Uchaguzi 2020 Nimemsikiliza sana bwana Lissu nikaelewa yafuatayo

Uchaguzi 2020 Nimemsikiliza sana bwana Lissu nikaelewa yafuatayo

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Kwa mtu anaekusudia kukiondoa madarakani chama kinachotawala huna budi kufanya homework yako vizuri ili uyaongelee mambo ya wananchi ambayo serikali iliyopo madarakani aidha iliyatelekeza au haijafanya vizuri.

Cha ajabu namuona huyu mheshimiwa amelipa uzito mkubwa sana suala la yeye kupigwa risasi, kufuta vitambulisho vya machinga, kuwatoa mashekh wa uamsho, kuzungumzia mambo ya korona akisisitiza mambo ya barakoa huku yeye mwenyewe akiwa hajavaa na kuwakusanya vijana kwa maelfu bila kuzingatia tahadhari yoyote nk kwa maoni yangu hizi hoja zitampuguzia kura.

Nashauri ajikite kutibumakovu yaliyoko kwenye mioyo ya watanzania walio wengi ambayo yamekua kero sugu na ccm haionyeshi Kama Ina iwezo wa kuyatibu Kama vile ukosefu wa ajira, maonezi na unyanyasaji wa Viongozi wa Serikali hasa wateule kwa watumishi wa umma, ukosefu wa soko la mazao ya kilimo, Serikali kushindwa kuwekeza kwenye sekta zinazoajiri watu wengi Kama vile kilimo, uvuvi, ufugaji na changamoto zilizoko kwenye sekta mbalimbali.
 
Umeona ameongelea jambo hilo kwenye Mkutano wa Nini?

Je Kampeni imeanza mpaka azungumze mambo hayo?

Unadhani wewe unamzidi Lisu akili mpaka ashindwe kujua jambo dogo kama hilo unalolizungumzia ambalo hata asiyesoma anaweza kulifahamu?
jambo lililompata lisu ni sehemu ya usalama brother,insecurity ni moja ya sababu ya political instability,
 
Tundu Lissu anagonga pale ambapo roho za watanzania zinapotaka kusikia

Mashekhe wa Zanzibar kawaongelea na watu wanaoonewa huko Magerezani nao kawaongelea

Kwa ujumla Lissu ni mwanasheria kaanza n uonevu na zulma sasa atakuja chizi flani ataongelea Ndege za kupeleka maea hostage india
 
Lisu ana SONONA
FB_IMG_1596790033084.jpg
 
Hivi huyu Lissu ana nini mbona watu mnaweweseka sana. Yaani kila dakika mnamuongelea yeye tu.

Mi nilidhani kushindwa kwake kuongelea sera ingekuwa ndio furaha yetu kwamba kampeni zetu zitakuwa nyepesi maana mshindani wetu hana sera. Hofu yetu juu ya Lissu inapelekea wafuasi wetu kuanza kuwa na wasiwasi kwamba Lissu ana kitu cha ziada ambacho hakijawekwa wazi ndio maana kila dakika tunaongea habari zake ili hali washindani wetu ni wengi. Kuna Lipumba, Membe, Shibuda, yule wa Nccr n.k.

Tuachane na habari za Lissu tujikite kwenye kuandaa mikakati ya ushindi.

Sent from my A37f using JamiiForums mobile app
 
Kama ni utunzi wa kitabu, alichokifanya Lissu ni "preamble" tu. Kwa kuwa hapo wala hakuwa akiinadi ilani ya chama chake, isipokuwa alikuwa ktk zoezi la kuwasaka wadhamini wake huku akiwapa tu "hints" chache wananchi juu ya serikali yao sikivu.

Watu waliojitokeza kwa wingi kumlaki kwa kuwa "walimmisi"' kweli kweli jukwaani kwa kipindi kariba cha miaka mitatu tokea lile dhahama la watekelezaji wa uhalifu waliofichwa kwa kutumia lugha ya "wasiojulikana" na huku wale wapanga mikakati ya uhalifu huu wakiwa na dalili zote za kuanza kujulikana na kuonyesha kupata mchecheto, na kuanza kumuundia kila aina ya zengwe ili apate kutenguliwa mapema na NEC.
 
Hujamwelewa hata kidogo..... Lissu ana akili nyingi anahitaji wenye akili timamu kumwelewa.... (Kusoma sio kua na akili)

Endelea kumsikiliza zaidi utamwelewa tu akiamza kampeni
 
Tulio wengi tunajua au kwa lugha rahisi tumeona majeraha ya Tundu Lissu si jambo la kubeza hata kidogo ashukuriwe Mungu kwa kumvusha katika ajali ile, Lakini swali langu ambalo limetanda ndani ya kichwa changu ni juu ya zile picha za gari ambalo alishambuliwa Mh Lissu. Iliwezekana vipi au ndo miujiza bado akili yangu inawaka moto, but in all tuzidi kuliombea Taifa letu
 
Back
Top Bottom