Nimempikia shemeji yenu njegere ngumu haziivi, msaada tafadhali

Nimempikia shemeji yenu njegere ngumu haziivi, msaada tafadhali

ww utakuwa uliweka chumvi mwanzoni maana ukiweka chumvi kwenye njegere au maharage wakati wa kuchemsha hapo utakesha hata masaa 4 na bado kuiva..ukitaka kuiva haraka iwe ngegere,maharage,mbatata au muhogo wa kuchemsha usiweke chumvi mwanzoni ila utaweka mwishoni au wakati wa kuunga..ili kuivisha haraka vitu vya kuchemsha weka mafuta ya kupikia kidogo tu hapo yataiva fasta ndani ya mda mfupi tena pishi linakuwa laini mno na usipokuwa macho baada ya kuweka mafuta ya kupikia utakuta rojo tupu kwani kuiva kwake sio mchezo ukizubaa.!
Hapana mkuu sikuweka chumvi
 
Haya maujuzi utayapata kwa makungwi wazoefu,wanawake wenzako waliofundwa wakafundika kupika,......Kuna siku mama aliyemaliza phD atakuja kuuliza hapa jinsi ya kukata viuno
Sasa unadhani haya maujuzi ya kufanya njegere zilainike ningeyapata wapi zaidi ya hapa mtandaoni? Unadhani ukijifungia tu jikoni bila kutafuta means ya kujifunza ndo utajua kupika?
Dunia ya sasa kila kitu kipo mtandaoni, haikwepeki
 
Haya maujuzi utayapata kwa makungwi wazoefu,wanawake wenzako waliofundwa wakafundika kupika,......Kuna siku mama aliyemaliza phD atakuja kuuliza hapa jinsi ya kukata viuno
Nenda wewe kwa hao makungwi. Sie wengine tupo hapa mtandaoni na tunatamba nao
 
Ipo hivi.
Hizi njegere nimezibandika kuchemsha tangu saa 6 na nusu hadi saa 8 kamili, ni ngumu hazilainiki.
Huyu shemeji yenu hapendi njegere ngumu, sikuwa na jinsi nimeunga hivyo hivyo nikamtengea ale, nipo mahali nimekaa nasubiri bomu lilipuke maana najua atafoka hadi kesho.

Msaada tafadhali jinsi ya kuzitambua njegere ambazo haziivi ili nisifanye kosa la kuzinunua siku nyingine.

Mwachiluwi nipe maujuzi
Ushauri mbovu lakini utasaidia kaa uchi....
 
Njegere kavu ndo mtihani zaidi sasa na zina ukorofi sana. Huko Usukumani Ntuzu kuna njia mbalimbali ambazo nimeshaziona zikitumika ili kuepusha shari (Japo sina uhakika kama njegere ndiyo ndulu)

1. Unaweza ukazikaanga kabla ya kuzipika hasa kama zimekaa muda mrefu. Unazikaanga kavu kavu tu bila mafuta ukiona zimepata moto ndo unazipika. Nusu saa tu zishasalimu amri na hakuna hata moja itakayogoma kuiva.

2. Mpe mtoto wa kike chini ya miaka mitano ndiyo aziweke chunguni. Kama ni zile ngangari zimekaa zaidi ya miaka miwili-mitatu hivi ni lazima awe uchi anapoziweka chunguni. Unaambiwa eti zoooooteee zitaiva chap.

3. Tumia mkono wa kushoto wakati wa kuziweka chunguni. Na unapoziweka usiongee 😳

Kwangu mimi njia ya kwanza tu ndiyo angalau inaeleweka. Njia 2-3 sijui zinavyofanya kazi lakini ukiongea na wenyewe wanawake watakuapia kuwa njia hizo ni konki na hazina kupoteza muda kama hiyo ya kwanza.

Wabeja 🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️
😁😁😁, mkuu
 
Back
Top Bottom