Nimekwenda DAWASCO Kimara, majibu nimepewa hadi nimemkumbuka mwenda zake

Nimekwenda DAWASCO Kimara, majibu nimepewa hadi nimemkumbuka mwenda zake

Ofisi za Umma zimeanza kurudi enzi za Kikwete aisee huduma mbovu majibu mabovu na wanajua huna pa kuwapeleka.
Dawasa Kimara kumbukeni mnafanya huduma jamani mtatuua 😂😂😂😂 yaani imefanya nimkumbuke marehemu Magufuli aisee may he continue rest in heaven sasa namwelewa japo too late
Nchi iendeshwe kimfumo siyo mtu mmoja binadamu tunapita mfumo utabaki mpaka mwisho wa dunia, endelea kumkumbuka ila alianzisha utaratibu mbaya wa yeye kuwa kila kitu, mf mawaziri na watendaji kumsifia kutoa hela za miradi wakati ni za watanzania wote
 
Ofisi za Umma zimeanza kurudi enzi za Kikwete aisee huduma mbovu majibu mabovu na wanajua huna pa kuwapeleka.
Dawasa Kimara kumbukeni mnafanya huduma jamani mtatuua 😂😂😂😂 yaani imefanya nimkumbuke marehemu Magufuli aisee may he continue rest in heaven sasa namwelewa japo too late
Hakukua na sababu ya kumtaja kikwete,ulipaswa kuzungumzia ulichokutana nacho.Wafanyakazi uliowakuta huenda hawakuwapo kikwete akiwa madarakani.Kuna uongozi mpya Muundo mpya.Yako mazuri mengi yalifanyika wakati wa kikwete na kikwete alishatoka madarakani miaka 6 iliyopita kama mambo yamekua mabaya ulaumu uongozi uliopo na sio kikwete ambaye mbele yake wameshakuja marais wawili.
 
Girlfriend wangu anafanya field hospitali moja kubwa ya rufaa hapa nchini. Kanambia wagonjwa wanakufa kizembe kisa mfumo wa GePG hapo hospitali unafeli mara kwa mara na hakuna anayefatilia kutatua tatizo likaisha. Wagonjwa wanalalamika na kuwafokea wahudumu maana yuko kitengo cha dawa. Kuna baadhi ya dawa haziko kwenye bima na kuna watu hawana bima hivo wananunua dawa. Bila mfumo wa malipo dawa hupewi wakati zipo. Tutakoma
 
mimi hawajapita kusoma mita na tarehe 26/6 nikaona mwezi unaisha hawajaja nikapigia simu waje wasome mita ili nilipe namehangaika kila siku unawaomba ndio leo wamekuja 30/6

Nadhani walibadili tarehe za kusoma mita
 
Ofisi za Umma zimeanza kurudi enzi za Kikwete aisee huduma mbovu majibu mabovu na wanajua huna pa kuwapeleka.
Dawasa Kimara kumbukeni mnafanya huduma jamani mtatuua 😂😂😂😂 yaani imefanya nimkumbuke marehemu Magufuli aisee may he continue rest in heaven sasa namwelewa japo too late
Unamkumbuka aliyekujibu ovyo?
Njoo pm nikupe namba ya WhatsApp ya DAWASA huyo mbwa ashughulikiwe kabla ya weekend.
Vile vile Kama unaweza kunipa jina au cheo tuzae naye leo leo
 
Unamkumbuka aliyekujibu ovyo?
Njoo pm nikupe namba ya WhatsApp ya DAWASA huyo mbwa ashughulikiwe kabla ya weekend.
Vile vile Kama unaweza kunipa jina au cheo tuzae naye leo leo
Uhuru wa kujieleza haufanyi kazi ofisi za umma mkuu???
 
Unakumbuka Magufuli !!!

Hakukuuwia nduguyo?
Hakumteka nduguyo?
Hakubomoa nyumba yako ama ya nduguyo?
Hakumfukuza kazi nduguyo kwa husuda?
Hakumpora nduguyo fedha zake?
Hakumweka ndani nduguyo kwa uonevu?
Hakumtukana nduguyo hadharani?

Huyu mtu siyo wa kumkumbuka hata kidogo.
Sawa Bwashee wewe ni wa Uru Kishimundu au Machame ?manake haya maandishi tunayajua wazee wa kanda yetu ya uchoyo,wizi na ufisadi kubebana,ukabila na malalamiko na chuki kwa kiongozi yoyote atakaye wanyima fursa za kuiba na kubebana. Bwashee mnazidi kujitengezea chuki na watu wengine, Magu yuko ndani ya mioyo ya watu hata iweje hamuwezi kumfuta.
 
Ofisi za Umma zimeanza kurudi enzi za Kikwete aisee huduma mbovu majibu mabovu na wanajua huna pa kuwapeleka.
Dawasa Kimara kumbukeni mnafanya huduma jamani mtatuua 😂😂😂😂 yaani imefanya nimkumbuke marehemu Magufuli aisee may he continue rest in heaven sasa namwelewa japo too late
Wewe ni mwongo, kuna ofisi haina boss? Ma DC,RC wanafanya nini?

Kabla ya hapo uliwahi peleka hata mmja kwa mwendazake au unaropoka tuu?
 
Unamkumbuka aliyekujibu ovyo?
Njoo pm nikupe namba ya WhatsApp ya DAWASA huyo mbwa ashughulikiwe kabla ya weekend.
Vile vile Kama unaweza kunipa jina au cheo tuzae naye leo leo
Dawasa kimara hii Ni mwezi wa Sasa watu wamefanyiwa survey na kufanya malipo na Risit zipo ila hawaji kuunga maji.

Kila siku wanasema vifaa hawajanunua. Wanashindwaje kununua vifaa wakati tumelipia hela?... Serikali sijui iko wapi. Mkuu wa Dawasa kimara hatumtaki. Kama waziri anasoma humu tunaomba amfukuze kazi mkuu wa Dawasa kimara Kuna michezo michaFu anaifanya.

Waziri aende pale atangaze mitaani watu ambao wamefanya malipo lakini hawajaunganishiwa maji. Kuna watu wana mpaka miezi 5 tangu walipe kuunganishiwa maji lakini hawajaunganishiwa. Wanataka uwape rushwa ndio Waje kukuungia.

Dawasa Kimara msidhani kila raia ni wapuuzi kaeni mkijua ukiona raia haongei kwa upuuzi mnaofanya msijione washindi. Mkiona Kobe kainama jua anatunga sheria.

Dawa yenu inakuja.
 
Tatizo sio mwendazake, tatizo ni lack of system or institution to keep these corrupt civil servants in check.
 
Upuuzi kwenye maofisi ya serikali hayajawahi kwisha hata wakati wa Magufuli hali iliendelea hivyo hivyo labda wajue una uhusiano na mkubwa au wewe mwenyewe ni mtu fulani acheni kutoa sifa za uongo
ingawa wakati wa mwendazake ulipungua kwakwel, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!
 
Back
Top Bottom