Mimi ni Mmasai na ninafuga.
Swala la kiangazi ni tata sana. Watu wengi huhangaika kuokoa mifugo yao isife kwa sababu ya njaa.
Sasa inapofikia swala la kulisha kwenye mashamba ya watu kuna utata mwingi sana.
Ukiona kiangazi kimezidi, tafuta mmasai muambie anunue shamba lako. Chukua pesa weka mfukoni.
Vinginevyo watakula kwa lazima.
Ila kama shamba limeshavunwa, nawe usiwanyime majani waokoe mifugo yako.
Asali inau vibaya sana, lakini ni wajanja sana siku hizi. Wanatangulia kukagua shamba kama limetiliwa sumu au asali kabla ya kuruhusu mifugo yao kuingia.
Ukishakuta wameingiza, ndugu yangu usizozane nao. Bali lia kama kuwalaani. Waambie acha ng'ombe wenu washibe huku wanangu wakilala njaa. Wamasai tunaogopa sana laana. Wanaweza kukupuuza, lakini watakurudia kukuomba radhi. Watakulipa kidogo.
Kama unadhani kudhuru ndiyo tiba, basi wadhuru ng'ombe. Siyo wao. Ukimuua mmasai, hama eneo hilo na usirudi tena. Watakusaka hata bila ta serikali.
Kwetu huo upuuzi tumeshauacha. Wabongo wenzetu hatuingilii mashamba yao. Tunamalizana nao mezani.
Ila mashamba ya wawekezaji wa Kizungu, maskini tutavamia tu.