Uchaguzi 2020 Nimelazimika kusafiri takriban kilometa 1000 kumzuia Robert Amsterdam na CHADEMA

Uchaguzi 2020 Nimelazimika kusafiri takriban kilometa 1000 kumzuia Robert Amsterdam na CHADEMA

Robert Amsterdam anaabishwa leo...watu wamejitokeza
 
Tanzania ni ya Watanzania hakika leo Robert na vibaraka wake wanafunzwa adabu
Uzalendo ni kuwabambikia kesi kesi kuwapiga risasi wapinzani uonevu unyanyasaji uovu mwingi? Uzalendo ni kuiba trilion 1.5 kisha kumtoa CAG kafara? Tanzania Nchi huru? Uhuru upi? Kuna uhuru Tanzania? Ingekuwa ni Nchi huru mtukufu angefanya ujinga huu wa kuzima Whatsapp tokea jana mpaka Leo ili aue watu Zanzibar na kuiba kura Tanganyika Dunia isijue mpaka NECCCM Tumeccm na Polisiccm wakimtangaza mshindi kwa njia haramu za kishetani
 
Robert hawezi kupandikiza mtu Tanzania,lazima tumfunze adabu
Ha ha haaa! Kwani Robert amefanya kosa gani? Yule ni wakili tuu kama mawakili wengine, anachofanya ni kutetea na kusimamia haki za mteja wake [emoji2375]
Sijawah kuona akilazimisha watu wamchague Lissu. Anachosisitiza ni uchaguzi huru na wenye haki, polisi kuacha upendeleo kwa CCM, kutoa nafasi sawa za wagombea kufanya kampeni bila kusumbuliwa.

Lakin tumeona waziwazi, magufuli amekuwa akisimama na kufanya kampeni maeneo ambayo hajapangiwa (na si tume wala polisi walimzuia) lakin Lissu akifanya hivyo inakuwa nongwa.

Nani ana uthibitisho kwamba lisu ametumwa na mabeberu? Tujuavyo sisi, Lissu alienda ubelgiji kutibiwa [emoji2375] sasa kutumwa hiyo vipi?

CCM ndio chama kinachoogopa sana siasa za haki, ndio maana hata sasa wanahangaika kuzima mitandao (huu ni ushahidi tosha kwamba hali ni tete mnoo kwa CCM)

Wanazima mitandao ili dunia isijue kinachoendelea, lakin hamuwezi kuzima camera za simu. Tutarekodi kila tukio ovu na tutatumia kama ushahidi dhidi ya hao ma policcm.

Hakuna mbabe anaekosa mbabe mwenzie, wako wapi kina Omar Bashir na genge lake?
 
Ndugu zangu,

Imenilazimu kusafiri kilometa takribani 1000 ili kumuonesha Robert Amsterdam kuwa hawezi kutupangia nani awe Rais wa Tanzania.

Ushindi upo ila tunataka uwe wa kishindo ili akome, apate fundisho yeye na mawakala wake.

Nimeahirisha kufanya biashara ya mamilioni ili kuilinda nchi yangu dhidi ya mabwanyenye.

Umuhimu wa kusafiri kupiga kura ya kizalendo ni kuepuka aibu kwa vizazi vijavyo watanilaumu wakisema "Babu na wenzio mlikuwa wapi hadi mkaruhusu Robert akapandikiza kiongozi?" hapana, sikubali lawama hii kamwe ndio maana nimesafiri kilometa zaidi ya 1000 kuwakomesha wanyonyaji hawa. Kamwe hatutaruhusu yale yaliyotokea mwaka 1884/5 kwenye mkutano wa Berlin yajirudie.

Tanzania ni nchi huru, tutachagua viongozi wetu wenyewe bila kupangiwa. Tanzania kwanza!
we safari poa sisi wa hapahapa tunamgoa magu mapema na huu utawala wake wa mabavu na wa kidikiteta na unyanyasaji ulio kidhiri dhidi ya watanzania, acha kuropoka yule ni wakili tu anafanya kazi yake kwa mujibu wa sheria kama hao wa ccm akina wankyo simon na albart msando
 
Sisi Watanzania asubuhi ya leo tumempigia kura Rais Magufuli kipenzi cha Watanzania, mpenda haki na amani,
Mchapakazi
Mvumilivu
Mnyenyekevu
Mzalendo

tumeshammaliza magu tayari kwenye box msaliti wa watanzania akijificha kwenye kinvuli cha wanyonge fisadi mkubwa
 
Kila mtu ana uhuru wa kumchagua kiongoz anayemtaka,Wagombea wote ni watanzania,Tundu lisu hajatumwa na mtu yeyote kuja kugombea ni uwanaharakat wake mashuhur kuona nchi haijakaa sawa ndio maana akaamua kugombea,hivyo bas Huyo Amstadarm ni Wakili tu kama wakili mwingine kwahiyo kutembea kwako km 1000 sio solution na usitake kutudanganya mtoa post
 
Sisi Watanzania asubuhi ya leo tumempigia kura Rais Magufuli kipenzi cha Watanzania, mpenda haki na amani,
Mchapakazi
Mvumilivu
Mnyenyekevu
Mzalendo
Amani iwe nanyi watu wa Mungu!

Kwa kipindi cha miaka 59 tangu uhuru, Tanzania imekuwa ikiongozwa na Chama cha mapinduzi. Katika miaka hii yote watanzania wamepitia mengi sana ila kila siku maisha ya watanzania yamezidi kuwa ya kuogofya na ya kusikitisha. Umasikini umekuwa donda kuu la watanzania na mbaya zaidi katika kipindi hicho chote, watanzania wamekuwa wakishuhudia wanasiasa wakizidi kujineemisha kwa pesa zao za kodi na mbaya zaidi wamekuwa wakiwafanya watanzania kuwa ombaomba na watumwa kwenye nchi yao.

Tofauti na miaka ya maraisi waliopita ambao pamoja na kujineemisha binafsi ila angalau walijitahidi kuheshimu utu wa mtanzania kwa kumuheshimu na kutomnyanyasa Ila katika kipindi cha miaka 5 watanzania wameshuhudia unyanyasaji mkubwa wa haki zao kutoka kwa watu waliojionesha kwao kuwa watu wazuri kumbe walikuwa chui waliojivika ngozi ya Kondoo!!

Mungu si Athumani alimuokoa mtoto wake Tundu Antiphas Lissu kwenye jaribio la mauaji hapo tarehe 7 mwezi wa 9 mwaka 2017 akiwa amepanga historia kuu iandikwe hapa Tanzania hapo tarehe 28/10/2020. Kwa hiyo ewe mtanzania usikose kuwa sehemu ya historia hii kuu inayoenda kuandikwa hapo tarehe 28/10/2020.

Kwa nini Tarehe 28/10/2020 ni siku ya watanzania kuandika Historia kuu juu ya nchi yao?

1. Kama wewe ni mzazi uliyemsomesha mtoto wako kwa shida hadi akamaliza chuo na hadi leo hajapata ajira, basi tarehe 28/10/2020 nenda kapige kura kuonesha kuwa CCM haistahili kabisa kuendelea kutawala nchi hii kwa sababu mfumo wao na sera zao umefanya mwanao akose ajira. Tarehe hiyo mchague Tundu Antiphas Lissu kuweka historia mpya Tanzania.

2. Kama wewe ni mtanzania uliyefanya kazi katika maisha yako ili uje kuishi vizuri, ila CCM wamefilisi mifuko ya pensheni na kufanya upate pensheni kidogo na kuishi kwa tabu, basi Tarehe 28/10/2020 nenda kaandike historia mpya kwa kuiadhibu CCM na kumchagua Tundu Antiphas Lissu

3. Kama wewe ni kijana uliyesoma kwa shida huku ukiingia mkataba na serikali wa kukukata asilimia 6 mpaka 7 ya mshahara ukipata ajira, ila CCM ya awamu ya tano imekufanya ukatwe asilimia 15 basi nenda kaandike historia tarehe 28/10/2020 kwa kuikataa na kuiadhibu CCM na kumchagua Tundu Antiphas Lissu.

4. Kama Wewe ni Mtanzania ambaye gharama za matibabu zimekuwa kubwa na umekuwa ukipata shida ya gharama za matibabu kwa miaka yote basi tarehe 28/10/2020 nenda kaiadhibu CCM kwa kuinyima kura na uandike historia kwa kumchagua Tundu Antiphas Lissu!

5. Kama Wewe ni mfanyakazi ambaye kwa miaka 5 hukupata haki yako ya kuongezwa mshahara na mwaka huu umeona bima ya afya ikiondoa baadhi ya dawa kwenye mfumo wa bima huku gharama ya maisha ikizidi kupanda basi kaandike historia kuu tarehe 28/10/2020 kwa kuinyima kura CCM na kumchagua Tundu Antiphas Lissu

6. Kama wewe ni mzazi uliyepata shida kumsomesha mtoto wako private na amefika chuo amenyimwa mkopo kwa kusomeshwa private elimu ya chini basi tarehe 28/10/2020 kaandike historia Kuu kwa kuwanyima kura CCM na kumchagua Tundu Antiphas Lissu

7. Kama wewe ulikuwa mfanyakazi uliyeajiliwa sehemu ila Sera za Awamu ya tano ya CCM zikafanya upoteze ajira yako kwa kampuni kufirisika basi tarehe 28/10/2020 kaandike historia kuu kwa kuwanyima kura CCM na kumchagua Tundu Antiphas Lissu

8. Kama wewe ni mfanyabiashara uliyeangaika kupata mtaji ikiwemo kukopa, ila kodi za tra na mnyanyaso ya tra yamekufanya ufunge biashara au ufirisike basi tarehe 28/10/2020 Kawe sehemu ya historia kuu kwa kuwanyima kura CCM na kumchagua Tundu Antiphas Lissu

9. Kama Wewe ni mkulima uliyekuwa ukiuza mazao yako vizuri bila shida ila sera za Chama cha mapinduzi zikakupiga marufuku kuuza mazao nje na kupelekea ukafirisika na kupata hasara basi Kawe sehemu ya historia kuu hapo tarehe 28/10/2020 kwa kuwanyima kura CCM na kumpa kura Tundu Antiphas Lissu.

10. Kama wewe ni kijana ambayo umekuwa ukihangaika bila ajira kwa sababu ya sera mbovu za kiuchumi za Chama cha mapinduzi basi tarehe 28/10/2020 kaandike historia kuu katika nchi yetu kwa kuwanyima kura CCM na kumchagua Tundu Antiphas Lissu.

Ewe mtanzania, kumbuka sehemu pekee ya wewe kueleza hisia zako juu ya mwanasiasa yeyote au Sera zozote zinazokuathili kimaisha na kiuchumi ni kwenye Sanduku la Kura. Hivyo Tarehe 28/10/2020 nenda Kawe sehemu ya Historia kuu inayoenda kuandikwa ya kuweka utawala mpya hapa Tanzania kwa maslahi mapana ya nchi yetu na watu wake

Ukipiga kura, usiache kulinda kura maana kura yako ina thamani sana

Share na mwenzako!
 
Mleta mada kwani wewe nani?

Unawezaje kumzuia huyu mzungu kuchukua hatua za kisheria?

Unaweza kuwalipa wanasheria mahiri kama yeye kumpinga?

Kama unaweza hayo hapo juu wewe ni kidume, lakini kama unaleta blah-blah kafie jalalani!
Ushasema Mzungu, hv unadhani hatua anazotaka kuchukua zina maslahi kwako!? Wewe kalagabaho, mwenzio Lisu keshapiga deal na washkaji! Mkimpa Nchi tunarejeshwa kwenye zama tulizozikataa.

Ukimsikiliza vzr Lisu utagundua kwamba hapendezwi kabisa na suala la Nchi yetu kujitegemea!! Yeye kwake bakuli ndo mpango mzima.

Hana tofauti na Membe anayesema yeye akipewa Nchi kazi yake ni moja tu kwenda Nchi za nje kuomba misaada ili mapesa yamwagike nchini. Hzi ni ideology za ajabu sana!!! #JMP TANO TENA!!
 
KAMA Amsterdamu kula yake ya kimaisha ni kuona damu za watu zinamwagika, Basi wale wanaomuunga mkono lazima tuwaepuke kama ukoma!
Kazi yake ni kuwashitaki wote wanaosababisha umwagikaji wa damu za watu wasio na hatia. Usimwogope. Huyu ni rafiki. Ogopa kama ukoma wale wanaomwaga damu za watu kwa risasi. Tundu Lissu alipigwa risasi, Shehe Ponda alipigwa risasi n.k. Waliotenda hayo tuwaogope kama ukoma na tukiwajua hiyo kazi tumpatie Amsterdam awapeleke kotini kule the Hague.
 
Kila mtu ana uhuru wa kumchagua kiongoz anayemtaka,Wagombea wote ni watanzania,Tundu lisu hajatumwa na mtu yeyote kuja kugombea ni uwanaharakat wake mashuhur kuona nchi haijakaa sawa ndio maana akaamua kugombea,hivyo bas Huyo Amstadarm ni Wakili tu kama wakili mwingine kwahiyo kutembea kwako km 1000 sio solution na usitake kutudanganya mtoa post
Amstadarm ni wakili tu,Tundu Lisu ndio mgombea
 
Sisi Watanzania asubuhi ya leo tumempigia kura Rais Magufuli kipenzi cha Watanzania, mpenda haki na amani,
Mchapakazi
Mvumilivu
Mnyenyekevu
Mzalendo
Mkatili,
mbabe,
mjeuri,
asiyejali watu,
dikteta,
muuaji
na kila sifa mbaya.
Kwa miaka mitano tumeshuhudia haya kwa Magufuli. Leo tusumpe kura kabisa. Wapo waliofaidi utawala wake lakini wengi wamepigika. Haya shime wananchi.
 
Kataa ushoga Tanzania, kataa kibaraka wa Mabeberu kutoka ubeligiji

Piga kura kwa Rais Magufuli kipenzi cha Watanzania
Mkatili,
mbabe,
mjeuri,
asiyejali watu,
dikteta,
muuaji
na kila sifa mbaya.
Kwa miaka mitano tumeshuhudia haya kwa Magufuli. Leo tusumpe kura kabisa. Wapo waliofaidi utawala wake lakini wengi wamepigika. Haya shime wananchi.
 
Sisi Watanzania asubuhi ya leo tumempigia kura Rais Magufuli kipenzi cha Watanzania, mpenda haki na amani,
Mchapakazi
Mvumilivu
Mnyenyekevu
Mzalendo
mnaynyasaji,mdhulumaji,mbinafsi muu-aji mzee wa visasi, tayari tumesha mchinjilia mbali,anategemea huruma za tume
 
Back
Top Bottom