Clark boots
JF-Expert Member
- Jun 5, 2017
- 6,770
- 6,202
Mkuu, njoo Mlowo hapa tumuombee mama yetu..
Apumzike kwa Amani
Apumzike kwa Amani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sawa nashukuruM
wewe unatabia za kikekike mwanaume unalia na kulalamika,wewe kweli ni lucy
Kwa hakika nitamkumbuka sana huyu mama.alikuwa kipenzi cha wana Mbozi.Kama Mlowo ndio tutaendelea kumkumbuka zaidi. Alishiriki kwenye shughuli nyingi sana .Mkuu, njoo Mlowo hapa tumuombee mama yetu..
Apumzike kwa Amani
Picha ikowap..wengine hatumjui
Ni kwasababu shetani kakutawala na kujazwa roho ya kishetani.Sijui kwa nini sijahuzunika hata kidogo
Daah !Yaani we jamaa hili jambo la msiba lakini unatufanya tucheke ili tuonekane wabaya sababu ya uandishi wako.
Pumzika kwa Amani Dada Ester
Duh 🙄 !Ni kafara za CXM kwa ajili ya uchaguzi baadaye mwaka huu, wengi wataondoka.
Sasa hivi yuko kwa babu yake anachanjwa chale hadi makalioni na amelala kwenye ngozi ya fisi ili kulilia mizimu imsaidie kupata hiyo nafasiLuca anawinda nafasi iliyoachwa wazi na marehemu.
Amepiga kazi sana MboziNdugu zangu Watanzania,
Kwa hakika nimeumia sana, nimehuzinika sana,nimesikitika sana,nimelia sana na bado moyo wangu unabubujikwa na machozi ya huzuni na uchungu mkubwa sana kwa Kifo cha Mkuu wangu wa wilaya ya Mbozi Mheshimiwa Esther Mahawe ambaye ametangulia mbele za haki.
Soma TANZIA - Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe, Esther Mahawe afariki Dunia
Huyu Mama aliipenda sana Mbozi,aliwapenda sana wana mbozi ,aliipenda kazi yake ,aliijali kazi yake,aliithamini kazi yake, alijua majukumu yake, alitimiza vyema majukumu yake, aligusa Maisha ya wengi, alichangamana na wengi, alizungumza na wengi, alikuwa kipenzi cha wana mbozi.
Alikuwa kimbilio la vijana, alikuwa mwana michezo, alikuwa faraja kwa wanamichezo, alipendwa na wengi, hakuwa na Makuu Mama wa watu, alifikika wakati wote, alishirikiana vyema na wanambozi, alikuwa msikivu, alikuwa muungwanahakuwa na kiburihakuwa na dharauhakuwa majivuno, cheo kwake kilikuwa ni dhamana, cheo kwake ilikuwa ni utumishi kwa watu.
Mbona imekuwa mapema hivi kwa huyu mama? Mbona naandika huku nikiisikia sauti yake ikinijia kwa sababu nilikuwa nikimsikiliza mara nyingi kwenye mikutano yake na sisi wananchi wa Mbozi. Sasa Esther Mahawe Kalala Usingizi wa Milele? 😭😭😭. Si angetupa nafasi ya kutupatia neno la Mwisho wana mbozi?
Si angetuambia tukamuone hospitalini na atupatie mkono wa kwa heri? Si angetuita wana Mbozi hospitalini alipolazwa ili tuzungumze naye? Kwanini ametuachia majonzi kiasi hiki wana Mbozi? Nani wa kutafuta machozi wana Mbozi? Kwamba Mheshimiwa Esther Mahawe hatutamuona tena?
Inaumiza sana tena sana,nalia mimi, nalia sana, nalia kwasababu ya mkuu wangu wa wilaya,nalia kwasababu ya huyu mama aliyekuwa na moyo wa upendo, ukarimu, unyenyekevu, utu, uungwana na moyo wa kujitoa na kujitolea kwa watu. Amesaidia wengi na amegusa maisha ya wengi. Ameacha alama kwa wana Mbozi.
Esther Mahawe Mkuu wetu wa wilaya ya Mbozi Pumzika kwa Amani Mama. Lala salama Mama, Mwanga wa Milele ukuangazie Mama yetu.
Umepigana Vita iliyo njema, Mwendo Umeumaliza na Imani Umeilinda.
Tangulia Mama yetu. Duniani sote ni wapitaji tu. Tutaonana Mama.View attachment 3201850
Embu acha utani wakati watu tupo kwenye majonzi mazito sana.Mwacheni Luca abubujikwe kwa raha zake.
Amefanya kazi kubwa sana huyu Mama.Amepiga kazi sana Mbozi
Mimi siyo kama wewe mwenye mawazo ya kushirikiana na ushirikina. Ninaomboleza Kifo cha Mkuu wangu wa wilaya kwa huzuni na uchungu mkubwa sanaSasa hivi yuko kwa babu yake anachanjwa chale hadi makalioni na amelala kwenye ngozi ya fisi ili kulilia mizimu imsaidie kupata hiyo nafasi
Acha mzaha kwenye majonzi.Luca anawinda nafasi iliyoachwa wazi na marehemu.
Sitafuti uteuzi mimi.Uteuzi nje nje mkuu usilie
Mungu akusamehe sana maana hujui utendaloKwaninavyo wachukia CCM kwa kusababisha mauaji ya wengine hata ukifa wewe kwa wapenda haki ni sherehe duniani na mbinguni.
Mimi siyo chawa ndugu yangu mtanzania uliyejaa chuki binafsiDogo acha uchawa na kujipendekeza hadi misibani