Nimelima ekari tano za mihogo, itakuwa tayari kwa mavuno mwezi wa Ramadhani

Kuanzia nov mpaka sasa maeneo ya mkoa wa pwani akukua na mvua ya maana,kama umelima maeneo hayo tegemea kupata mhogo mzuri na utapiga hela ya kutosha
 
Chukua hiyo million 3, .... ili kuepuka usumbufu ujao.
 
Ukanda wa Pwani kutoka Gombero,Pangani Bagamoyo mpaka Lindi na Mtwara mihogo inastawi sana na ladha ya mihogo yake ni mitamu sana.
Gombero hapo nimepaelewa sijafika ila wanasema ni poa sana mim nimefika Kwediboma and vitongoji vya jirani nimeona watu wakilima sana ila vile soko haieleweki sana mpaka mihogo vinakomaa sana shambani
 
Are you serious au michezo tuu?
 
Are you serious au michezo tuu?
Mkuu, mimi ni mtoto wa mkulima na nimeshuhudia Bi mkubwa alivyokuwa akigombana na wateja wake aliokua akiwauzia mbaazi mbichi, kunde, choroko, kisamvu n.k.

Alikuwa anawachumia mwenyewe kama asipokuwepo mteja ataniambia nimchumie mimi,

wengine wanajua kabisa wakiwa kwenye siku zao hawaruhusiwi kuingia shambani kuchuma chochote hivyo huwa wanakuja na mtoto siku ambazo wanajua bi mkubwa hayupo, maana mimi huwa nilikuwa sipendi ile harufu inayobaki kwenye mikono

Kiufupi kama una shamba au hata kwako kama umelima mboga mboga siku mwambie mkeo achume akiwa kwenye siku zake, kitakachotokea mimea yote ambayo itakuwa imechumwa haitastawi ili uendelee kuchuma bali itaanza kupata ugonjwa usioeleweka kisha itakauka itakayobaki ni ile ambayo haikuchumwa, sasa hiyo iliyobaki chuma wewe au mkeo akiwa ameshamaliza mzunguko wake mwambie achume kisha leta ushuhuda hapa

Maana mimi mwanzo bi mkubwa alipokuwa akigombana na wateja wake nilikuwa simwelewi ila kuna siku nilimuuliza ndo akanifungukia
 
Nimeandaa kikapu
👏🏽👏🏽akili mingimingi
 
Aiseee,
 
Mihogo mbegu ya wapi hiiinachukua miezi mitano hadi kuvunwa?
 
Mi naomba unialike nije "kula Kisamvu"....Pia naweka order ya mihogo, gunia moja kubwa, ikishakuwa tayari.
 
Ramadhani ndio mwisho mwisho, vipi mrejesho wa biashara ya muhogo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…