antimatter
JF-Expert Member
- Feb 26, 2017
- 47,274
- 126,778
Duh,Wakuu,
Hivi inakuwaje kila mara hawa viongozi wa serikali wakitaka kuchonga sanamu la baba wa taifa huwa wanakosea?
Kuna hili sanamu jipya la Mwalimu Nyerere huko nchini Cuba kiukweli imenishangaza sana kuona Waziri Ndumbaro amelipitisha na kuona kuwa linafaa.
Soma pia: Sanamu ya Abraham Lincoln Washington DC na Sanamu ya Julius Nyerere Dodoma
Au huwa kuna hela zinabanwa then tenda ya kuchonga ya sanamu wanapewa wasanii uchwara?
Hili sanamu halina tofauti sana na lile la Kigwangala. Ndumbaro jitafakari!
Hapo walichopatia ni jina pekee. Hiyo sanamu ni bandia, labda ni ya ndugu yao!!
CHAWA Tlaatlaah & co, tukiwambia ccm imechoka mno muwe mnaelewa