Nimempikia shemeji yenu njegere ngumu haziivi, msaada tafadhali

Nimempikia shemeji yenu njegere ngumu haziivi, msaada tafadhali

Njegere kavu ndo mtihani zaidi sasa na zina ukorofi sana. Huko Usukumani Ntuzu kuna njia mbalimbali ambazo nimeshaziona zikitumika ili kuepusha shari (Japo sina uhakika kama njegere ndiyo ndulu)

1. Unaweza ukazikaanga kabla ya kuzipika hasa kama zimekaa muda mrefu. Unazikaanga kavu kavu tu bila mafuta ukiona zimepata moto ndo unazipika. Nusu saa tu zishasalimu amri na hakuna hata moja itakayogoma kuiva.

2. Mpe mtoto wa kike chini ya miaka mitano ndiyo aziweke chunguni. Kama ni zile ngangari zimekaa zaidi ya miaka miwili-mitatu hivi ni lazima awe uchi anapoziweka chunguni. Unaambiwa eti zoooooteee zitaiva chap.

3. Tumia mkono wa kushoto wakati wa kuziweka chunguni. Na unapoziweka usiongee 😳

Kwangu mimi njia ya kwanza tu ndiyo angalau inaeleweka. Njia 2-3 sijui zinavyofanya kazi lakini ukiongea na wenyewe wanawake watakuapia kuwa njia hizo ni konki na hazina kupoteza muda kama hiyo ya kwanza.

Wabeja 🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️
Njegere na usukumani wapi na wapi? hizo unazozungumzia ni Nduru (CHOROKO).
 
Enzi za utafutaji ili kubana matumizi na mimi nilinunua maharage.

Aloo yale maharage nilikua napika kiasi kidogo sana ila vile vyuma vilikua haviivi dadeki, nikawa namaliza gesi kindezi tu. Sijui maharage ya wapi yale, hayalainiki hadi mwisho wa siku nayala kama karanga tu.
 
Ipo hivi.
Hizi njegere nimezibandika kuchemsha tangu saa 6 na nusu hadi saa 8 kamili, ni ngumu hazilainiki.
Huyu shemeji yenu hapendi njegere ngumu, sikuwa na jinsi nimeunga hivyo hivyo nikamtengea ale, nipo mahali nimekaa nasubiri bomu lilipuke maana najua atafoka hadi kesho.

Msaada tafadhali jinsi ya kuzitambua njegere ambazo haziivi ili nisifanye kosa la kuzinunua siku nyingine.

Mwachiluwi nipe maujuzi
week moja kwenu ukajifunze kupika njegere ziisizoiva ziive...
 
Enzi za utafutaji ili kubana matumizi na mimi nilinunua maharage.

Aloo yale maharage nilikua napika kiasi kidogo sana ila vile vyuma vilikua haviivi dadeki, nikawa namaliza gesi kindezi tu. Sijui maharage ya wapi yale, hayalainiki hadi mwisho wa siku nayala kama karanga tu.
Ungekuwa ukiyaloweka kwanza kabla hujachemsha. Mfano unaloweka usiku kwaajili ya kuchemsha kesho yake
 
Enzi za utafutaji ili kubana matumizi na mimi nilinunua maharage.

Aloo yale maharage nilikua napika kiasi kidogo sana ila vile vyuma vilikua haviivi dadeki, nikawa namaliza gesi kindezi tu. Sijui maharage ya wapi yale, hayalainiki hadi mwisho wa siku nayala kama karanga tu.
Kuna maharage ya hivyo sijui wanasema yamekaa sana.
 
Back
Top Bottom