Nimemkuta jirani yangu anazunguka nyumba yangu usiku

Nimemkuta jirani yangu anazunguka nyumba yangu usiku

Guru Guja

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2019
Posts
217
Reaction score
285
Mimi nimepanga kwenye nyumba kubwa yenye vyumba vya uwani. Mimi nafanya biashara nina maduka ya nguo Kariakoo nimepaga bado sijamaliza ujenzi kwangu Madale.

Usiku wa leo niliamka ghafla nilipoona kama kivuli kwenye kioo cha dirisha nikasogea polepole kuangalia kama kuna mwizi nikashangaa kumuona jirani yangu na mkewe wanazunguka nyumba ninayoishi ambayo ni nyumba kubwa wakiwa uchi kabisa.

Mara ya tatu walipofika dirishani nilikuwa nimeshafungua nikawauliza mmebakiza mizunguko mingapi? Walishituka mke akajificha nyuma ya mumewe maana alikuwa uchi.

Nikamuambia mama Omari kumbe una kitako cha ndanindani. Mume akalopoka. Tumeshaaribu dawa.

Wakarudi Ndani kwao. AsubuHi leo Hawataki kuonana nami nimempigia simu jirani hapokei nilitaka nimsalimie kagoma jirani ana roho mbaya sana.
 
Heading umeandika vizuri kabisa, bila spelling errors zote, halafu kwenye contents za Uzi ukaamua kujitoa akili
Duuuuuuuuuuh umenikpsea sana dugu yagu mimi sina akili?eshima kitu ya bule dugu
 
Pole kaka, ila jitahidi kuwa unarejea chapisho unalotaka kulichapisha.

Kwenye kichwa cha habari umesema 'Nyumba yako', kwenye maelezo ukasema umepanga. Na hayo maelezo kidogo hujayatiririsha inavopaswa. Anyway, isiwe kesi. What's your hometown? Nisijekuwa nashauri mhadizabe! 😁
 
Back
Top Bottom