Nimemjengea mama yangu nyumba nikiwa bado nipo kwenye 20's

Nimemjengea mama yangu nyumba nikiwa bado nipo kwenye 20's

Financial markets ndio nini ? Mbona unatufanya wajinga wewe dogo, umepiga picha nyumba ya Shemeji yako unakuja kujimwambafai nyumba yenyewe unapiga kwa kuiba unapiga dirisha unatuona mbwiga.

Hao kuku ulianza nao wangapi na mpaka sasa una wangapi? Unawafugia wapi? Nipe mahitaji yao ikiwemo chanjo na aina ya chakula unachowapa. Wanakomaa baada ya muda gani? Unawauza wapi na kwa bei gani? Unauza wapi?

Kilimo, unalima nini? Wapi? Kwa ukubwa wa shamba upi? Mtaji upije? Unatumia mbegu gani?¡

Halafu nielezee hiyo kitu umesema inaitwa financial markets ndio biashara gani aisee? Ni kitu gani financial Market???

Dogo acha balehe ukinijibu hayo maswali kama kweli unalima na kufiga nitajua tu maana unatufanya wengine wajinga humu. Financial markets mkubwa wewe[emoji2]
Mkuu,nimeona Kama umeandika kwa jazba ukiwa na kinyongo moyoni(Sina uhakika),lakin Cha kukushauri ni kwamba kinachoongoza maisha ni AKILI sio UMRI
#ukiwa mvivu usiwe n wivu#
 
Tutajuaje kama ni kweli umeishia Form 6 tu kwa uandishi huo na kiingereza mujarab?

Tutaamini vipi kuwa kweli umejenga wewe na si kuwa amejenga mwingine ukapiga tu picha na kupost hapa?
 
Tutajuaje kama ni kweli umeishia Form 6 tu kwa uandishi huo na kiingereza mujarab?

Tutaamini vipi kuwa kweli umejenga wewe na si kuwa amejenga mwingine ukapiga tu picha na kupost hapa?
Lugha ni kigezo Cha elimu mkuu!?,
Ina maana aliyeishia form 6 hawezi kuandika vizuri....!?

-imani ni nini!?,
 
mimi nimependa dogo anavyojibu maswali[emoji23][emoji23], Anajua kujibu vzuri maswali, wacha amjengee mama yake nyumba[emoji1787][emoji1787]
 
Vinginevyo uwe GINIMBI AU IVAN
Sihitaji kuwa Ginimbi au Ivan,najihitaji Mimi zaidi mkuu
Mkuu,niamini Mimi ,unaweza kufanya makubwa Sana Kama tu utatambua nafasi yako.....
 
Sihitaji kuwa Ginimbi au Ivan,najihitaji Mimi zaidi mkuu
Mkuu,niamini Mimi ,unaweza kufanya makubwa Sana Kama tu utatambua nafasi yako.....
Wengi wanatambua nafasi zao. Sijui kama unajua maana ya kutambua nafasi yako?. Na wanapambana ili kufikia kucaver ile nafasi yao lakini inashindikana,mpaka ana miaka 40 bado hajafikia malengo,japo wanatamani sana wajenge
 
Pole halikuwa jukumu lako bali la Baba ako!!!Jukumu lako ni kuandaa kwako pawe pazuri ili uje ulee watoto wako vema na wazazi wako wakizeeka tu!!Ulijipa kazi ambayo sio yako!!!!NAKUOMBEA USIJE UKAUMIA MUNGU AKIMCHUKUA MAMA NA NYUMBA IKAANZA KUGOMBANIWA NA NDUGU ZAKO KWA KIGEZO NI YA MAMA !!!!NAKUANDAA TU MAPEMA!!!
 
Pole halikuwa jukumu lako bali la Baba ako!!!Jukumu lako ni kuandaa kwako pawe pazuri ili uje ulee watoto wako vema na wazazi wako wakizeeka tu!!Ulijipa kazi ambayo sio yako!!!!NAKUOMBEA USIJE UKAUMIA MUNGU AKIMCHUKUA MAMA NA NYUMBA IKAANZA KUGOMBANIWA NA NDUGU ZAKO KWA KIGEZO NI YA MAMA !!!!NAKUANDAA TU MAPEMA!!!
-Moja ya malengo yangu ni kuwajengea wazazi wangu nyumba,mzazi mmoja(baba yangu) alitangulia mbele za haki kabla hata sijamaliza advance (kazi ya mola haina makosa),sikuacha kutimiza NADHIRI yangu ndipo nlipomjengea mama yangu..

-wajibu wa wazazi ni kuhakikisha watoto wao wanapata mahitaji muhimu(makazi,mavazi, malazi) pamoja na ELIMU bora
-wajibu wa watoto watakapokua vijana ni kuhakikisha wazazi wao wanapata mahitaji muhimu(mavazi,malazi na malazi) pamoja na UPENDO....it's like reversible reaction[emoji18]

"Waheshimu wazazi wako ili upate miaka mingi na heri duniani"....
 
Niliwahi kukutana na scenerio ya aina hii, ila yenye nyongeza kidogo. Kuna mtu aliwahi kufanya kitu kama hiki ulichofanya wewe. Baada ya hapo, miaka kadhaa mbele mwenzake naye akafanya hivyo hivyo naye akamjengea mama yake. Kwa hiyo nyumba zikawa mbili wakati huo mjomba wao yuko jirana anaishi kwenye Kibanda cha nyasi. Huyu wa kwanza wakati anajenga, hakuwa na uwezo wa kuwajengea wote, mjomba na mama.

Alifanikiwa kumjengea mama tu. Huyu wa pili wakati anamjengea mama, wala mama hakuwa anahitaji nyumba nyingine ya pili, na wakati mjenzi wa kwanza anajenga, huyu mjenzi wa pili hakuwa na uwezo wa kujenga, alikuja akapata uwzo huo miaka michache mbele. Badala ya kumjengea mjomba, naye pia akaamua kumjengea mama tena na kwa bahati mbaya mama naye hata hakuwa na ile kauli ya kusema "mjengee mjoba wako badala yangu".

Baadaye huyu wa kwanza akaja akagundua kuwa kumbe wa pili alijenga ili kumpiku mwenzake, wa kwanza na diyo maana hakuona haja ya kumjengea mjomba ambaye yeye alikuwa bado yuko kwenye hali mbaya.

Mungu atusaidie sana, mashindano watoto wamezaliwa tumbo moja halafu mnakua wote mkiwa mnajua kila mmoja ana akili timamu kumbe mojawapo ni chizi. Kuna uwezekano kuna watu ambao huwa tunaishi nao kwenye familia zetu wakiwa wamevaa maumbile ya binadamu, lakini kumbe roho zao ni za mapepo ya kuzimu, wakala wa shetani 100%. Unaishi nalo ukiwa ujua kuwa ni bindamu kumbe ni pepo la kutoka kuzimu
Magepi ni lazima tu
 
Mleta mada umeshapata mpenzi toka JF maana humu kuna mademu wanajua kunusa pesa ilipo.
Otherwise kama ulituletea chai bila sukari.
 
Pole kijana kwa kua na wazazi masikini wasiokua na makazi ya kuishi ......binafsi wazazi wangu walinijengea nyumba,kabla hata sijazaliwa
Hongera, wazazi wengi hususani akina baba hufanya uvivu ujanani na starehe, uzeeni wanategemea watoto ndio wa kujenga nyumba.
 
Pole kijana kwa kua na wazazi masikini wasiokua na makazi ya kuishi ......binafsi wazazi wangu walinijengea nyumba,kabla hata sijazaliwa
Ila haimaanishi kwa sasa bado wazazi ni masikini, kwa sasa ni matajiri nao, ni suala la kuwahi na kuchelewa tu. Wako waliwahi, wake wamechelewa, kitu ni kile kile.
 
Back
Top Bottom