Wachaa...umeguswa pia. Iko hivi, ukitaka familia zikae sawa bila kujali ndugu wa kike au kiume, hasa wageni wenyeji, ni kuwaingiza kwenye mfumo wa mazingira yenu. Na hiyo heshima ihubiriwe kwa pande zote wenyeji waheshimu wageni na vivyo hivyo kwa wageni. Heshima pande zote inapunguza makando kando mengi ikiwemo hii ya roho ngumu ya kukwazika na mtu kununuliwa shati.
Kikubwa ni mawasiliano mema kati ya wenye nyumba wenyewe, hasa kwenye mustakabali wa ndugu zao.
Ila bado nakataa, nikaanze harakati za kusomba maji ya shemeji wa form 4! Hapana, na kufuga kucha au bila kufuga hapana.