Nimemiss kupendwa....

Nimemiss kupendwa....

Ukiona hivyo ujue familia imekuwa majukumu yameongezeka ule muda wa kupetiwa petiwa umegawanyika ktk majukumu mengine, kwa watoto wenu wapendwa, na kwa wakwe, acha kukariri maisha na kutamani mombo ya wakati ukiwa kigori na leo ni mama wa watoto watatu.
Kila jambo ktk familia na maisha ya mwanadamu lina muda na ukomo wake, kubaliana na hali na mabadiliko ktk mwili wako na hasa maisha ya familia. Waza kuijenga familia ili uwe msaada kwa baba watoto badala ya kikwazo, hata yeye hakuwa na mrembo mmoja wakati huo na hata sasa hapendi ila amekubaliana na mabadiliko kwa afya ya familia.
Naelewa, ahsante
 
Mapenzi yako na mwenzio yamekwishakomaa sasa. Yataenda, mpaka mtatengana vyumba. Siyo kwa sababu ya ugomvi.., la hasha. Kwa sababu ya kuzoeana tu, kutokutaka kujambiana, ama kupigiana kelele za kukoroma, nk. Hata ukibadilisha mwenza... ni hivyo hovyo... mwanzoni mapenzi motomoto, baadae yatachuja tu. Ni kawaida ya wanadamu. Utamaliza mabucha, nyama ni ile ile.
Ushawahi kujisikia hisia za hivi?unakua kwenye relation ila muda mwingine unajihisi upweke unatamani ukakae mahali upigwe upepo, kuna muda unajisikia moyo umejaa mapenzi hadi yanamwagikia unatamani umuoneshe mtu ila ndio utaonekana mfilipino tu kama sio muhindi....hizi hisia zimekua zinajirudia sana kwangu, nahitaji kuwa updated teh sijui kuwa updated sijui kujiupdate aahh hivo hivo.

Nimemiss sana kupendwa, kuoneshwa mapenzi kwa vitendo, asubuhi style ya kuamshwa iwe kushikwa shikwa nashtuka ooh nakutana na vipi baby mambo, achana na hizi style ya sahivi nakurupuka natupa kule shuka baada ya kupigwa pigwa mgongoni mama nanii amka ukampe mtoto uji, namiss kupigiwa simu kusemeshwa vitu vizuri vizuri, kukutana na text nzuri "unafanya nini njoo nipo huku desh desh garden" ukiachana na sms za mama nanii andaa msosi nakuja sijala, mama nanii hivi uliangalia luku units zimebaki ngapi, nmemiss kupokea kiparcel ndani kuna viatu, gauni nk...nmemiss zile siku nikiwa off mood nawekwa kati ya miguu naulizwa nini mbaya mamaa jamani sahivi nini off mood hata hiyo mood ipige shoti buyuuu hahaha (baba niokoeeee), namiss kuwa huru I miss mambo mengi mnoo.

leo nimevurugwa hadi basi, mnifariji tu, alamsik.
 
Sasa hiyo unayoishi ndio reality ya maisha. Yale ya zamani ishapita hivyo, sasa hivi ni mwendo wa bills za LUKU, king'amuzi, maji nk. Ukianza kusomesha ndio mziki utakuwa mnene zaidi, mkoa za kujenga ndio utaipata raha zaidi. Hapo omba Mungu kipato kiwe kinaongezeka ili kukidhi mahitaji ya kila siku, otherwise kubebishwa utakusikia kule Nyamagana...
 
Hili ndio la muhimu. Na pengine ndilo linalom-keep busy mume wake. Ashukuru kuwa na mme ambaye anatumia muda wake kwa mabo ya msingi na siyo text message za babe, babe....
Hapo omba Mungu kipato kiwe kinaongezeka ili kukidhi mahitaji ya kila siku,
 
Just normal feelings Madame.
Unasikiaga kula mifupa meno yangaliko! Ukivuka stage...zitabaki story tu Kama hizi
 
Ndo nakafanyia haka kabinti nowadays haya yote.Ila naona kama kanachukulia poa tu.
 
Kiukweli hata na mimi nimemiss kupenda. Ile feeling niliyokuwa nayo kitambo hicho yaani mtu usipomuona siku tatu moyo hautulii ni kama kiu flani hivi [emoji4][emoji4][emoji4][emoji4].. Siku hizi hiyo relationship ninayo zaidi na pesa maana hakuna dollar yenye drama wala mapenzi ya uongo
 
Endelea tusilaumiane Hapo mbele
Kipigo Cha mbwa koko shaur yako
Acha kunipiga mkwara, ulichozoea kufanyiwa usilinganishe na wengine
tapatalk_1542630832304.jpeg
 
Back
Top Bottom