Nimelizwa, nimeumizwa na kufadhaishwa mno na kifo cha kijana huyu

Nimelizwa, nimeumizwa na kufadhaishwa mno na kifo cha kijana huyu

Hawana ukazi wa kindaki ndaki chochote, hawa ni wakimbizi waliokimbia utawala wa kimabavu na kibaguzi wa kihutu mnamo miaka ya 60 hadi 70.
Kumbuka miaka hiyo wapo watutsi waliokimbilia Congo, Tanzania, Burundi, Uganda, Kenya na kwengineko. Waliokimbilia Tanzania na Uganda ndio wale kina Kagame waliorudi kupigania nchi yao mwaka 1994, ila wale waliokimbilia Congo wengi hawakurudi, bali waliomba vibali vya ukazi kwa kutaka waunganishwe kuwa sehem ya raia wa Congo. Serikali ikawakubalia na kuwa wakazi rasmi wa Congo bila serikali hiyo kujua kitachotokea baadae.
Sasa leo ndio wanaotumiwa na nchi fulan kuiba rasilimali za Congo na kuzipeleka huko kwa waliowatuma.
Haya mambo ni mazito, kwa mtu mwenye mtazamo kama wako hawezi kuyajua. Mimi nimekwambia hadi umoja wa mataifa unajua afu ww unasema sio kweli, sasa nakuwekea kipande cha taarifa hapo chini afu uniambie kama kweli umoja wa mataifa huo haujui kinachoendelea. Kati ya umoja wa mataifa na wewe au mimi nani anaeijua zaidi dunia na yale yanayoendelea huko kongo na kwengineko duniani?
Sisi tunaongea vitu vyenye fact kwa vile 85% hadi 90% ya nchi za Afrika na makabila yake tunaifahamu vizuri tu.
Sijui ni kitu gani kinachofanya hao UN wasimshuhhulikie Kagame, kama ushahidi wanao sasa shida iko wapi?

Inasikitisha sana kuona wacongo sio watu wa kukaa kwa amani ndani ya nchi yao kwasababu ya majirani wabinafsi wanaowaza kuiba mali za Congo, bora waibe bila kuua raia wasio na hatia.
 
Sijui ni kitu gani kinachofanya hao UN wasimshuhhulikie Kagame, kama ushahidi wanao sasa shida iko wapi?

Inasikitisha sana kuona wacongo sio watu wa kukaa kwa amani ndani ya nchi yao kwasababu ya majirani wabinafsi wanaowaza kuiba mali za Congo, bora waibe bila kuua raia wasio na hatia.
Mkuu denooJ kwa Congo ni vigumu sana umoja wa mataifa kuleta amani ya kudumu au kuyamaliza kabisa makundi ya waasi kama tunavyofikiria. Na sababu kuu ni hizo nimeziandika chini 👇
Kinachoiponza kongo ni rasilimali zake. Pale kila taifa kubwa linachaka lake la kuchimba madini na rasilimali mbalimbali.
Mfano Marekani wanachaka la dhahiri kupitia mikataba ya serikali na la siri kupitia vikundi kama hivi vya M23, Halikadhalika Wingereza, Ufaransa, Belgium na wengineo.

Solution ni serikali kuwatafutia raia wote wanaoishi maeneo yenye rasilimali na madini maeneo mengine ya mijini kama vile Kinshasa, Lubumbashi nk. Afu hayo maeneo waachie hao wanaochimba wachimbe na kuipatia serikali kiasi chochote watachoona hao wakubwa kinawafaa. Bila hivyo wataendelea kufa miaka kwa miaka.
Na pia hapo chini 👇
Hilo haliwezekani na lisingewezekana.
Congo ilipata uhuru wake huku wazungu wakiwa wameshajigawia maeneo yao ya kuchimba madini, gesi asilia nk.
Ndio maana tangu mwanzo wa uhuru, mpigania uhuru wa nchi hiyo na waziri mkuu wa kwanza mweusi hayati Patrick Lumumba alipotaka kutengeneza udhibiti wa rasilimali hizo aliuwawa kifo cha kutisha, tena aliuliwa na jeshi la nchi yake mwenyew ambayo aliipigania hadi uhuru.
Jeshi hilo lililoongozwa na Mobutu halikutaka kujali au kujua ni jinsi gani Lumumba alikuwa tayari kuweka maisha yake hatarini kwa ajili yao na nchi yao.
Walichofanya ni kumuuwa ili wazungu waendelee kuchota bila bughuza yoyote.
Kabila baba alipoingia nae alitaka kuleta za Lumumba matokeo yake akauwawa kiwepesi wepesi na mlinzi wake mwenyewe.
Toka wakati huo ikaamulika kama mbwai na iwe mbwai, watu waibe na nchi isitawalike maeneo fulani, ili iwe ngumu kuwadhibiti wanaotorosha madini yao.
 
Tuvumilie yote ndugu zangu watanzania,vita si nzuri kabisa
Vita haifai mkuu, tumeona nchi kama Libya, Syria, Iraq na kwengineko ambapo hapo mwanzo nchi hizo zilikuwa na amani na usalama mzuri, lkn leo wengi wameuwawa, wameteswa, wametekwa, wamebakwa, wamevunjiwa nyumban zao na kulazimishwa kukimbilia katika nchi za wenzao.
 
Vita haifai mkuu, tumeona nchi kama Libya, Syria, Iraq na kwengineko ambapo hapo mwanzo nchi hizo zilikuwa na amani na usalama mzuri, lkn leo wengi wameuwawa, wameteswa, wametekwa, wamebakwa, wamevunjiwa nyumban zao na kulazimishwa kukimbilia katika nchi za wenzao.
More than danger
 
Habari zenu wana JF wenzangu, ama baada ya salam ningependa sasa nijielekeze kwenye mada husika.

Kabla ya yote, ningependa niweke wazi kuhusu jinsi nilivyofahamiana na huyu kijana kupitia uncle wake ambae niliwahi kufanya nae kazi katika kampuni fulan, miaka kadhaa iliyopita.

Kijana ninaemzungumzia hapa anaitwa Jems, na huyo mjomba wake ambae alikuwa rafiki yang alikuwa anaitwa Ramadhan. Ilikuaje hadi kufariki kwake, naomba unifuatilie hapo chini.

Jems ni kijana aliezaliwa mwaka 1997, katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Alikuwa mtoto wa kwanza katika familia ya watoto wa tatu, ambapo waliomfuata kwa kuzaliwa alikuwa mwanaume pia alieitwa Janvier (January) na wa mwisho mwanamk alieitwa Julieta.

Mwaka 2011, waasi wa M23 walivamia kijiji chao na kuuwa makumi ya wanavijiji. Hali hiyo ilipelekea Jems, ndugu zake na wazazi wake watoroke kwao ili kwenda kutafuta hifadhi sehem nyingine. Kwa vile ilikuwa usiku, basi Jems akapoteana na wazazi wake pamoja na ndugu zake.

Jems akakimbilia katika kambi ya ndan nje ya kijiji chao, ambapo alikutana na huyu rafiki yang alieitwa Ramadhan ambae alikuwa amekwenda kwao kutembea na kukutana na mkasa huo siku chache baada ya kufika.

Huyu rama hakuwa na undugu na Jems, lkn alijikuta anaguswa na yaliomkuta huyo dogo ambae tayari alikuwa ashapoteana na wazazi wake.

Baada ya kukaa kambini kwa muda, waliamua kukimbilia Tanzania kambini mkoani Kigoma ambapo walikaa kwa muda wa miaka miwili na nusu.

Mwaka 2014, Rama na dogo Jems wakaanza safari ya kuja Kaburu kutafuta hifadhi ya uhakika. Ikumbukwe Rama tayari alikuwa ni mkazi wa huku, ila alikwenda kwao kusalimia na kuona familia yake. So njia za kufika Kaburu alikuwa anazijua na pesa kidogo alikuwa nayo, ingawa nyingine pamoja na vitu aliviacha baada ya uvamizi ule wa ghafla wa waasi.

Baada ya kujikongoja na kijana wake huyo waliejuana nae njiani, mwaka 2015 wakafanikiwa kuingia Kaburu.

Baada ya kufika rama alianza kazi kama kawaida, ila Jems kwa vile alikuwa mgeni ilibidi aanze kwanza kukaa nyumban mpaka pale vibali vyake vya ukimbizi vitakavyokuwa tayari.

Baada ya vibali kuwa tayari Rama alimuuliza Jems kuwa anataka asome au afanye kazi, Jems akachagua kusoma. Basi Rama akafanya makeke dogo akafanikiwa kupata shule.

Baadae dogo akawa anasoma huku anajifunza kazi nyingine ya mkono (kunyoa)

Muda wote dogo hakuwa na amani moyoni mwake, maana hakuwa anafahamu mustakabali wa wazazi wake kwamba wamefariki au wako hai somewhere.

Mwaka 2019, akabahatika kupata mawasiliana na familia yake, kumbe inasemekana wazazi walikimbilia Uganda na baadae wakarudi, ila mdogo wake wa kumfuata Janvier alikuwa ameuwawa katika uvamizi mungine uliofanywa muda mfupi na waasi baada ya wazazi wake hao kurejea nyumbani toka ukimbizini Uganda.

Dogo alilia kwa uchungu mkubwa, ila sisi kama wajomba zake tulikuwa na kazi ya kumtuliza na kumliwaza.
Rama alimpenda, alimthamini na kumjali huyu dogo kama vile mtu anavyomjali mtoto wake au ndugu yake wa damu.

Hakuwahi kumbagua kwa lolote, na hata dogo Jems na yeye alipoanza kuongea na wazazi wake aliwambia kuhusu ambae alikutana nae njiani na kuamua kumsaidia kama mtoto wake au mtoto wa ndugu yake, kiasi kwamb wazazi waliguswa na msaada ule wa Rama na kuahidi siku atakayokwenda tena Congo kutembea watamwalika kwao na kumfanyia sherehe kubwa kama vile ndugu yao.

Mambo yalibadilika mwaka 2021, baada ya Rama kupatwa na maambukizi ya korona ambapo alifariki muda mfupi tu baada ya kufikishwa hospital. Kilio kile kilikuwa cha wote, lkn kilimuumiza zaidi Jems ambae kwake yeye Rama alikuwa ni sawa na mzazi wa kumzaa.

Baada ya kilio kuisha huku tukiendelea kumueleza kwamba ile ni kazi ya Mungu na kamwe huwa haina makosa. Basi ikabidi akubaliane na matokeo kwamba kweli Mungu amechukua kilicho chake. Dogo akakonda na kupoteza nguvu za mwili kutokana na kuwaza sana juu ya kifo cha uncle wake Rama.

Hajakaa sawa, mwaka huu miezi ya mwanzo akapokea tena taarifa kuwa wazazi wake wote wawili pamoja na dada yake waliuwawa na waasi huko Congo.

Wazazi waliuwawa kwa mapanga, huku dada yake akiuwawa kwa maumivu ya kubakwa na kundi la waasi hao.
Hapo ndo dogo alipotaka kuwa chizi kabisa, ilihitaji kazi ya ziada kutoka kwetu ili kumuweka dogo katika hali ya kawaida.

Ilifika kipindi mpaka tuliona dogo anaweza kujiuwa mwenyew, kwahiyo watu tukaamua awe anaishi na dogo mungine (rafiki yake) katika nyumba aliyokuwa anaishi na marehem Rama ambae alichukua nyumba nzima (flat) na kuweka wapangaji katika vyumba vingine.

Baada ya miezi kadhaa dogo akaomba tumsaidia kumchangia changia ili arudi kwao Congo maana haoni tena sababu ya kukiogopa kifo au kuishi mbali na kwao. Wengi tulijaribu kumsihi kuwa abaki tu huku maana kule hali bado haijawa shwari, lkn yey alikataa kwa madai kuwa wazazi wake waliacha nyumba na mifugo kwahiyo kwa sasa hajui ni nani anaeiangalia nyumba na mifugo hiyo.

Akasema ni bora aende akafanye mpango wa kuuza hiyo nyumba afu atafute nchi nyingine ya kwenda kama ni kurudi huku au aende Tanzania, au Kenya au Uganda.

Baada ya kuona dogo ashapoteza muelekeo wa kuishi au wa maisha ikabidi tukubaliane na ushauri wake, ila tulimtaka auze nyumba na kuwahi kutoka kabla wale jamaa hawajavamia tena kijiji chao, akakubali. Tukachanga ikapatikana kiasi fulan cha hela ambayo ilimsaidia nauli na nyingine ya kuanzia maisha huko aendako.

Dogo alisafiri na kufika kwao salama, na muda mwingi tulikuwa tunawasiliana nae na kushauriana mambo mbali mbali ya kimaisha.

Wakati akiwa katika mchakato wa kupata mteja wa kumuuzia nyumba, ghafla kijiji kikavamiwa na waasi tena ambapo yeye alikuwa ni mmoja wa waliouwawa na waasi hao.

Sisi tulipokuwa tunamtafuta tulimkosa, tukajua labda dogo amepoteza sim, au ashauza ila yuko njiania anakuja.

Ghafla tukapata taarifa kutoka kwa aliekuwa jirani yao ambae alikuwa anafamiana na mkongo mmoja anaeishi huku, kwamb Jems aliuwawa kwa kuchomwa moto na waasi hao akiwa ndani ya nyumba yao amelala usiku. Ni mauaji ambayo yamechukua maisha ya wakongo wengi katika eneo hilo.

Baada ya taarifa hiyo ki ukweli nilijukuta nalia bila kujijua. Dogo amepitia changamoto nyingi za maisha na sasa mwisho wake umekuwa wakusikitisha zaidi.

Walaaniwe hawa waasi wa M23 na wengineo wanaouwa maelfu ya raia wasiokuwa na hatia huko Congo na ulimwenguni kwa ujumla. Dah nimejikuta sina cha kuongea zaidi ya kumtakia pumziko jema dogo Jems.

Inna lillah wainna illayhi rajiun (Sisi wote ni wa Mungu, na kwake Mungu tutarejea)

Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

Mungu ailaze roho yake na wazazi wake mahali pema peponi amiin.

Polee sana mkuu! R.I.P dogo james
 
Inapaswa tutoe sadaka ya shukrani kwa kuzaliwa Tanzania na tuilinde amani yetu
Kweli kabisa mkuu, kuwa mtanzania na kuzaliwa Tanzania ni tunu kubwa tuliojaaliwa na Mungu. Kuna watu wanatamani wangekuwa watanzania leo hii, lkn ndo hivyo imekuwa haiwezekani labda wale majiran zetu wanaoingia nchini kwa njia za panya na kujichanganya na wazawa.
 
Back
Top Bottom