Nimeletewa Kesi: Mke wangu anatoka kimapenzi na Mume wa Mtu

Nimeletewa Kesi: Mke wangu anatoka kimapenzi na Mume wa Mtu

Ukishindwa kuyamaliza na mke wako au mme wako. Basi bora muachane.

Kutegemea ushauri kwa mambo ya mtu kaliwa huko huo ni ujinga mnajitangaza na kuchafuana.

Tukae tuzungumze kama unakubali na kuomba msamaha sawa. Na mimi itategemea nakusamehe au lah. Hayo ndiyo maamuzi kwa mwanaume anayejielewa..

Huko kwenye ushauri mtaambiwa msamehehane tu ni mambo ya ndoa unadhani watakwambia muachane?
Una manisha hili jukwaa lifutwe kama hutaki tujadiri masuala ya ndoa
 
What? Jamani kuweni serious na mpeni mwenzenu ushauri bora na sio utani, mambo mengine kama haya hayafai kufanyia dhihaka.
Mwenzetu?
Hayo ndio maoni yangu baada ya kusoma bandiko lake wala sio utani, kama unaona nimefanya dhihaka na unajua kipi sahihi anapaswa kufanya msaidie kwa kuyaandika hapa.
 
Mwenzetu?
Hayo ndio maoni yangu baada ya kusoma bandiko lake wala sio utani, kama unaona nimefanya dhihaka na unajua kipi sahihi anapaswa kufanya msaidie kwa kuyaandika hapa.
Ok sawa kama hayo ndio maoni yako ya kimaisha juu ya issue kama hii basi sawa, sina sababu ya kupingana nawe, ila kwa upande wangu nilihisi kuwa hukuwa serious!
 
Ndugu zangu wana jamiiforums habari za asubuhi hii ? kwangu mimi ni mzima wa afya na nipo sawa kabisa

Sina cha kupoteza Kama mnavyoona hapo juu kwenye bandiko.

Jana jioni mida ya saa moja nikiwa kazini kwangu kuna dada ninayemfahamu kwa sura tunaishi mtaa mmoja alikuja kazini kwangu, hapo kazini kulikua na watu kadhaa wakipata huduma,

Baada ya watu wote kuondoka alinifata huyo dada akanieleza kwa uchungu mkubwa kuwa "mke wako anatembea na mme wangu mwambie mkeo aachane na mme wangu" maneno hayo aliyatamka kwa kuyarudiarudia na mpaka machozi yakamtoka

Kuna watu wakatokea pale kupata huduma yule dada akaondoka sikupata nafasi ya kuzungumza nae kiundani ili kujua mke wangu alitembea na mme wake lini, na nimeshindwa kuchukua hatua yoyote mpaka sasa nashindwa nianzie wapi, inavyoonekana mpaka dada huyu kulia kwa uchungu mbele yangu itakuwa kweli mke wangu anatoka kweli na mmewake

Ndugu zangu hili suala ni zito kweli kwangu nianzie wapi, majibu sina. Nimeamua kulileta hapa mimi kijana mwenzenu mnipe mawazo nifanye nini nimetuliza akili yangu sijakurupuka ila hatua ya kwanza nimeona nililete hapa.


Asanteni
Yuda_exalioth
Jamiiforums_Geita
Usipaniki, usikurupuke, kuwa mpole, tenda kwa akili yaani fikiri vizuri sana kabla ya kutenda lolote.
 
Back
Top Bottom