Kwa hili exactly tutumie comment ya kwanza ya denno amejibu kwa usahihi sidhani kama kuna fact nyingine, it’s purely sababu za kimaumbilie ambazo zinaathiri mambo chungu tele kwa wanawake na kutuweka nyuma ya wanaume functional wise.
Again hili linaangukia katika kile ambacho sisi wa kundi letu ndio tumeziita disparities (tumezipa mzani wa uchache) na kinyume chake ni similarities (sisi wa kundi letu tumezipa uzani wa nyingi)
Ambapo kwa muono wangu hisia au matumizi ya hisia yanatuathiri wanawake katika functionality level mathalani tukiwa na mood swings inaweza kuathiri uwezo wetu wa kupata matokeo chanya/makubwa katika tunachokishughulikia, kutokuact accordingly au kuoveract. Haya ni madhara ya mwanamke kuwa mnyama wa kihisia. Reflection yake tunaiona katika
1. Matumizi huruma kupitiliza
2.Kuamini kwa haraka
3.Kutuexpose kuhusu tunavyopenda na tusivyopenda kwa haraka
4.Kutengeneza bias sababu ya kutumia hisia katika kuangalia mambo
5.Kuonesha hasira, hofu, chuki
6.Msongo wa mawazo
7.Uvivu/kukosa motivation etc
Ikiwa ulikusudia kutumia kipengele cha vipindi vyote vya mabadiliko ya mwanamke (vya umri, mzunguko wa hedhi na pregnancy, ambavyo vinapelekea mood swings kueleza atlarge matumizi ya hisia kwa mwanamke sitakanusha.
Nina NB: ya kuwa moodswings sio gender-based thing. Wanaume wanapata moodswings SIO KWA VIPINDI MAALUMU , na hii inaeleza gape la nani anatawaliwa na hisia kuliko mwenzake.
Wanaume hutawaliwa na hisia kwenye mambo mengi tu, Kibayolojia kiwango cha testosterone hubadilika badilika na hiyo inapelekea athari katika hisia zao hence kuathiri ufanyaji wao wa maamuzi,
tofauti na sisi wao hujustify hisia zao kwa logic nimetumia neno kujustify kwa makusudi (Si tulikubaliana wanaume wanatuzidi maarifa na kutawala mazingira yao?) This is …
Kwangu mimi ili uniambie mwanaume hatawaliwi na hisia katika maamuzi ni mpaka uniambie maamuzi yake hayaleti madhara hasi , (irrationality)Back to reality je ni kweli maamuzi yao hayaleti madhara hasi individually na kwa jamii?
Tunaelezeaje, impulsive decisions
Mfano Tukiona mtu amelipukiana na mwenzie wakaanza kupigana, ametumia hisia au hajatumia hisia? Kwangu mimi asingetumia hisia pengine asingefikia kupigana,
Tunaelezeaje tabia ya kiume ya kutake risk zisizo za lazima.
Mfano kwa tabia ya umalaya , mtu anayefanya umalaya anatumia hisia hajatumia hisia? Kwangu mimi mtu mwenye agency ya kufunga zipu ndiye hatumii hisia, uhalisia ukoje?
Tunaelezeaje violence kama namna ya kucontrol/kusurvive, Kwa number wanaume wanaongoza kwa violence, msiniambia mtu ambaye hisia zake ziko stable ninini kinampelekea kufanya violence wakati angechagua amani?
Tunaelezeaje msongo wa mawazo? Simply ni hali ya mtu kushindwa kuzitawala hisia zake/ kuzidiwa na hisia zake… Kama msongo wa mawazo sio gender based problem, inaweza mkumba yeyote ninini kinafanya tuone mmoja yuko stable kihisia mwingine hayuko stable kihisia (Core ya mada)
Kwa maoni yangu jambo la kuzingatia ni kuwa: Ni nani anaathirika zaidi na sio huyu haathiriki kabisa.
Hii sikuiona, ngoja nizungumzie hapo kwa upande wa wanaume, huku nikilinganisha na wanawake.
Kwanza tukubaliane, point moja ya msingi kwenye hili jambo la hisia, kati ya wanawake na wanaume, kwangu mimi naiona tofauti yao kwenye timing na chanzo pekee.
Muda ambao individual anachukua kukaa na hisia fulani, zinazosababishwa either na mtizamo wa kiakili, au mabadiliko ya kimwili, hapa ndipo pa kuzingatia.
Suala la hisia kwenye maamuzi kwa upande wa wanaume, sio lazima zilete madhara hasi, sijui kwa nini umeamua kuiweka hivyo pekee, hisia kwa mwanaume zinaweza kuleta madhara chanya pia.
Mfano.
Mimi baba mwenye nyumba leo nikiwa nimefulia kwasababu ya kipato kidogo, kihisia nitayumba. Lakini baada ya hapo huo mkanganyiko wa kihisia nitautumia kubuni vyanzo vingine vya kuongeza kipato, hapo utaona madhara chanya ya kuyumba kwangu kihisia.
Mambo mengine uliyoelezea kwa mwanaume, mfano, impulsive decisions, taking risks, na violence, haya pia kwa upande wa pili hutokea hata kama sio kwa kiwango kikubwa kama itokeavyo kwa wanaume.
Tunaona watoto wa kike wanajilipua wanakamatwa na madawa ya kulevya, tunaona watoto wa kike uswahili kila siku wanakunja mashati kugombea mabwana, pia mnalipuka hata majumbani huko kugombeza kila apitaye mbele yenu mkiwa kwa siku zenu!.
Mind you, hawa wanaokunjana mashati, kujilipua kwenda nje ya nchi kudanga, pia yale mambo ya kibiolojia yaliyoorodheshwa mwanzo wa hii mada yanawahusu vilevile.
So, kimsingi utaona kabisa, mzigo wa madhara ya mabadiliko ya kihisia kwa upande wa mtoto wa kike ni mkubwa ukilingnisha na mwanaume.
Pia kwenye issue ya timing, kiuhalisia mwanamke anavurugika kihisia karibia kila mwezi, wakati mwingine anavurugika kihisia muda mrefu zaidi akiwa kwa pregancy period.
Lakini kwa mwanaume tuwe wakweli, huwezi kusema kuna mwanaume ambaye kila mwezi lazima a take risk, kila mwezi lazima alipukiane na mwenzie nk. If that could be the case, hii dunia isingekalika!.
Sipati picha kila mwezi wanaume wapigane kama nyie mnavyoingia period!
So bado tunaona, suala la madhara ya mabadiliko ya kihisia kwa upande wa mwanamke linachukua muda wake mwingi zaidi unaopelekea kuathiri utendaji wake ukilinganisha na mwanaume.
So all in all, ni kweli; wote wanawake na wanaume wana hisia, lakini kwa upande wa mwanaumke muda anaoishi akiwa kwenye mabadiliko ya kihisia ni mkubwa zaidi kulinganisha na mwanaume.
Pia, vyanzo vya mabadiliko ya kihisia, kwa uoande wa mwanamke ni vingi zaidi ukilinganisha na wanaume, so hawa hisia zao haziko sawa.