa kwenye magunia ya mkaa wa moto, na hakuna atakae muurumia maana ni halali yake.
 
Back
Top Bottom