mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,864
- 10,483
Mara baada ya kurudishwa tena mfumo wa vyama vingi hapa nchini, ilichokifanya ni kuendesha "looting" ya mali zilizotokana na nguvu za wananchi kote nchini. Pasipo kuwa na aibu walijitwalia nyumba na majengo, viwanja vilivyopimwa na hata vya wazi, viwanja vya michezo, miradi ya ufugaji huku wakitambua vyema ni kinyume kabisa na kanuni na taratibu, na ukweli ni ya kuwa vilipaswa kukabidhiwa ktk halmashauri za miji husika.
Ebu makada waje na uthibitisho, kuwa ni ruzuku ipi ya CCM imewahi kuhusika kujipatia mali hizo? Kihistoria chama hiki kikiwa ktk hatua za "nascent stage" ya kujijenga kwake kiliweza kununua mali zipi zaidi ya kubebwa na dola na hata kupora tu mali za umma. Malezi ya awali ya mtoto huathiri kwa kiasi kikubwa tabia za maisha ya ukubwani kwake, ndivyo hasa CCM inavyoathirika kwa nyakati za sasa.
Wazazi wake TANU na ASP pasipo kujua yupi alikuwa ndiye baba ama mama yake, toto hili CCM lilizaliwa familia ya wakora na kudekezwa sana kupitia dola. Kwa hiyo hata walipotokea wadogo zake, bado limeendekeza na tabia za kudeka na hata kujimilikisha kila kitu ambacho wazazi wake waliuibia umma wa Watanzania.