Binti Sayuni03
JF-Expert Member
- Jan 21, 2025
- 1,075
- 1,913
Habari za wakati huu wana JF ni matumaini yangu mu wazima wa Afya.
Bila kupoteza muda twende kwenye jambo husika tajwa hapo juu.
Mimi ni msichana, kipindi nasoma kuna maisha nilikuwa naishi hapo nyuma hayakuwa mazuri nadhani ni kwasababu ya utoto na kutojitambua pia, ama ni ile foolish age pia ilichangia.
Kwasasa nimekua nina kibarua nafanya nimeshakuwa kwenye mahusiano kadhaa kadhaa lakini tulishindwana, pia watu niliokuwa nao kwenye mahusiano hawakuwa tayari nadhani au walikuwa na watu wao.
Mwaka jana nilibahatika kuanzisha mahusiano na mwanaume mmoja mpaka sasa hivi nipo nae lakini hatuko kwenye mkoa mmoja, sasa jambo ninalohofia ni kwamba ikitokea siku akafatilia background yangu akaambiwa maisha niliyoishi hapo nyuma itakuwaje na mimi sijawahi kumwambia, nahofia akija kujua anaweza kuniacha.
Ninaomba ushauri wenu wadau je ni sahihi mimi kumweleza mpenzi wangu ukweli wa maisha niliyopitia hapo nyuma au ninyamaze tu haina umuhimu??