Nimempikia shemeji yenu njegere ngumu haziivi, msaada tafadhali

Una uhakika umewasha moto?
 
Chemsha tena baada ya kuweka kijiko kimoja cha sukari, utakuja kunipa zawadi
 
Ungejihami mapema ili akianza kula ajue ni kitu gani anakutana nacho.

Kuna muuza njegere aliwahi kuniambia za Morogoro ni laini na zinaiva haraka.
Njegere kavu ndo mtihani zaidi sasa na zina ukorofi sana. Huko Usukumani Ntuzu kuna njia mbalimbali ambazo nimeshaziona zikitumika ili kuepusha shari (Japo sina uhakika kama njegere ndiyo nduulu)

1. Unaweza ukazikaanga kabla ya kuzipika hasa kama zimekaa muda mrefu. Unazikaanga kavu kavu tu bila mafuta ukiona zimepata moto ndo unazipika. Nusu saa tu zishasalimu amri na hakuna hata moja itakayogoma kuiva.

2. Mpe mtoto wa kike chini ya miaka mitano ndiyo aziweke chunguni. Kama ni zile ngangari zimekaa zaidi ya miaka miwili-mitatu hivi ni lazima awe uchi anapoziweka chunguni. Unaambiwa eti zoooooteee zitaiva chap.

3. Tumia mkono wa kushoto wakati wa kuziweka chunguni. Na unapoziweka usiongee ๐Ÿ˜ณ

Kwangu mimi njia ya kwanza tu ndiyo angalau inaeleweka. Njia 2-3 sijui zinavyofanya kazi lakini ukiongea na wenyewe wanawake watakuapia kuwa njia hizo ni konki na hazina kupoteza muda kama hiyo ya kwanza.

Wabeja ๐Ÿƒ๐Ÿฟโ€โ™‚๏ธ๐Ÿƒ๐Ÿฟโ€โ™‚๏ธ๐Ÿƒ๐Ÿฟโ€โ™‚๏ธ
 
wafundishe hawa akina Abigail wanatuwekea chumvi na blueband kwenye ugali...๐Ÿคฃ
Duh hii ngeni sisi kwetu ilikuwa mama anachemsha anaweka chumvi tu usiku ana mwaga kwenye sinia mnaanza kula uku story zinaendelea sasa hii mpya magadi
 
We msukuma., nazungumzia zile njegere mbichi za kijani. Sio hizo za kukausha...
Anyway, asante kwa maujuzi kuhusu njegere kavu, nitafata ushauri wako siku nikizipata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ