Justine Marack
JF-Expert Member
- Jul 31, 2014
- 612
- 1,698
Katika Kampuni yangu ya usafirishaji nilikuwa na Mfanyakazi muhimu lakini shabiki wa Yanga. Kazini alikuwa anatimiza majukumu yake vizuri sana. Tatizo lilianza pale nilipoanza kujua kuwa anashabikia Yanga. Huyu jamaa alikuwa yuko tayari kukosana na wafanyakazi wengine sababu ya kubishana mambo ya Yanga. Hii ilinifanya nijiulize maswali mengi, hasa nilishangaa kuona mtu anakuwa kama mwehumwehu.
Nilimvumilia sana kwa ujingaujinga wake, ikafikia mpaka utendaji kazi wake ukaanza kuyumba na ushirikiano na wenzake ukapungua.
Jana kukatokea ubishani juu ya Feisal Toto. Wakati Aucho alipoonekana kukamia kumuumiza Feitoto wakati wa mchezo, kuna kijana alikuwa analaumu kuwa Aucho anamchezea vibaya Feitoto. Sasa pale kulizuka mzozo mpaka kuzima TV.
Hapohapo nilimfukuza na Leo namlipa stahiki zake. Sitaki ujinga Mimi. Na siwezi tena kuajiri mtu anaye shabikia Yanga.
Wanakuwaga hawapo sawa, haijalishi amesoma au hajasoma. Hata marafiki wanao shabikia Yanga naanza kuwapunguza.