Nimemchukia mke wangu

Nimemchukia mke wangu

Habarini wanajamvi, kama tittle inavojieleza, sina amani ndani ya ndoa kwa muda mrefu sasa najikuta nina stress hadi afya imeanza kuzorota.

Nipo kwenye ndoa mwaka wa 10 sasa, nilifurahia mapenzi ya mke kwa miaka 2 tu ya kwanza ya ndoa. Wakati namwoa mke wangu alikuja na mtoto ambaye alidai ni wa kwangu nami nikampokea, ila kadri siku zinavyosonga namwona kabisa mtoto huyu sio damu yangu kwani hana anachofanania na mimi tofauti tu na tabia kachukua za kwangu , nisichokula naye hali, si kwa kuniiga bali vinakuja naturaly.

Kingine sina ile parental feeling na huyu mtoto, yaani naweza kumpenda mtoto wa ndugu yangu zaidi kuliko huyu mwanangu. Nimempeleka boarding school yaan hata sifikirii kana nina mtoto huko japo nawajibika kwa kila kitu. Amezaliwa mtoto wa 2 mwaka jana ni binti, huyu wala sina swali anafanana na mimi kama mayai, and ninampenda kiasi hata cha kutoa uhai wangu nikampa, huyu kuna muda nakaa nimemwangalia tuuu hata sijui naangalia kitu gani.

Kingine nilichoanza kupata machungu ni kunyimwa papuchi, hii ilianza mwaka wa 2 wa ndoa nikawa napangiwa weekend tu ndo napewa, ilileta ugomvi sana. Yeye akaenda chuo ambacho ni kama 50km toka tunapoishi kwa makubaliano kuwa kila weekend aje. Matokeo yake akawa anakuja kwa mwezi na baadae akawa anakuja wakifunga. Nikaona isiwe shida nikawa namfuata huko.

Baadae napo ikaonekana ruhusa za kutoka ni shida halafu anatoka na uniform kuingia guest ni tabu tu. Nikaacha kuwa nakwenda, rafiki yangu akanishauri nitafute mchepuko, nikafanya hivo hadi nikamsahau kabisa.

Nimeendelea hivyo kwa maumivu maana sikuzoea kuchepuka, baadae nikawa mzoefu nikaona ni haki yangu kuchepuka hata akinikamata nilikuwa namwambia unaweza kuondoka ama kutafuta mwanaume mwingine akuoe.

Shida nliyonayo sasa ni kuwa natumia hela nyingi sana kuchepuka karibu nusu ya mshahara wangu unaishia kwa wanawake. Sina mshahara mkubwa saaana, si wa chini pia. Huwa naangalia chain ya wanawake niliokwishatembea nao ni wengi kidogo toka nlipooa. Nikiri tu kabla ya kuoa sikuwahi kufanya ngono saaaana. Yeye ni kama alikuwa mwanamke wangu wa 3, hivo sikuwa na experience na wanawake. Hata kumwoa sikuchukua muda wa kumfahamu maana tulikuwa tunaishi mikoa tofauti so tulitongozana kwenye simu tu na tukafikia hatua ya kuoana tukiwa tumekutana mara 2 au 3 hivi. Kwa sasa nikihesabu nilokwisha date nao wanafikia hata 30.

Sasa hivi sina hisia naye hata kidogo toka alipobeba mimba alikataa kushiriki tendo la ndoa, na baada ya kujifungua sijamgusa wala kuomba papuchi na mtoto ana miezi 7nsasa.

Kuna kipindi nafikiria kuoa mke mdogo niwe nao wawili, wasiwasi wangu ni dini nitatengwa hadi na ndugu zangu( hili sio tatizo kubwa sana najua litaisha kadri mda unavyoenda), ila tatizo kubwa sijapata mwanamke sahihi wa kuanzisha naye familia kama mke mdogo. Kila ninaokuwa nao naona sio wife material. Natamani sana kuoa mtoto wa kiislam kutoka Tanga, Arusha, Zanzibar, au Kigoma awe kama mke mdogo.
Fanya hiv mkuu kuokoa ndoa yako.Mfanye mkeo ni mchepuko,mpe ingalau robo ya mshahara wako,badala ya hiyo nusu unayoipeleka kwa michepuko nje.Anza kumpenda.utashangaa mambo yanageuka.Haya mambo yamechagizwa na kuchepuka kwako.umeshatengeneza hisia kiroho.Yaani in short umesababisha wewe.

Huwa inatokea wanawake kupoteza hamu ya tendo hasa pale anapokuhisi unacheat
 
Moja ya Njia rahisi ya kumfanya mumeo akuchukie na asikuhudumie ni kumnyima sex,kumpangia sex au kumpa kwa masharti.

Kuhusu kumchukia mtoto ni ujinga wako mwenyewe sababu hupaswi kumchukia mtoto unapaswa kutoa maamuzi ya usaliti uliofanyiwa kama ushahidi upo nasi kulia lia...

Wanawake:inawezekana mwanaume anatelekeza mke na familia

Majibu ndo yapo kwenye huu uzi.
 
Mleta mada kwa maelezo yako pamoja na kutoa lawama kwa mkeo ni wazi kwamba wewe hasa ndiye mwenye matatizo mengi yakiwemo ya kisaikolojia, inaonekana bado HUNA maarifa na uzoefu wa masuala mengi ya ndoa na uhusiano kwa jumla, nakushauri utafute msaada wa kisaikolojia, anza kusoma hata vitabu ili ujiongezee maarifa. Kama hujui wapi pa kuanzia tafuta kitabu kinaitwa Fungate ya Milele, utajifunza mengi sana, ukikwama nitafute pembeni
 
Pole sana ni vizuri ukashirikisha wazazi wa pande zote mbili ikibidi hata viongozi wa Dini, kwanini akunyime haki yako ya msingi ya Ndoa?
Tatizo kubwa hata wakienda kusuluhishana mambo ya msingi yanayofanya wagombane hatasema. Watasuluhisha hewa tu.

Unafikiri atasema mbele za wakwe au mshenga kwamba mke wangu ananinyima papuchi?

Hakuna kitu kigumu kama kusuluhisha ndoa.
 
Hilo kwamba kuna tatizo la kunyimwa uchi inawezekana lipo lakini ni mara ngapi humu tumesoma ME wakilalamika kunyimwa uchi kwa visingizio mbali mbali hadi wengine kuomba uchi wa house girl na wengine hata kufikiria kuwaoa HG? Kuhusu KE kunyimwa gegedo nimesoma labda moja tu au mbili lakini za ME kulalama kunyimwa uchi ni milioni 😜😜😜
Kitendo cha mkeo kukunyima haki yako ya ndoa inaonesha kuna tatizo ambalo hapa kwenye uzi wako umekataa kuandika.Umenishangaza kuweka chuki kwa mtoto kisa hajafafa nawe uzi wako kuna vitu vingi umefukia ili unekane u sahihi.
 
Hilo kwamba kuna tatizo la kunyimwa uchi inawezekana lipo lakini ni mara ngapi humu tumesoma ME wakilalamika kunyimwa uchi kwa visingizio mbali mbali hadi wengine kuomba uchi wa house girl na wengine hata kufikiria kuwaoa HG? Kuhusu KE kunyimwa gegedo nimesoma labda moja tu au mbili lakini za ME kulalama kunyimwa uchi ni milioni 😜😜😜
Mpendwa nijuavyo sex ni hisia jiulize kwa nini mkewe agome kumpa haki yake ina maana hana hamu ya tendo. Kuna kipindi inafikia kwenye mahusiano hutamani hata kiss kutoka kwa mwenzio hii yote inatokea baada ya migogoro ya mara kwa mara.
 
Melezo yako yamejaa hisia nyingi za maumivu , na hapo amekufikisha mke wako, sasa kitu ambacho sijasikia nikwamba umefanya jitihada gani za kimazungumzo kuweka mambo sawa wewe na mke wako , je wazazi wanajua hali mliyonayo hapo ?
 
Hilo ni kweli kabisa lakini si mara zote kutokana na maelezo mbali mbali niliyowahi kuyasoma humu. Nakumbuka jamaa mmoja mbongo mke mbongo wako majuu na watoto wao wawili wadogo. ME alilalamika humu kunyimwa uchi na mkewe kwa madai kwamba wakitoka kazini anakuwa amechoka. Mume akaamua kuanza kusafisha nyumba na kuwaosha watoto kila siku lakini hakukuwa na ahueni kwani mke alikuwa ni lazima aangalie vipindi vyake kwenye TV kuanzia mbili usiku hadi saa tano usiku kisha kudai masaa yameenda na anaamka asubuhi sana. Mume akaamua kuanza kuchepuka.

Bro nampa kila kitu na ninaonyesha upendo wa hali ya juu kwake, ila sina ile feeling ya mzazi kwa mtoto wake, nafikiri umenielewa. Nampa kila kitu na mama yake hahusiki kwa kila kitu yaan yy hela yake nishamwambia ni yake ya matumizi binafsi. Hivo mshahara wake huwa siugusi
Kuna kitu umeshajenga kwenye mind, tatizo lipo hapo, jitahidi kuondoa hilo kwanza
 
Hilo ni kweli kabisa lakini si mara zote kutokana na maelezo mbali mbali niliyowahi kuyasoma humu. Nakumbuka jamaa mmoja mbongo mke mbongo wako majuu na watoto wao wawili wadogo. ME alilalamika humu kunyimwa uchi na mkewe kwa madai kwamba wakitoka kazini anakuwa amechoka. Mume akaamua kuanza kusafisha nyumba na kuwaosha watoto kila siku lakini hakukuwa na ahueni kwani mke alikuwa ni lazima aangalie vipindi vyake kwenye TV kuanzia mbili usiku hadi saa tano usiku kisha kudai masaa yameenda na anaamka asubuhi sana. Mume akaamua kuanza kuchepuka.
Huyo dada amekosea Mume hanyimwi ile kitu hata kama mmegombana ni haki yake .
 
Hilo ni kweli kabisa lakini si mara zote kutokana na maelezo mbali mbali niliyowahi kuyasoma humu. Nakumbuka jamaa mmoja mbongo mke mbongo wako majuu na watoto wao wawili wadogo. ME alilalamika humu kunyimwa uchi na mkewe kwa madai kwamba wakitoka kazini anakuwa amechoka. Mume akaamua kuanza kusafisha nyumba na kuwaosha watoto kila siku lakini hakukuwa na ahueni kwani mke alikuwa ni lazima aangalie vipindi vyake kwenye TV kuanzia mbili usiku hadi saa tano usiku kisha kudai masaa yameenda na anaamka asubuhi sana. Mume akaamua kuanza kuchepuka.
Kazi kweli, kama jitahada zangu zikikwama naona hatari ya kwenda nje ya ndoa, fasta naanza mchakato wa kumpiga chini.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wala si kulaumu ni haki yako na baadhi ya KE kunyima uchi wanaitumia kama silaha ya kumuadhibu ME bila kujua pia inavuruga ndoa na hata kuweza kuivunja kabisa.
Kazi kweli, kama jitahada zangu zikikwama naona hatari ya kwenda nje ya ndoa, fasta naanza mchakato wa kumpiga chini.
 
Suluhu inaanza na nyie wenyewe,
Mume ndiyo muamuzi wa ndoa iendeje, kama kuna mistake ulianza kuzifanya lazima wewe mwenyewe uanze kwa kuweka mfano kuachana nazo
Tatizo kubwa hata wakienda kusuluhishana mambo ya msingi yanayofanya wagombane hatasema. Watasuluhisha hewa tu.

Unafikiri atasema mbele za wakwe au mshenga kwamba mke wangu ananinyima papuchi?

Hakuna kitu kigumu kama kusuluhisha ndoa.
 
Tatizo lipo kwako mkuu. Badilika kwanza wewe ujipende mwenyewe kwanza.
 
huna mke hapo zaidi ya mla bure na mjaza choo

anabana papuchi , it means hana kingine cha ku offer kwenye ndoa

mpige chini, stick na mchepuko,
 
Melezo yako yamejaa hisia nyingi za maumivu , na hapo amekufikisha mke wako, sasa kitu ambacho sijasikia nikwamba umefanya jitihada gani za kimazungumzo kuweka mambo sawa wewe na mke wako , je wazazi wanajua hali mliyonayo hapo ?
Hatuna wazazi wote. Kwa kawaida mm na mke wangu wote sisi wakimya kupitiliza si waongeaji ongeaji so nishamweleza hapo nyuma kuwa anachofanya sio vizuri baada ya kuona hashtuki basi nikatafuta akili ya kutoka nje. Ukitukuta wala huwezi kugundua hatuelewani si chimbani wala sebuleni, tunaongea vizuri tu na mda mwingi rukitoka job tunautumia room maana mm pia huaa nikitoka kazini saa kumi namoja lazima inikutie nyumbani, haijalishi nina mgegedo ila piga ua saa 1! Jioni kila ratiba inaahirishwa naenda kwa mke wangu
 
Ndugu yangu niliandika walaka mrefu hapo juu upitie vizuri ,mpende mkeo rekebisha yako kwanza,usimchukie mtoto mpende sana,mwombe mkeo msamaha kwani ukijishusha utapungukiwa kuwa mwanaume ila utakuwa umetengeneza kitu kikubwa mbele za Mungu, mwisho hachana na michepuko kaka.all the best
 
Back
Top Bottom