LIKUD
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 18,037
- 33,681
- Thread starter
- #41
Akupe ya mokasini ee
I say sintorudia tena. Nina mshipa mmoja. Mara ya mwisho ilikuwa 2003. Nilikuwaga nikimpiga mtu ngumi mambo yafuatayo ilikuwa lazima yatokee.Usirudie kumpiga hivyo mwenzio msije mkagawana majengo ya serikali mkuu
1. Lazima azirai.
2. Lazima nikimbie.
3. Usiku silali kwetu nalala kwa uncle.
4. Lazima niamke saa kumi na moja alfajiri na kwenda hadi nyumbani kwao na jamaa kuona kama wameweka turubai kuna msiba.
Hali hii ilinitesa sana hadi nikaweka nadhiri kwamba sintopigana tena maishani.
Mara ya mwisho nilimliga jamaa akazirai nikakimbia.
Alafajiri naenda kwao kuchungulia nikakuta turubai nikasema "
Mungu wangu nimeua" sikutaka hata kuuliza nani amekufa.
Wakati nipo kwenye harakati za kutaka kutoroka nikasikia tangazo msikitini wanatangaza msiba kumbe aliefariki alikuwa baba wa jamaa niliye mpiga akazirahi nikasema " Alhamdulilahi"