Nimemaliza masomo Canada ninahofia kurudi nyumbani

Nimemaliza masomo Canada ninahofia kurudi nyumbani

Tupe data. Je mshahara wa Canada na mwenye Masters ni kiasi gani?. Huku kabla ya kwenda Canada ulikuwa unalipwa kiasi gani?. Baada ya kujibu maswali hayo basi mimi nitakushauri.
 
Khaa!si waje jamani!seriius mie nikipata hela ndef najikataa mazimaaa!mambo yakikaa sawa naagiza watoto waje!mwarabu ataendelea kumtumikia Magu![emoji28]!

Ukisikia kuna bwana mzungu anahitaj mbongo nishtue!
Poapoa ntakuunganisha usijalii..ila sijui sana kama wanatumia mtandao pendwa[emoji41]

Usiwaze lakini 2020 must yaan tuondoke huko madongorokoni
 
Kama wewe ni mwanamke fanya uolewe uko upate na document ubaki huko Bora uwe Mama wa nyumbani ukiwa ughaibuni.Kama ni mwanaume pambana utengeneze future huko,kama umeshindwa kufanya maamuzi jiandikishe usome PhD.Na ukija na Masters yako mshahara wako utakuwa ni ule wa Bachelor auta badilika.
 
Hahaha labda.. Anampango wa kuja kugombea udiwani 2020....wajua kuna watu wengine huwa wanapenda ego...Huko canada anaona kwamba hakuna anayemjua na hata akiwa anaingiza kitu hawezi kuwa tambia watu...kwa sababu wenye ukwasi niwengi mnoo...

Ila binafsi na mshangaa sana mtoa mada.. .kwa sababu canada kwa sasa ni moja ya nchi zinazo ongoza kwa kuwa na uchumi mkubwa duniani..how come unashindwa kuitumia opportunity kama hiyo ili uweze kuboresha maisha yako......Au Jamaa ni mzalendo huwenda hajaridhishwa na matukio ya canada kuzuia zuia ndege za taifa lake mama.......[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Yaani mfungwa gerezani anagoma kuachiwa huru aje uraiani...

Afu mtu yuko ughaibuni anataka aje uraiani...

Kweli vichwa vimetofautiana ubongo...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa unarudi kufanya nini huku mkuu.. jitupe norway,Sweden,Germany,Finland,South,nk. Kwa sasa huku elimu yako hai-worth kitu. Utakuja na master yako afu ukabebeshwa mabeseni ukauze ulipwe kwa cammisions..
Kama huna connection za uhakika huku jilipue huko huko kiongozi ata ukapige Dishwasing
Unasema Norway...Kuna mzungu yupo bongo hapa toka Norway anasema hakuna kaxi huko anahaha
 
Mimi nimemwelewa mtoa mada, anawaza labda akibaki huko, let's say akapata kazi na nini. Then ikaja kutokea amrudishwa kwao kwa kuzamia coz Naamin aliomba visa ya kuja kusoma and not otherwise.
By the time Inatokea hivyo automatically na huku bongo ile kazi aliyokua nayo itakua imesha Ota mbawa.....
Mwisho wa siku anajikuta amekosa vyote.

Cha msingi we Angalia njia sahihi kama unaamua kubaki huko baki kihalali na kazi utakayopata basi iwe ya kueleweka.

Na kama unaona kazi uliyo nayo huku hailipi au Mazingira ya huku hayakuridhishi basi achana nayo kistaarabu tu.. Ili itakapo tokea unataka kurudi basi uwe na amani ya kuomba kurudi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wana jamvi ninaomba ushauri wenu,

Mimi ni mwajiriwa wa serikalini nilipata nafasi ya kuja kusoma Masters kwa ufadhili wa chuo kimoja hapa Canada. Japokuwa nilifanya kazi kwa mwaka mmoja tu kabla sijaja masomoni.

Muda wangu wa masomo unakaribia sana kuisha na ninaona nafasi za ajira na maisha bora huku niliko kuliko nyumbani. lakini ninawaza nitafanyaje juu ya mkataba wa kazini Tanzania na kama ni maamuzi sahihi kubakia huku baada ya masomo yangu.
Kwa nini uhofie kurudi nyumbani Mkuu? Au unatuzuga kwa kuwa ulishirikiana na MKULIMA kuzuia BOMBADYEE iliyoachiwa majuzi kati? (Jokes).

Hapa cha msingi ni vema ukaja kufanya utaratibu wa kuondoka kwa kuaga. Usitoroke kwani mwisho wa siku, NG'OMBE AKIUMIA MACHUNGANI, HUREJEA ZIZINI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani wewe unaonaje, maamuzi ya maisha yako mwenyewe unakuja kutuuliza sisi, tuambie jinsia yako angalau tunaweza kujua tuna deal na mtu wa aina gani..
 
omba likizo bila malipo
Wana jamvi ninaomba ushauri wenu,

Mimi ni mwajiriwa wa serikalini nilipata nafasi ya kuja kusoma Masters kwa ufadhili wa chuo kimoja hapa Canada. Japokuwa nilifanya kazi kwa mwaka mmoja tu kabla sijaja masomoni.

Muda wangu wa masomo unakaribia sana kuisha na ninaona nafasi za ajira na maisha bora huku niliko kuliko nyumbani. lakini ninawaza nitafanyaje juu ya mkataba wa kazini Tanzania na kama ni maamuzi sahihi kubakia huku baada ya masomo yangu.
 
Unasema Norway...Kuna mzungu yupo bongo hapa toka Norway anasema hakuna kaxi huko anahaha
Watu wanafikiri huko majuu life ni kama kumsukuma mlevi, ndo maana tunamuuliza mtoa mada baada ya kukaa huko na kusoma masters akili yake inamtuma kufanya nini, maana wengine tumefanya hadi PhD na bado tumerudi home..
 
Tunawategemea wasomi kama nyinyi mje mtusaidie kuijenga nchi, kama serikali imechangia kukupeleka huko ni lazima urudi la sivyo utaipata pata
 
Back
Top Bottom