Leo nimeingia kwenye kioski kimoja hapa mtaani kwetu, nikiwa na lengo la kununua bidhaa. Tatizo nilikuwa sina pesa taslimu (cash), nikamwambia muuzaji hivyo. Akanijibu kwa utulivu, "Usiwaze, unaweza kulipa kwa simu."
Nilifurahi sana kwa sababu nilikuwa nahitaji hiyo bidhaa kwa dharura. Nikatoa simu, nikapiga malipo chap chap. Bidhaa yenyewe ina bei ya elfu tatu tu (3,000). Lakini kwa bahati mbaya au uzembe wangu, nimetuma elfu kumi (10,000).
HESABU NILIZOTEGEMEA:
· Nimetuma: 10,000
· Bei ya bidhaa: 3,000
· Chenji inayotakiwa: 7,000
Sasa hio huduma ya lipa Kwa simu nini maana yake?