Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

nenda kamshitaki kwa mke wake na umwambie yote haya. ukimaliza hapo mwombe msamaha mwanamke mwenzio, na ukatubu kwa Mungu ili uanze maisha mapya. hayo aliyokutendea ni makaratasi tu, ni upepo tu, na umekufanya ukatengana na Mungu wako, hapo ulipo unaelekea jehanamu ya moto wa milele. furahia mali zinazotoka kwa Mungu sio hizo zinatoka kwa shetani. our God is a lifter of men, he can lift you hata zaidi ya huyo mume wa mtu.

nakuhakikishia kama ameshakugharimiia sana, hauwezi kumwacha kirahisi. dawa yake ni na wewe kuingia kwenye moto/mdomo wa simba, tafuta hata mtu fulani tu akamtonye mkewe kwamba mume wako anakufuatilia, akija kwako mwambie ni kweli ananifuatafuata, waachie msala huo uone kama hamtaachana. dawa ya moto ni moto.
 
rudisha vitu vya mtu ndio uendelee na maisha yako na huyo mpenzi wako ...kakupendezesha sasa unajifanya kuwa akili imerudi ...nje ya hapo kweli utakufa hakika nakwambia hakunaga mwanaume mjinga aliyekugharamia halafu apotezee tu ni lazima aone namna ya kurudisha gharama zake
 

Ayeeee jamani [emoji1787][emoji1787][emoji1787] weee una hela au unatoka kusumbua dada wa watu
 
Unajengewa nyumba, ulifikiri huyo mpita njia?
 
1. Hukumuomba asiheshimu ndoa yake, hakuiheshimu akakutongoza...na wewe hukuiheshimu ukamkubali.

2. Hukumuomba akujengee nyumba, ni kiherehere chake, badala ya kujengea mkewe na watoto akaamua kutapanya

3. Hukumuomba akununulie gari, inawezekana mkewe hajawahi mnunulia ila ametapanya


4. Muite, ukiwa na ukinzi [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] mwambie mahusiano yenu yamefika mwisho arudi kwa mkewe.

5. Hama anapokulipia kodi ujilipie mwenyewe

6. Kata RB

7. Tembea na ulinzi atakukata shingo kwelj huyo ohooooo


8. Muachage kutembea na waume za wenyewe.....matokeo yake mkishachuma ndio mnajiona mnahitaji wa kwenu peke yenu
 
Ameyabadilisha maisha yako na sasa anaenda kuyakatisha maisha yako.

Rudisha vyake, kwa aliyofanya na mmekua pamoja kwa miaka 3 manake jamaa kawekeza sana, sasa hakuna muwekezaji anaeacha mradi wake kiwepesi.
 
Hyo inaitwa love desire, and obession kutoka kwa huyo bwana, kwakuwa alishakupa maisha ya ganda la ndizi nawewe ukawa unafurahi pasipo kucheki negative impact hayo ndio mazara yake, kama unataka rudisha nyumba aliyokujengea , gari, hapo alipokukupangishia, kazi aliyokuwezesha, rudi katika maisha yako ya mwanzo...,, kama unaona hyo nishida nautaki kurudi ulikotoka kimaisha "hapo naisi harufu ya damu kumwagika"
 
Rudisha gari na nyumba,Kisha Anza kulipa Kodi,ACHA hiyo kazi uliyopewa Kisha ungana na huyu kijana mmefahamiana miezi 5 uone kama kijana atakaa hapo na mizinga yako
 
Hapo kwenye akili hapo..
wanawake tunajisahau sana kwa kweli.. haswa ukiwa unaachiwa kodi ya meza nzuri halafu ubaya wa hiyo kodi ya meza sasa.. huwa haitolewi mpaka jambo fulani likamilike😂😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…