Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Tatizo huwa ni nini mpaka mnaingia kwenye mahusiano na mume wa mtu?.?.. Lengo lako kuu ilikuwa ni nini mpaka unaingia kwenye mahusiano na mume wa mtu angali wajua ana mke?. .

Shida ni TAMAA ambayo inaenda kukuponza maana naona huyu jamaa anaweza kukufanya kitu kibaya ama huyo Kijana uliyenae asiye na hatia.

Ushauri ni huu. Anza kurudisha vitu vyake kwanza vyote kama nyumba na gari. Ikiwezekana acha na kazi aliyokutafutia kisha mwambie unataka kuanza upya maisha yako maana unahisi humtendei haki mke wake, . Mwambie dhamiri inakusuta na kama ungekuwa wewe mkewe usingependa mume wako awe na mahusiano nje na kimada.

Kwa kurudisha vitu utakuwa umejiweka huru kwa 75% na kwa kumwambia utakuwa umefika 98%, hiyo 2% iliyobaki ni yeye kuamua sasa. Maana Vitu ndio vinakufunga.

Na ukimwacha na akajua unamtu mwingine ambaye anatumia vitu vyake lazima itamuuma sana na itaonekana kwake kuwa wewe ulimfanya Sponsor wa kupata vitu ili ukavitumie na umpendaye.
 
Ninaona njia rahisi ya kuwaachanisha ni mauti.
Muda wote mtu anawejeza ulikuwa unafurahia.
Subiri cha moto hamna namna.
 
Umemaliza
 
Hapa hachomoki...kuchomoka pekee ni kifo
 
Nimeipenda
 
Knock yourself out, gal...

But remember...

...if he was able to give you a decent job, he can also be able take it away!

...if he was able to get you a nice house, he can also be able to send you back to where you exactly belong!! Unadanganyika na kuona jina lako kwenye makaratasi ndo ushajiona Mama Mwenye Nyumba, sio?

...if he was able to buy you a car, he can also be able to make you daladala girl!

Good luck!!
 
M
Mwambie amuache mke wake Halafu akuoe wewe,
Hakika Atakataa na icho ndo unachokitaka akishakataaa unamrudishia nyumba na gari unaanza maisha mapya na huyo unayemtaka.

Akikubali kumuacha mke wake pia uta mind vilevile maana mwanaume mpumbavu ndo anaweza kuacha mke wake maana yake na wewe badae anaweza kukiacha, unamrudishia nyumba na gari halafu unaachananae.
 
Nitaweza vizuri tu, nimejijenga vya kutosha na akiba bank si haba.
Sista, huyo mshua ndio "aliyekujenga".

Hiyo "akiba bank" ni kwa sababu ya huyo Mshua. Unapokea pesa ya kodi ya nyumba uliyojengewa, mekupangishia nyumba ambayo yeye ndo analipa kodi, akakutafutia kazi ambayo mshahara sio haba, akakununulia gari(ambalo pia mazaga yote kutoka mafuta mpaka service anaweza akawa nahudumia yeye), kakununulia viwanja(ambavyo pia hata kodi ya viwanja hivyo atakuwa analipia yeye), bado anakuhudumia na mishe nyingine. Pesa yako/mshahara wako unakuwa hauna kazi hapo, kila kitu unapewa. Na bado alisaidia familia yako na wanamfahamu(unafikiri ilikuwa bahati mbaya yeye kufanya hivyo?! Niamini sista hiyo ilikuwa makusudi kabisa.)
Mshua kakutoa katika level moja ya maisha kakupeleka level nyingine, ambayo kwa juhudi zako binafsi labda ingechukua zaidi ya miaka mitatu. Ndani ya miaka mitatu status yako imebadilika kabisa, wewe wa sasa ni "land lady","Land owner","mmiliki wa chimbo cha usafiri(bila shaka na driving school alikupeleka mshua, kwa hivyo akakuongezea na skill hapo, "driving")",
Mshua alikuondolea shida zako kwa asilimia 90 hadi 99(shida nyingi zinasababishwa na kutokuwa na pesa ama koneksheni), akakuondolea stress za ajabu ajabu. Uhuru wako mpya(ambao hapo kabla uliutumia kutatua shida zako) ndo huo huo unakwambia unashida mpya, ambayo ni huyo mshua.

Huyo mshua ndo kakujenga. Akiamua kukubomoa huwezi pingana nae kivyovyote vile

Unawaza kurudisha mali tu. Je, muda wake ? hisia zake? Utazirudishaje? (Usije sema ooh muda wako, hisia zako, kwa sababu kwa unchokisema huo muda wako na hisia zako ni Feki tu, hazikuwa za ukweli hata punje.)
Utasema amekutumia, la hasha, wewe ndo umemtumia. Mshua kajitoa mazima kwako, wewe unajitoa kwa kujifikiria sana.

"All is Fair in Love and War."
 
Rudisha vyote ulivyohongwa na huyo mwanaume,vinginevyo tutakusikia ukitangazwa kwenye vyombo vya habari roho imeachana na mwili.
 
Umeingia mdomoni mwa mamba hautoki Leo Wala kesho, HUYO unayempenda mwambie akupe gari,nyumba,mhamie mkaanze maisha,mme wa mtu huyo mtumie sms kwenda kwa MKE wake andika JINA LAKE na maneno baba fulani kuwa nipo tayari kukuzalia mtoto...utakuja unishukuru
 
Sasa kama moyoni hampendi na wala hisia naye hana afanyeje ?

Iwapo akiwa naye raha ya nafsi haipati afanyeje?
Mkuu,unafikri kinachomsumbua ni kwamba hampendi na moyoni hana nafasi?Hapana.Kuna kitu kinaitwa wenge.Wenge kwenye mapenzi humfanya mtu afikiri kwamba hampendi mtu ila unakuta ni wenge tu linamsumbua hasa ukizingatia wako wawili.Kwa nionavyo mimi na kwa uzoefu wangu mimi hili wengi hupata watu wengi sana hasa pale wanapohisi hawamtegemei sana yule mtu emotionally au financially na kuwa na ile kauli ya I can do without them.Kwa wanaume huwe tunajikuta wanadharau wapenzi wao na kuangaika ni videmu na kwa wanawake huwa wanakuwa na dharau hata kama hawana wapenzi wengine.

Sasa uhusiano ukivunjika wenge linatoka then reality inakuja na ule usemi wa kiswahili wa PEMA UKIPEMA SI PEMA TENA.
 
Rudisha vyote ulivyohongwa na huyo mwanaume,vinginevyo tutakusikia ukitangazwa kwenye vyombo vya habari roho imeachana na mwili.
Hta akirudisha bado jamaa atafanya maamuzi magumu.Kwa kiwango cha uwekezaji ina maana jamaa anampenda na ana mpango nae so whatever she does will not end easily.
 
Nimeipenda

Ushauri huu ni mzuri kama ana uhakika na anachotaka kufanya na SIO wenge.I have seen many GOOD girls wakijaribu hii strategy na ikawork lakini wakaishia kuumizwa wao tena sana
 
Rudisha vyote ulivyohongwa na huyo mwanaume,vinginevyo tutakusikia ukitangazwa kwenye vyombo vya habari roho imeachana na mwili.
Huyu ata arudishe vyote bado ataliwa tigo na atapotezwa. Usalama wake yeye aendelee tuu na huyo mume wa mtu ama kama vipi atafute cyanide
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…