Nimekwenda DAWASCO Kimara, majibu nimepewa hadi nimemkumbuka mwenda zake

Nimekwenda DAWASCO Kimara, majibu nimepewa hadi nimemkumbuka mwenda zake

Kama unataka kumsifia dhalimu we msifie tu kwa namna yako, lakini hakuwa anaogopwa kihivyo. Kama angekuwa anaogopwa hivyo tusingeona watu kuchimba na kujiunganishia bomba la mafuta.

Na wale aliowapora hela kwenye Bureau de change wanamsifia kwenye post ipi?
Acha wivu.....
tutamkumbuka kwa mema
 
Ofisi za Umma zimeanza kurudi enzi za Kikwete aisee huduma mbovu majibu mabovu na wanajua huna pa kuwapeleka.
Dawasa Kimara kumbukeni mnafanya huduma jamani mtatuua [emoji23][emoji23] yaani imefanya nimkumbuke marehemu Magufuli aisee may he continue rest in heaven sasa namwelewa japo too late.
``Mtanikumbuka kwa mazuri na si kwa mabaya.....nimesacrifice maisha yangu kwaajili ya watanzania maskini''
 
Siku mfanyakazi wa Umma akinijibu vibaya mjiandae kuja kunitoa mahabusu. Washenzi sana tena sana. Kuna dada mmoja alinijibu huku anakula chakula nilichompa najua hatokaa anisahau kbs maishani mwake.
Hapa nani alikutoa mahabusu mkuu? Napita tuu
 
Nchi hii haikuwahi kushuhudia utovu wa nidhamu kuoneshwa na watumishi wa umma kama kipindi cha Magufuli, wananchi walikuwa wakidharirishwa hovyo wakiongozwa na yeye mwenyewe sana sana watumishi wadogo ndiyo walikuwa wakinyanyasika zaidi na kudharauliwa,kuonewa na kutishwa hovyo na Ma DC's na ma RC's labda mseme mlikuwa mnafurahishwa na unyanyasaji wa wananchi wakiwemo hao watumishi wa kada ya chini.
Umeelewa topic? au unapuyanga tu kisa unahasira na MAGUFULI?
 
Watumishi wa Umma wameteseka sana jamani waacheni wajinafasi.
Mmh. Ok. Labda hadi they bring their behaviour to your doorstep ndo utaelewa its not someone else problem but OUR problem kama tax payers.

'Statement ile:

First they came for the socialists, and I did not speak out—
Because I was not a socialist.

Then they came for the trade unionists, and I did not speak out—
Because I was not a trade unionist.

Then they came for the Jews, and I did not speak out—
Because I was not a Jew.

Then they came for me—and there was no one left to speak for me.
 
Ofisi za Umma zimeanza kurudi enzi za Kikwete aisee huduma mbovu majibu mabovu na wanajua huna pa kuwapeleka.
Dawasa Kimara kumbukeni mnafanya huduma jamani mtatuua 😂😂 yaani imefanya nimkumbuke marehemu Magufuli aisee may he continue rest in heaven sasa namwelewa japo too late.
Unakosea kidogo mkuu.

Ungemlaumu badala ya kumkumbuka kwa hayo yaliyokukuta huko.

Hakuweka mfumo wa kuyaondoa hayo, badala yake katumia vitisho.

Ni kama kidonda kilichokauka juu juu, kumbe ndani palikuwa panaendelea kuoza.

Imenibidi nitumie mfano huu kukurahisishia kuona maana halisi.
 
Hili la nyodo kwenye ofisi za umma awamu hii linakwenda kuwa baya hata kuliko wakati wa Kikwete. Huyu mama by nature hana haiba wala tabia ya ukali.
Siyo hayo tu uliyotaja, hana hata habari ya kurekebisha chochote bila ya ukali.

Mazuri sana yanaweza kufanyika bila ya kuburuzana kama alikokuwa akifanya Magufuli.

Taratibu za kazi maofisini zipo, na zinafahamika vizuri na wafanya kazi wenyewe, akiamua kuzisimamia taratibu hizo zifanye kazi kama inavyotakiwa, ni mfanya kazi gani ataacha kutimiza wajibu wake ipasavyo?
 
Ofisi za Umma zimeanza kurudi enzi za Kikwete aisee huduma mbovu majibu mabovu na wanajua huna pa kuwapeleka.
Dawasa Kimara kumbukeni mnafanya huduma jamani mtatuua 😂😂 yaani imefanya nimkumbuke marehemu Magufuli aisee may he continue rest in heaven sasa namwelewa japo too late.
Kwani wewe mkuu uliwaulizaje? Inawezekana umeanza kuwaulizia sawali lako kwa nyodo, lazima wakujibu kwa nyodo pia!
 
Unakumbuka Magufuli !!!

Hakukuuwia nduguyo?
Hakumteka nduguyo?
Hakubomoa nyumba yako ama ya nduguyo?
Hakumfukuza kazi nduguyo kwa husuda?
Hakumpora nduguyo fedha zake?
Hakumweka ndani nduguyo kwa uonevu?
Hakumtukana nduguyo hadharani?

Huyu mtu siyo wa kumkumbuka hata kidogo.
Hoja za kipuuzi kabisa, kumbe ndio maana mnaitwa nyumbu.
 
Dawasa kimara hii Ni mwezi wa Sasa watu wamefanyiwa survey na kufanya malipo na Risit zipo ila hawaji kuunga maji.

Kila siku wanasema vifaa hawajanunua. Wanashindwaje kununua vifaa wakati tumelipia hela?... Serikali sijui iko wapi. Mkuu wa Dawasa kimara hatumtaki. Kama waziri anasoma humu tunaomba amfukuze kazi mkuu wa Dawasa kimara Kuna michezo michaFu anaifanya.

Waziri aende pale atangaze mitaani watu ambao wamefanya malipo lakini hawajaunganishiwa maji. Kuna watu wana mpaka miezi 5 tangu walipe kuunganishiwa maji lakini hawajaunganishiwa. Wanataka uwape rushwa ndio Waje kukuungia.

Dawasa Kimara msidhani kila raia ni wapuuzi kaeni mkijua ukiona raia haongei kwa upuuzi mnaofanya msijione washindi. Mkiona Kobe kainama jua anatunga sheria.

Dawa yenu inakuja.
aisee nanusa harufu fulani ya kaugomvi
 
Kwani wewe mkuu uliwaulizaje? Inawezekana umeanza kuwaulizia sawali lako kwa nyodo, lazima wakujibu kwa nyodo pia!
Hili ndilo tunakosea watanzania. Kutoa huduma siyo kushindana na wateja kwa nyodo au dharau. Unapokuwa sehemu yoyote ya kutoa huduma unapaswa kuheshimu wateja wako wote. Na wateja wako wa aina nyingi na wenye tabia nyingi lakini hupaswi kuonyeshana nao umwamba. Miiko ya customer care inakataza.
 
Tatizo sio mwendazake, tatizo ni lack of system or institution to keep these corrupt civil servants in check.
Na mimi nakubaliana na wewe. Ila kujenga hizo system lazima uwe na kianzio. Na kianzio ni kuwa na kiongozi asiyependa uzembe. Magufuli kwenye hili eneo alikuwa hana simile lakini kosa lake ni kutokuweka system kama ulivyosema. Na kingine: watanzania tuna utamaduni wa uzembe na uvivu. Hili ni janga kuu na lipo kila mahali. Mtanzania hatimizi wajibu wake bila ya vitisho. Dawa ni waliye juu kuwa mkali, aweke system inayoeleweka ya kupokea na kushughulikia uzembe kama huu.
 
Hili la nyodo kwenye ofisi za umma awamu hii linakwenda kuwa baya hata kuliko wakati wa Kikwete. Huyu mama by nature hana haiba wala tabia ya ukali.
Dah....tumpe muda Mama banaa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2960]
 
Unakumbuka Magufuli !!!

Hakukuuwia nduguyo?
Hakumteka nduguyo?
Hakubomoa nyumba yako ama ya nduguyo?
Hakumfukuza kazi nduguyo kwa husuda?
Hakumpora nduguyo fedha zake?
Hakumweka ndani nduguyo kwa uonevu?
Hakumtukana nduguyo hadharani?

Huyu mtu siyo wa kumkumbuka hata kidogo.
Kwanini iwe Ndugu?..
 
Ofisi za Umma zimeanza kurudi enzi za Kikwete aisee huduma mbovu majibu mabovu na wanajua huna pa kuwapeleka.
Dawasa Kimara kumbukeni mnafanya huduma jamani mtatuua [emoji23][emoji23] yaani imefanya nimkumbuke marehemu Magufuli aisee may he continue rest in heaven sasa namwelewa japo too late.
Jiwe ndie aliekuwa anaenda kukulipia bili au? Acha upuuzi wako
 
Hili ndilo tunakosea watanzania. Kutoa huduma siyo kushindana na wateja kwa nyodo au dharau. Unapokuwa sehemu yoyote ya kutoa huduma unapaswa kuheshimu wateja wako wote. Na wateja wako wa aina nyingi na wenye tabia nyingi lakini hupaswi kuonyeshana nao umwamba. Miiko ya customer care inakataza.
Shida wengi hawaelewi 'Customer Service' you have to leave your attitude and mood swings at home. Ukishindwa basi wapishe wenye wito wa kazi hiyo ya kutoa huduma. Tatizo hawana ushindani ndio maana wanachukulia pouwa. Ingekuwa Private Sector wangeuona muziki.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Back
Top Bottom