Nimempikia shemeji yenu njegere ngumu haziivi, msaada tafadhali

Nimempikia shemeji yenu njegere ngumu haziivi, msaada tafadhali

Kama ni aina ya wanaume wanaoongea maneno hawamalizi kazi unayo 😁.

Kuna wengine hususa hadi kutoa chakula ya NDOA.
Kesi zake huwa haziishi, hana jambo dogo.
Na isitokee bahati mbaya katafuna kajiwe ha haaa my friend...haendelei tena kula na kwa kosa hilo utanuniwa wiki nzima au zaidi
 
Ipo hivi.
Hizi njegere nimezibandika kuchemsha tangu saa 6 na nusu hadi saa 8 kamili, ni ngumu hazilainiki.
Huyu shemeji yenu hapendi njegere ngumu, sikuwa na jinsi nimeunga hivyo hivyo nikamtengea ale, nipo mahali nimekaa nasubiri bomu lilipuke maana najua atafoka hadi kesho.

Msaada tafadhali jinsi ya kuzitambua njegere ambazo haziivi ili nisifanye kosa la kuzinunua siku nyingine.

Mwachiluwi nipe maujuzi
Hongereni sana muliooa wanawake wanaotumia muda mwingi mtandaoni kuliko jikoni kuboresha mapishi yao
 
Kama siyo nyingi weka kidogo. Hata ukitaka nyama iwive haraka tunaweka sukari badala ya chumvi ya magadi. Hata maharage. Jaribu na uniletee zawadi yangu baada ya kufanikiwa
Nashukuru sana.
Kwenye maharage nimeshawahi kujaribu na ikafanya kazi.
 
Kama siyo nyingi weka kidogo. Hata ukitaka nyama iwive haraka tunaweka sukari badala ya chumvi ya magadi. Hata maharage. Jaribu na uniletee zawadi yangu baada ya kufanikiwa
Binafsi sipendi sukari kwenye maharagwe nilimtembelea rafiki nukakuta kapika maharagwe kaweka sukari ile kutia mdomon tu nikamuuliza maharagwe umeweka sukari akasema ndio sikuendelea kula

Sukari itumike vizuri mboga weka chumvi chumvi nikiungo tosha
 
Unaweka kidogo sana hata huwezi kuisikia. Siyo unaungia kama chumvi
 
Hongereni sana muliooa wanawake wanaotumia muda mwingi mtandaoni kuliko jikoni kuboresha mapishi yao
Sasa unadhani haya maujuzi ya kufanya njegere zilainike ningeyapata wapi zaidi ya hapa mtandaoni? Unadhani ukijifungia tu jikoni bila kutafuta means ya kujifunza ndo utajua kupika?
Dunia ya sasa kila kitu kipo mtandaoni, haikwepeki
 
ww utakuwa uliweka chumvi mwanzoni maana ukiweka chumvi kwenye njegere au maharage wakati wa kuchemsha hapo utakesha hata masaa 4 na bado kuiva..ukitaka kuiva haraka iwe ngegere,maharage,mbatata au muhogo wa kuchemsha usiweke chumvi mwanzoni ila utaweka mwishoni au wakati wa kuunga..ili kuivisha haraka vitu vya kuchemsha weka mafuta ya kupikia kidogo tu hapo yataiva fasta ndani ya mda mfupi tena pishi linakuwa laini mno na usipokuwa macho baada ya kuweka mafuta ya kupikia utakuta rojo tupu kwani kuiva kwake sio mchezo ukizubaa.!
 
Back
Top Bottom