Nimemfungulia wife biashara ndogo tu! Ila naona kama ishaanza kumpa jeuri Najutaaa

According to psychology
Women don’t need balance even if they have money they will want you to pay for every expenses
 
Mke atulie ndani only.
 

Huo ni mtazamo potofu
 
Umenena Vyema Mkuu.
 
Wanawake wana drama nyingi
 
😂
"Utazaa kwa uchungu na mume atakutawala." (Mungu)

Mengine kujitakia
 
Mkuu ulikosea sana kumfungulia biashara mkeo,kama ulitaka kuoa mfanya biashara ungetafuta mwanamke mfanya biashara,wewe ulioa mke mama wa nyumbani sasa umkambadili na kumfanya mfanya biashara,hili ni kosa kubwa sana,mke ukimuoa mwache Aishi kama ulivyomkuta ikiwezekana mrudishe nyuma kabisa asisonge mbele


Kumfungulia biashara mke ambaye hukumuoa akiwa anafanya biashara ni kosa kama kosa la kumsomesha mwanamke ili uje umuoe,Mimi Nina mifano mingi sana ya wanaume waliojaribu kuwasukuma wake zao mbele mwisho wa siku ndoa zikawashinda.

Mimi mke wangu ni mwalimu,mwaka Jana niliona harakati za maafisa kumpigia promo ili awe mkuu wa shule,nilimwambia sitaki habari hizo,Mimi sikuoa mkuu wa shule,na kama ningetaka mke mwenye cheo cha mkuu wa shule basi ningetafuta


Hawa wanawake ni hatari sana.
 
Mwachie tu, usipende kushindana kama umeamua kumfungulia biashara mwachie aendeshe kadri atakavyo labda kama lengo lilikua sio hilo umefanya sawa.

Kama ataamua kubadilika kwasababu ya biashara uliyomfungulia nadhani kuangalia namna ya kukabiliana aidha kumwacha aende ila hamna haja ya kumweka mtu mateka kiuchumi ukiogopa kwamba atakubadilikia, hayo yatakua ni mashindano.

Binafsi ningempa baraka na kumsisitiza apitie njia bora za kukuza hiyo biashara ili ikue na ikue zaidi.

Nadhani nitagombana na yule anaeharibu mtaji kwa kufanya vitu visivyo vya msingi kuliko kuhofia ya kwamba atabadilika😁
 
📌🙌
 
Sana
 
Jamaa yangu niliyesoma naye form six na chuo Kila siku analia na kujutia ile siku aloamua kumfanyia maombi ya nafasi ya ualimu mke wakev aliyeuwa mama wa nyumbani kwa miaka 8.

Baada ya mwanamke kupata financial freedom,hakuna maelewano Wala masikilizano,wakati mke Hana kazi , ndoa ilikuwa na amani sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…