Nimemiss kupendwa....

Nimemiss kupendwa....

Bora hata ngekua nshapata darasa, ningekaa tu nakatika zangu na kurusha wowowo huku na kule hebu nifanyie mpango asee
Hahaaah na wasiwasi baba nanihii kapata mchepuko mtaalamu wa mambo hayo ya kurusha wowowo so unataka uingie darasani ili upindue matokeo umrudishe baba nanihii
 
Pole waachie wadogo zako,wewe endelea kuhisi tu ni muda wa wadogo zako sasa,wewe km zimesoma sana
 
Evelyn upo mama? Umeadimika balaa
Ushawahi kujisikia hisia za hivi?unakua kwenye relation ila muda mwingine unajihisi upweke unatamani ukakae mahali upigwe upepo, kuna muda unajisikia moyo umejaa mapenzi hadi yanamwagikia unatamani umuoneshe mtu ila ndio utaonekana mfilipino tu kama sio muhindi....hizi hisia zimekua zinajirudia sana kwangu, nahitaji kuwa updated teh sijui kuwa updated sijui kujiupdate aahh hivo hivo.

Nimemiss sana kupendwa, kuoneshwa mapenzi kwa vitendo, asubuhi style ya kuamshwa iwe kushikwa shikwa nashtuka ooh nakutana na vipi baby mambo, achana na hizi style ya sahivi nakurupuka natupa kule shuka baada ya kupigwa pigwa mgongoni mama nanii amka ukampe mtoto uji, namiss kupigiwa simu kusemeshwa vitu vizuri vizuri, kukutana na text nzuri "unafanya nini njoo nipo huku desh desh garden" ukiachana na sms za mama nanii andaa msosi nakuja sijala, mama nanii hivi uliangalia luku units zimebaki ngapi, nmemiss kupokea kiparcel ndani kuna viatu, gauni nk...nmemiss zile siku nikiwa off mood nawekwa kati ya miguu naulizwa nini mbaya mamaa jamani sahivi nini off mood hata hiyo mood ipige shoti buyuuu hahaha (baba niokoeeee), namiss kuwa huru I miss mambo mengi mnoo.

leo nimevurugwa hadi basi, mnifariji tu, alamsik.
 
Kweli umevurugwa! Maana hapo unaonekana una Mwanza wimbo wa Diamond kama gunia hivi.

Yaani jipu limekosa mkunaji!

Yaani upele umekosa kucha!

Pole sana!
 
Back
Top Bottom